Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
19,035
28,669
Habari za mchana wakuu kama kawaida huwa nakuja na mada za kuchokoza fikra zetu hasa kwenye mambo ya kiimani hivyo mada hizi sio za kukosoa dini fulani au vitabu vya imani ila ni kuhoji tu ili tupanue fikra zetu kwenye masuala haya kwa faida yetu sote so sitegemei iibue mijadala ya kidini bali kuelimishana juu ya mambo haya baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye mada husika ya leo.
images (81).jpg

Biblia na umri wa Dunia
Mwaka 1650 professor wa masuala ya theologia na Askofu wa makanisa ya protestant wa Ireland John Ussher aliandaa maandiko yake kupitia mfululizo wa vitabu vyake kuanzia cha Annals of the Old Testament: Origins of the world ambacho ndani yake aliibua mjadala mpana sana wa karne nyingi sana. Ussher alipiga hesabu ya muda ulivyopita kati ya Adam kuumbwa hadi Yesu kuzaliwa na kugundua kwamba ni miaka 4000 imepita tokea Adam aumbwe hadi Yesu kuzaliwa hivyo kufanya dunia yetu ikiwa na wanadamu kuwa na miaka elfu 6 pekee mpaka sasa!!. Ussher alitumia maandiko kama chanzo cha nadharia yake alitumia nyaraka za masoretic zilizotumika kuandaa Biblia za agano la kale ili kuweza hesabu umri wa Adam hadi vizazi vya Abraham hadi kufikia Yesu na baada ya mnyambuliko huo alifanikiwa kugundua kwamba dunia iliumbwa usiku wa October 23 4004 kabla ya kristo.

Young Earth Creationists
Vuguvugu hili la YEC lilianza miaka ya 1960 ambapo iliasisiwa na wasomi 9 chini ya PhD wa theolojia na uhandisi Bwana Henry Morris wakijikita kwenye utafiti wa uhalisia wa umri wa dunia na uumbaji na wakahitimisha rasmi kuwa dunia tunayoishi iliumbwa ndani ya miaka elfu 10 pekee na sio zaidi ya hapo na wao pia walitumia maandiko ya Biblia ya kiebrania ili kufikia hitimisho hilo hivyo na wao wakaunga mkono hoja za hapo nyuma za Professor John Ussher na hata leo hii wameweza shawishi zaidi ya 40% ya wakazi wa marekani kwa takwimu za 2017 wanaamini nadharia hii kwamba uumbaji wa dunia ni kwa mujibu wa Biblia hauzidi miaka 10,000 iliopita.

images (79).jpg

SAYANSI inasemaje??
Baada ya sayansi na teknolojia kukua na kuongezeka vifaa vya kupima umri wa miamba,mazao na mifupa ya wanyama wakaibuka wasomi wa sayansi waliohoji kuhusu uhalali wa nadharia hizi na imeleta utata na mjadala mzito kwa miaka mingi sasa. Mwanasayansi wa karne ya 20 Clair Cameron Patterson baada ya tafiti kadhaa juu ya miamba akagundua ulimwengu toka uanze una miaka billion 4.5 na baadae wanasayansi mbalimbali wakaja na tafiti mbalimbali zikidai kwa usahidi wa kisayansi na kiacholojia kwamba uhai duniani umekuwepo miaka takriban 3.8 Billion iliopita hivyo kukinzana kabisa na nadharia hizo mbili za juu kuwa Biblia

Jinsi ya kupima
Kwa upande wa Young Earth wao wanalalia maandiko kwa kiasi kikubwa na kupiga hesabu miaka ya kibiblia tokea Adam hadi Yesu lakini wanasayansi wamepiga hesabu zao kwa ushahidi wa kushikika wakitumia mfumo unaitwa radiometric dating ambacho kinapima miamba hasa stage tofauti za jinsi miamba inavyooza na ambapo kila stage ina umri wake yake yaani miaka kadhaa ili ifike stage nyingine ya kuoza hivyo wanapiga hesabu kuanzia layer ya mwisho mpaka ya kwanza na kufikia hitimisho la umri wa mwamba huo na wakafanikiwa kugundua mwamba wa kwanza ulitokea miaka 3.8 Billioni iliyopita.
images (80).jpg

Utafiti wangu (Primary)
Binafsi nilichukua hatua kuonana na wanatheolojia kadhaa kutoka chuo fulani cha Biblia wenye ngazi ya PhD na wamenijuza kwamba Biblia haikuandikwa kwa maneno bali mafumbo hivyo isitafsiriwe kwa maana zetu bali kwa mafunuo na maana zilizo kwa Biblia... Mfano wanadai Dunia haikuumbwa kwa siku 7 kama zetu hizi bali miaka mamilion na wakaenda mbali kusema Biblia haikuanza kuandika matukio yote bali imeandika matukio juu ya watu waliochaguliwa tu hivyo wanakiri kuwa kweli dunia ina miaka mabillion na sio miaka elfu 6 pekee bali wanaotafsiri maandiko kwa akili zao ndio wanapotosha sababu wameitafsiri maneno kama yalivyo badala ya kutafuta maana ya hayo mafumbo na wakanipa mistari michache.

Yohana 16:25
25 Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.

Na wakaenda mbali kusema hata hayo mafumbo walioambiwa kuandika Biblia hawakuyaelewa sababu ni siri imewekewa hadi wakati muafaka yaani mwisho wa dunia ufike soma hapa kisa cha Daniel

Daniel 12:4
4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

Hapa tunaona kuna maandiko na nabii zimefichwa kwa uelewa wetu kabisa hata Daniel hakuelewa!!

Daniel 12:8-9
8 Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?
9 Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa
mwisho.

Hivyo kama hata Daniel kuna baadhi ya vitu alifichwa na mpaka anaandika hakuvijua basi hata sisi hatuwezi vijua mpaka siku ya mwisho hivyo wakahitimisha mjadala kwa kusema huenda ni kweli dunia ina 4.5 Billion years ila sio 6000 kama YEC inavyosema maana Biblia haielezi hicho kuwa ni miaka 6000 bali watu wanatafsiri maandiko kwa akili zao ilihali YAMEFICHWA!!
images (78).jpg

Hitimisho
Ukinzano huu kati ya maandiko na sayansi juu ya asili ya umri wa ulimwengu umezua mjadala mpana sana huku kila upande ukivutia kwake nikaona kwa kuwa JF ni kisima cha maarifa nilete hii mada ili tuweze kufikiria pamoja je umri wa dunia upi ni halisi

4.5 Billion ama 6000?

Naomba kuwasilisha
 
Wamepima kuanzia Adam alipoumbwa!
Mbona tunasoma humu ndani Kuwa Dunia ilikuwa ina watu kabla ya Ujio wa Adamu?

Samahani kama nitakuwa sijaeleweka maana sipo vizuri kwenye hizi mambo.
Mkuu hiyo ya Adam kuwa wa kwanza au lah ni mada pana sana inayostahili uzi wake na ntakuja kuielezea siku nyingine ila kwa sasa tunajikita umri wa Dunia iwe na wanadamu ama lah kupitia hoja za hao YEC/Ussher Vs wanasayansi je nani mkweli juu ya umri wa dunia??
 
Kwa kuwa huuuu ni mjadala huu, Maoni yangu ni kuwa Dunia hii ina umri mrefu sana kuliko miaka 6,000/=. Aidha mwanadamu atakuwa na umrefu mrefu kushinda hiyo miaka 6000.

Machache ninayoelewa kutoka ndani ya kitabu kitukufu cha Qur'an ni kuwa: Ulimpitikia umri mrefu sana (Dahari ya miaka) mwanadamu alikuwa sio kiumbe mwenye kutajwa katika dunia hii.

Qur'an 76: 1 - 3
Hakika kilimpitia binadamu kipindi (dahari) katika zama ambacho kwamba hakuna kitu kinachotajwa.
Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hiyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
Hakika Sisi tumembainishia njia, Ama mi mwenye kushukuru, au ni mwenye kukanusha.

Kwa hiyo, ni wazi kuwa kulikuwa na kipindi kirefu sana toka Dunia ilipoumba kama zao la Big Bang hadi pale mwanadamu (Adam) alipoumbwa na kuletwa Napa duniani.
Sihitaji kuhoji umakini wa vifaa vilivyotumika kisayansi kupima umri wa Dunia na kuja na conclusion ya 4.5B years lakini dunia ina umri mrefu sana kuliko umri halisi wa mwanadamu.
 
Je wana uhakika gani Rock waliyopima Ndo rock ya Toka Ulimwengu kuumbwa?

Vifaa vyao Vimedhibitishwa na Nani ?
Vimethibitishwa na uwezo wake wa kutambua mfano ukilifukia fuvu lako leo kwa siri mpaka mwaka 2020 wakilichimbua wakipima wanagundua lina miaka miwili tu hivyo baada ya kutumika kupima miamba mingi na elementa zingine kwa mafanikio na kuweza kuthibitisha umri wake basi ndipo ilipopata credibility
 
Kuna tofauti kubwa kati ya ulimwengu (universe) na dunia (world), ukiyaelewa haya maneno mawili huwezi kupata shida kujiuliza maswali kama haya...
Kumradhi mkuu nami nimeliona hilo kosa nilitaka kumaanisha dunia tunayoishi i hope kwenye maelezo ya uzi umeliona hilo

Karibu kwa mchango
 
Hoja ya kuwa dunia ina miaka takribani 6000 sio kweli kwasababu kuna baadhi ya maandiko yanasema kuna viumbe walipata kuishi duniani kabla ya Adam kuumbwa.Mungu aliwaondoa viumbe hao baada ya kuleta machafuko ikapita million years ndo akaja kuumbwa Adam.
Nadhani kutumia bible pekee ili kuelezea umri sahihi wa dunia ni kutokuvitendea haki vitabu vingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom