Bibi yangu Litabhori Uongozi wa Kijiji umekushinda, achia ngazi

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!.

Tangu alipofariki babu yangu mzee Nyanchabhakenye, mzee wa kimila wa kijiji akakupitisha ukawe msimamizi mkuu wa kijiji kwa kuwaongoza wana Mogabiri hadi pale watakapopata kiongozi mwingine, sasa ulipofika hapo kijijini ulikuta wanakijiji wengi wanaishi maisha ya umasikini wa kutupa na ufukara uliopendezesha mifuko ya suruali na sketi zao.

Ulipopata idhini ya kuongoza kijiji hicho wengi walitarajia utakuja na mpango mkakati wa kupunguza umasikini kwa wanakijiji na kuongeza uchumi wao, lakini jambo la kusikitisha umasikini umeongezeka maradufu zaidi hata ya utawala wa babu na pia umekuwa ukienda kukopa mikopo nje ya kijiji hicho kizuri cha Mogabiri ili familia yako pendwa na ndugu zako washibishe matumbo yao.

Leo kulikuwa na upokewaji na usomaji wa ripoti ya kijiji kulikoletwa kwako na mkuu wa Ukaguzi wa kijiji hiki mtiifu wa kijiji bwana Matiko Machori, ripoti hiyo imepokelewa na wewe kipenzi chetu mzaliwa wa Ukerewe Bi Litabhori Mwajuma Sikosei, kiukweli nikiri hadharani ya kwamba, hapa Babu alipata msaidizi.

Tatizo lako Bibi yetu kipenzi unachokosea ni kwamba hauendani na mapigo ya midundo ya wana Mogabiri, wakati unakabidhiwa kijiji ulikuta wacheza Ritungu wanacheza Rege, ulikuta wacheza Rirandi wanacheza dogori, sasa wewe umekuja unataka kubadirisha iwe kinyume chake, hapo ndipo Bibi Litabhori unapotaka kukosea.

Leo wakati naongea na binamu yangu Mbusiro Kamona aliyeko hapo Mogabiri ameniambia umechukia kweli kweli na ameniambia uenda ukawabadiri watendaji wakijiji ili wafuate unayoyataka.

Naomba nikuambie Bibi ya kwamba, kuwabadiri watendaji wa kijiji siyo suluhisho, Babu aliwafukuza katika utendaji wa kijiji na aliwafungulia mashitaka pale Mahakama ya wilaya ya Tarime na wengi walizitapika pesa walizokuwa wamezila au walifukuzwa kazi kabisa.

Tatizo lako Bibi yangu ni kwamba, watu waliofukuzwa kazi na Babu kwa utendaji wao mbovu hapo Kijijini, wewe ndiyo umewateua tena kuwa watendaji wakuu wa kijiji cha Mogabiri. Kijiji hicho kilichojaa rasilimali za kila aina kimegeuka shamba la "kila mtu ale anavyojisikia na akichoka amwachie mwanae".

Maoni yangu kwako Bibi.

Naomba uchukue hatua kwa kila mtendaji hapo kijijini kwasababu wengi wanakudharau huwezi kuwachukulia hatua kwakuwa unamaslahi nao,pia wanasema huko kwenu Ukerewe huwa mnamwambia mwizi atangulie polisi mtamkuta huko;Bibi yangu hapo kijijini ukimwambia mwizi atangulie polisi mwenyewe bila kumpiga "Tanganyika Jeki" hakika hutomkuta Polisi bali utamkuta anakung'uta pombe na wasimbe pale Tarime mjini kwenye klabu maarufu ya JJ na ukimfumania atakwambia "ACHA KUHANGAIKA NA KIJIJI CHA GIZA, KAA HAPA UAGIZE PAJA LA KITIMOTO ULE UNYAMAZE".

Bibi ukiona umewashindwa sana watendaji wako kwa kuwaogopa nadhani uachie ngazi ili Bwana Matiko Mnanka Kiseri aliyekuwa mtendaji mkuu wa babu ashike uongozi kwasababu huyu wakati wa babu alikuwa mkali sana na bila shaka ataendeleza ukali wake hata atakapokuwa kiongozi wa kijiji.

Bibi una mamlaka,una jeshi la Sungusungu,Una Jeshi la Mgambo,Una jeshi la Wakurya waliotahiriwa kwa kisu bila Ganzi lijulikanalo kama ABHAGHAKA lakini kwanini unawaogopa watendaji wako uliowateua wakusaidie?,Je,huoni hapa wana Mogabiri tutahoji kwanini huwatimui?.

Mogabiri ni kijiji kikubwa kuliko hata vijiji vya Bhakenya na Bhaganda lakini umeendelea kukifanya kijiji hiki kuwa "SHAMBA LA BIBI WA MOGABIRI".

Hii haikubariki Bibi,tafadhali tuachie kijiji chetu.

#Ukilala nayo hakikisha unaamka nayo.

Ni hayo tu kwa Leo Bibi yangu Kipenzi Litabhori Mwajuma Sikosei.
 
hahaaaaaa tatizo Babu nae alikuwa anakurupuka mno kipindi akiwa kiongozi ndo maana kila kitu kizuri alitaka ajenge kwenye kitongoji chake cha Komaswa na kuacha vitongoji vingine vikiwa masikini pia babu bhana aliwapendelea sana Wairege ila wakira wakenye na wanyabhasi hata hakuwa na mda nao ndo maana na wao wanafukia pale alipochimba.

Nikukumbushe pia babu unakumbuka aliwahi kumkata na panga Mwita Marwa kwa sababu ya kuuliza matumizi ya mali za kijiji.

Tumuache Bibi yetu wa Ukerewe amalizie mda wake huenda tukabadilisha viongozi wa kijiji ambao watatusaidia zaid ya huyu bibi wa Ukerewe.

Eeeee nimekumbuka hebu ngoja nikaangalie pale kwenye tambara nasikia msaidizi wa mwenyekiti wa kijiji cha Wegero amekuja ngoja nisikie anasema nn huenda Mazur yaliyopo Wegero yakaja na huku kwetu Mogabiri
 
Mama analialia bila kuchukua maamzi, sisi wananchi wa kawaida tumsaidieje hahahahaaaa

Wanangu wapigaji huu ndiyo muda wa kupiga kama hata mwenye maamzi ya mwisho analialia Nan atatufanya kitu?

Tupige kadri tuwezavyo

Hawa wa chini wakitaka kuchukua hatua wape rushwa kadri ya upigaji wako.

Muda ni huu kesho anaweza akaja kama mwenda zake akatudhibiti jamani tupige pesa kwa moyo nakwa nguvu zote
 
Mama ana haki ya kuwa na hasira na kukemea na kutukana. Hana kashfa ya wizi hata kabla hajawa makamu na rais. Lakini Magufuli kaanza kuiba toka 1995(unabisha?). Na akavunja rekodi ya wizi tangu tupate uhuru kwa kukwapia 1.5 Trillions.

Na bila aibu akaiba rambirambi mchana kweupeee (unabisha?) Cha kushangaza huyo huyo Magufuli mwizi wa matrillion alikuwa anawakashifu wengine kwa wizi tena kwa ku bagua. Alikuwa hana moral authority ya kuwasema wengine wezi wakati yeye Magufuli alikuwa the greatest thief of all.

Mama ana haki ya kuwa mkali na uchungu
 
hahaaaaaa tatizo Babu nae alikuwa anakurupuka mno kipindi akiwa kiongozi ndo maana kila kitu kizuri alitaka ajenge kwenye kitongoji ...
Babu Magufuli lilikuwa jizi toka 1995. Halafu lenyewe halikuwaga na aibu likija swala la kiiba hadi rambirambi. Halafu cha kuchekesha eti alikuwa akipigana na mafisadi. Aliita wengine wezi wakati yeye ndo kinara wa wizi.
 
Tatizo bibi anacheka nao Sana akifika sehemu Kijijini hakuna mtendaji anae muogopa ili aheshimike inabidi akunjue makucha awe mkali kweli kweli sisi Wana Kijiji kwenda kunywa maji bila kutupeleka kwa fimbo muda mwingine hatwendi
 
Tatizo bibi anacheka nao Sana akifika sehemu Kijijini hakuna mtendaji anae muogopa ili aheshimike inabidi akunjue makucha awe mkali kweli kweli sisi Wana Kijiji kwenda kunywa maji bila kutupeleka kwa fimbo muda mwingine hatwendi
Kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom