Rabin
Senior Member
- Mar 21, 2009
- 181
- 39
Wana jamvi habari zenu, nimekuwa nikijiuliza kila wakati na sipati jibu hasa ninaposoma au kuona habari na maagizo ya kiserikali kupiga marufuku uingizaji wa bidhaa ambazo zinaua masoko ya bidhaa zetu zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani ambapo hupelekea pia kuwakosesha wakulima mapato kwa maana ndiyo wazalishaji wa malighafi husika za viwanda vya ndani, LEO ningependa kuleta huu uzi hapa hasa uingizaji wa sukari na mafuta ya kula kutoka nje, kwa wale wakazi wa maeneo ya Bunju, Boko hadi tegeta watakubaliana nami kuhusu kasi ya uingizaji wa sukari kutoka BRAZIL ilivyoongezeka kupitia bandari bubu hizi, tunashuhudia madereva wa bodaboda wanvyoshiriki kikamilifu tena wakikimbizana barabarani kwa mwendo mkali na hatari ili kufanikisha zoezi , mara nyingine hupata ajali mbaya sana hupoteza hata maisha yao, usiku kucha pikipiki zinapita zikisafirisha SUKARI ya brazil na mafuta ya kula mengi tu ambayo bado sijajua yanatoka wapi lakini sijui kama yana viwango na yanafaa kwa matumizi ya binadamu.
Ukupita kwenye maduka mengi maeneo niliyoyataja hapo juu sukari inayouzwa ni ya BRAZIL na mafuta ya kula wanajua wao yanakotoka, najiuliza hivi POLISI na TRA na mamlaka nyingine hawalioni hili? hata mifuko ya sukari ni dhahiri imeandikwa THE PRODUCT OF BRAZIL, sasa hivi ni kweli hawalioni? nashangaa tena eti siku hizi kasi ndiyo imezidi mno usiku ni hatari zaidi badaboda wanavyosomba mizigo hiyo, hivi watendaji wa MAGUFULI hawajui au hadi magufuli mwenyewe aje atumbue hili jipu? nawakilisha.