Bidhaa feki zamkera Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bidhaa feki zamkera Rais Kikwete

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, May 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete.  Rais Jakaya Kikwete, amesema bidhaa feki zinazoingizwa nchini, zimekuwa kero katika maeneo mbalimbali na kuwataka wadau, wakiwamo wafanyabiashara na wawekezaji kushirikiana na serikali kutafuta njia ya kuzikomesha.
  Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa Taasisi ya Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji barani Afrika (ICF), uliowashirikisha viongozi wa ngazi mbalimbai serikalini, marais na mawaziri wakuu wastaafu na wadau wengine, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuzungumzia na kuweka mikakati ya kuimarisha uwekezaji.
  “Bidhaa za bandia ni moja ya tatizo katika nchi zetu, tunapaswa kutafuta njia ya kukomesha hali hii. Bidhaa feki zipo katika dawa, vyakula, vifaa mbalimbali na katika nguo,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
  Alisema tatizo kubwa linalochangia kuwapo kwa bidhaa feki ni wafanyabiashara, ambao ndio wanaonunua bidhaa na kuingiza nchini na kwamba, baadhi yao si waaminifu, lakini wadau hao wakishirikiana na serikali husika inaweza kusaidia kupunguza ukubwa wa tatizo.”
  “Hivi karibuni nilikuwa katika mkutano Uganda, wafanyabiashara wakawa wananiuliza serikali inafanya juhudi gani kukomesha bidhaa feki. Jibu ambalo nimewapa ni kuwa wao ndio wanatakiwa kutafuta ufumbuzi kwani ndio wanaoingiza bidhaa. Serikali ikipata ushirikiano kutoka kwao ufumbuzi utapatikana,” alisema.
  Alisema Tanzania imekuwa na mikakati ya kuweka vivutio vya uwekezaji hivyo wanaotaka kuwekeza ni wakati muafaka.
  Alisema sera ya nchi inatambua umuhimu wa uwekezaji na ndio maana kuna Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambacho muwekezaji anapokuja anaweza kupata taarifa mbalimbali, zikiwamo za eneo analotaka kuwekeza, huku mazingira mazuri ya uwekezaji yakitokana na utulivu na amani iliyopo na juhudi zinazochukuliwa katika kuboresha baadhi ya sekta muhimu, kama vile Bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Kuhusu mgomo wa wafanyakazi aliwaomba wawekezaji kutokuwa na wasi wasi na hali hiyo kwani tayari wameishughulikia na isifike wakati wakaona kuwa Tanzania wafanyakazi wake ni watu wa migomo. Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfBD), Dk. Nkosana Moyo, alisema pamoja na mambo mengine ya uwekezaji bado wawekezaji wadogo nao wanatakiwa kupewa nafasi kwa kila nchi.
  Wadau walikubaliana kuweka mikakati ya kuhakikisha sekta ya uwekezaji inapewa nafasi. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa na ushawishi ambao utawafanya wawekezaji kuwekeza na hatimaye kujenga uchumi imara wa nchi za bara hilo. Baada ya mkutano huo kumalizika na kufikia maamuzi hayo, Mkurugenzi Mkuu wa ICF, Omar Issa, alisema maamuzi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji yamefikiwa kutokana na maoni ya walioshiriki.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Lakini Mheshimiwa si ndio mwaka 2006 alipokuwa akijibu maswali ya Waandishi wa habari alisema Bidhaa feki wacha ziingie kwa kila mmoja ana uwezo wake wa kununua bidhaa. Kuanzia hapo ndiyo Wafanya biashara wakaanza kuchangamka. sasa tatizo limeshakuwa kubwa sana.
   
 3. M

  MJM JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  ]Kuhusu mgomo wa wafanyakazi aliwaomba wawekezaji kutokuwa na wasi wasi na hali hiyo kwani tayari wameishughulikia na isifike wakati wakaona kuwa Tanzania wafanyakazi wake ni watu wa migomo. Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfBD), Dk. Nkosana Moyo, alisema pamoja na mambo mengine ya uwekezaji bado wawekezaji wadogo nao wanatakiwa kupewa nafasi kwa kila nchi.


  Kwani kule kwao wafanyakazi hawagomi? Njia bora ya kutatua matatizo ya wafanyakazi ndiyo inahitajika kuwa emphasized.
   
Loading...