Dumelo
Senior Member
- Apr 23, 2015
- 139
- 235
Kwanza nianze kwa kusema kuwa Mimi si Fani wa DIAMOND Isipokua napenda Muziki Mzuri anaofanya, Pamoja na Jitihada, Bidii na Discipline aliyonayo katika kufanya kazi zake. Sitaki kuingia kwenye Ugomvi au Maneno au Ushauri ambao Kaka yangu Eric Shigongo ameutoa kwa Managers wa Diamond.
Hoja yangu mm ni kwamba ni Lazima tukubali kuwa Diamond amefika hapo alipo kutokana na Jitihada, Kipaji, Uchu wa mafanikio pamoja na Discipline ya Muziki wake. Swala alilotoa Le Mutuz kuwa Babu Tale na Sallam ndo Mameneja Bora wa Wasanii hapa Bongo, ni uwongo mkubwa, kwani Ili hawa mameneja wa Diamond waonekane ni mameneja Bora, ni Lazima tuone uwiano sawa wa mafanikio ya kumziki kwa wasanii wengine ambao pia wako chini yao, mfano Tiptop, Chege, Temba, Yamoto, Madee, na Tunda.
Ukiangalia hawa wasanii wamepotea kabisa kwenye game, hawana muelekeo mzuri kimziki, hawana mafanikio aliyonayo Diamond, hawafanyi show kama anazofanya Diamond, ndani na nje. Je, swali la kujiuliza ni kwamba kwann kama wao ni mameneja wazuri kwann wameshindwa kuwaweka juu kimziki hao wasanii? Je hawana kipaji kama diamond?
Je, kwanini tusikubali kwamba, kwa vile Diamond kwa kipaji chake, jitihada na Discipline aliyonayo ndo.imewavutia hawa mameneja? na hivi sasa Nguvu, akili na macho yao yote wameangalia kwa diamond maana wanajua diamond ni bidhaa au Brand inayojiuza kwa Sasa na hata bila wao bado angeweza kujiuza tu.
Kuna wakati hao walijiona wao ndo wameshika mziki wa Bongo, lakini ukweli ni kwamba wapo kwa Diamond kimasilahi, siku diamond akichuja watamkimbia tu. Hilo ndilo tatizo la kuwa na managers ambao hawajaenda shule, full Uswahili.