Bibi wa Miaka 102 Aanza Shule ya Msingi

Bibi wa Miaka 102 Aanza Shule ya Msingi

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
1,672
Reaction score
184
4345714.jpg

Bibi Ma Xiuxian akiwa darasaniTuesday, April 13, 2010 2:33 AM
Bibi mmoja nchini China amekuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani baada ya kuamua kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka 102.Ma Xiuxian, kutoka Jinan, katika jimbo la Shandong alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuanza elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 102.

Ma alianza kufanya kazi kwenye kiwanda cha nguo tangia alipokuwa na umri wa miaka 13 na kwa miaka yote aliendelea kufanya kazi huku akiwa na ndoto ya kuwa na angalau elimu ya shule ya msingi.

Ma aliolewa akiwa na umri wa miaka 18 na alifanikiwa kupata watoto tisa, saba kati yao ni wahitimu wa shahada ya kwanza ya chuo kikuu.

Ma alipewa nafasi ya kusoma kwenye shule hiyo baada ya kulieleza gazeti moja la mjini mwake kuwa alikuwa na ndoto ya muda mrefu sana ya kwenda shule.

"Nina furaha sana nimeweza kutimiza ndoto yangu ya kwenda shule ingawa katika umri huu", alisema Ma.

Ma alienda shuleni akisindikizwa na mwanae wa mwisho wa kiume Yi Fengxin mwenye umri wa miaka 58.

Katika somo lake la kwanza katika shule yake ya Weishan Road Primary School, Ma alisema "Nawashukuru walimu wangu, nawashukuru wanafunzi wenzangu nawaahidi nitajisomea kwa nguvu zote na nikimaliza shule nitasaidia kulijenga taifa".

Ma anatumia kifaa cha kumsaidia kusikia vyema ili aweze kuwasikia walimuwa wake vizuri na huwatumia wanafunzi wenzake kumsaidia kusoma vitabu vya masomo yake.

Ma ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mwanafunzi mzee kuliko wanafunzi wote duniani.
 
Kweli elimu haina mwisho..duh ngoja nami nijikongoje angalau niende nijiunge na Ngumbalu hizi za Kata...ali maarufu Voda fasta
 
Atasaidiaje kujenga taifa wakati nguvu zenyewe hana

She dont' have to be physical, she could contribute even by advicing through life experience, and also...age aint nothing but a number dear!, this tells not to loose hope, she wanted to go to school and she's fulfiling her wish, good for her.
 
Back
Top Bottom