Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Bikra, Jun 30, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Habari Wana JF !

  Naomba kama kuna Mtu Yoyote anajua Historia ya Bibi Titi anijuvye.

  Huyu Mama anaonekana kutajwa sana hapa Tanzania Mpaka kuna Barabara inaitwa Bibi Titi Street, Je Huyu alikua ni Mwanasiasa au ?

  Umaarufu wake unatokana na Nini ?

  Wadau Naomba Majibu yatakanifunua Macho na Kujua Historia ya Taifa Letu.

  ----------------------------------------------------------------------------------------------------
  Kwa habari zaidi zinazo Mhusu Soma Hapa
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  alikuwa mpigania uhuru wa Tanganyika pekee mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele....pia alikuwa mtuhumiwa wa uhaini kwa kutaka kumpindua nyerere miaka hiyo ya nyuma kweusi....lol
   
 3. K

  Kinto Senior Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hisani ya Wikipedia,

  Bibi Titi Mohammed (1926–2000) was a Tanzanian politician. She was born in 1926 [1], in Dar es Salaam, Tanzania to a Muslim family. She was a close friend of the first President of Tanzania, Julius Nyerere being introduced to him in 1954, by the driver of a family cab.[2]

  Mohammed was one of the founding members of the Tanzanian African National Union (TANU), and played a major role in fighting for Tanzania's independence.

  In October 1969, Mohammed, and the former Labour Minister Michael Kamaliza were arrested, along with four army officers, being charged with plotting to overthrow the government.[3]

  Tanzania's first treason trial was held, and after the 127 day trial, Mohammed was sentenced to life imprisonment.

  Two years later, in April 1972, Mohammed received a presidential pardon. Upon her release, Mohammed led a life of isolation. Her husband had abandoned her during the trial, her political associates disowned her, and most of her friends deserted her.

  In 1991, when Tanzania was celebrating 30 years of independence, Bibi Titi appeared in the ruling party's paper as "A Heroine of Uhuru(Freedom) Struggle".

  On November 5, 2000 Mohammed died at Net Care Hospital in Johannesburg where she was being treated.[4]

  One of Dar es Salaam's major roads is named after Mohammed in honour of the great achievements made by her toward Tanzanian independence.
   
 4. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Bititi alikuwa mpigania haki kwa nchi hii ,lakini binafsi siami kama walivyokuwa hawamini watu wengi kuwa huyu bibi alitaka kumpinduwa Rais Kambarage, sababu kubwa ya kushukiwa kuwa alitaka kumpinduwa nyerere ni kule kuwa rafiki mkubwa wa kambona na wale watu wanne.

  Lakini pia ikumbukwe kuwa Nyerere hakumtendea haki huyu bibi alipompeleka kule katika Gereza la ZANZIBAR na akafanyiwa kila aina ya Machafu anayoweza kufanyiwa mwanamke na mateso makubwa, lilikuwa ni moja ya mambo yaliyomfanya mume wake amsaliti tukumbuke binadamu hujafa hujaumbika ipo siku kizazi cha nchi hii itajuwa ukweli ya mambo yaliyopita kama yalivyojulikana yale yaliyofanywa na uongozi wa MR Aldof Hittler dhidi ya binadamu wengine.
   
 5. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kuuliza si ujinga.

  Huyu mama amefanya mambo mengi kwenye nchi yetu unaweza kusoma kitabu cha hivi karibuni kinaitwa UAMUZI WA BUSARA mtunzi Mohamed Said AU LIFE AND TIMES OF ABDULWAHID SYKES.

  Michango mingi ya wazalendo imefichwa.
   
 6. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Bi Titi Mohamed alitoa mchango mwingine mkubwa wa kuwafanya wabunge waongee kiswahili bungeni,ni wakati bunge letu lilikuwa linatumia lugha ya kingereza alipodai "The light in the bottle" akiwa na maana ya kudai taa za umeme barabara za magomeni.Bunge likachukua busara ya kutumia lugha inayoweza kutumiwa na kila mmoja.(INASEMEKANA)
   
 7. Ether

  Ether Senior Member

  #7
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 137
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Historia ya Bibi Titi unaweza kuipata kwenye vitabu vifuatavyo:

  1. Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (Life and Times of Abdulwahid Sykes
  2. TANU Women: Gender and Culture in the Making of Tanganyikan Nationalism, 1955-1965
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bahati mbaya Bibi Titi alipopewa msamaha mwaka 1972 hakuthubutu tena kumkosoa Nyerere, hakusikika tena mpaka Nyerere alipochoka na madaraka mwaka 1990. Alizimwa na state security ya Nyerere, akanyang'anywa nyumba yake Temeke, maskini mama wa watu.

  Kuna mawili: aidha ni kweli alikuwa guilty wa kutaka kumuua Nyerere kwa hiyo aliposanehewa "akaokoka" au alikuwa mwoga mwoga tu, kiasi cha ku compromise principle alipotoka mazabe. Either way, inasikitisha.
   
 9. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  kanyang'anywa nyumba? and of all places Temeke.Nyerere can not be that bad,would someone enlighten us please
   
 10. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mtafute Ustaadh Mohamed Said Dar es Salaam, maarufu sana kwa kuchokonoa historia zilizofichwa atakwambia..nina imani kaandika na kitabu kuhusiana na hili. Nazikumbuka mada zake wakati nilipokuwa skonga....
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Somo kubwa la NDIVYO TULIVYO!

  Two years later, in April 1972, Mohammed received a presidential pardon. Upon her release, Mohammed led a life of isolation. Her husband had abandoned her during the trial, her political associates disowned her, and most of her friends deserted her.
   
 12. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  This is Tanzanian history abecedary, lazima tuyajue haya! Kanyang'anywa nyumba ndio, tena mbili, moja iko Upanga. Baadae, Nyerere alipochoka madaraka ndio akarudishiwa. Lakini hakuwahi kupata pesheni yake ya Uwaziri, TANU, Umoja wa Wanawake. Nafurahi alimwambia haya Nyerere usoni, kabla hawajafa.

  Bibi Titi alianza kukosana na Nyerere miaka ya '60s, wakati Nyerere alipo submit Azimio la Arusha. Bibi Titi hakulipinga, at least not the substantive themes of it, lakini alipinga jinsi lilivyoletwa letwa, anasema Mzee alikuwa anaitikiwa "ndio Mzee, ndio Mzee," bila deliberation na michango.

  Imagine Nyerere katoka masomoni Scotland kwenye ma Fabian Society anakuja kuyumbishwa na Mama wa Temeke hukusu transparency na democracy? Unashindwa kudebate na mwanaharakati mwenzio, unamfunga?

  "Siku moja mimi na Bibi mwingine na Bi Maua tulipelekwa kama kuonyeshwa, wanawake ni hawa na hawa wanakaa hapa na hivi na hivi. Sheneda akaombwa waandikiwe barua kwa waume zao tukamwambia wote tuna waume zetu, ila Bi Maua tu.Tukaingia mjini na Bibi Tatu kila mahali na kila nyumba.

  ...mimi nilikwenda nyumba ya mtu safari ya kwanza kwenda kuarifu mkutano wa TANU. Nilipoingia nyumba moja wanawake wote wakakusanyika wakaniambia, ehee bibi, unataka wanaume wa chumba gani, wa chumba hiki au hiki au kile. Nikajua ehee leo nitapigwa leo; nimeshangaa. Jamani kosa gani tena nimekosa, mimi nimekuja hapa kueleza habari za mkutano, leo kuambiwa nimefuata mwanamume mmoja wa chumba cha uani tena mpaka hivi ninamkumbuka, anaitwa RASHIDI.

  Akasema Bibi Titi nilichoijia ndilo hilo la kutangaza chama, nikasema ndilo hilo, hapo akawaambia ndio huyu mama anayetangaza chama cha Nyerere kuingia kila nyumba, na nilimuona hata nyumba ya mbele huko, ndiyo nikarudi nyumbani nimenusurika."
   
 13. Ether

  Ether Senior Member

  #13
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 137
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  i was blessed kuishi jirani na bibi titi na nimekuwa na wajukuu zake. hiyo nyumba ya temeke unayosema alinyang'anywa alirudishiwa hata kabla nyerere hajaondoka madarakani na alirudishiwa ya temeke kwanza halafu ya upanga. mpaka sasa hivi wajukuu zake wanaishi pale upanga na temeke.
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani hapo juu nimesamaje, sikusema kwamba baadae alirudishiwa wakati Nyerere alipochoka madaraka? Acha mapepe bro. Unafikiri wote tunaposti posti taarifa fyongo fyongo hapa? Historia ya Bibi Titi nayo ina utata?

  Alirudishiwa, so what, hakunyang'anywa? Walim reimburse renti zake alizokosa wakati wanamiliki nyumba zake?
   
 15. F

  Falconer JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Marehemu Bibi Titi akishirikiana na Kawawa ndio walio mleta Nyerere kwenye chama cha TAA na kuutetea UHURU wa Tanganyika. Waislamu wa tanganyika ndio waliokuwa mstari wa mbele kupigania UHURU wa Tanganyika na bila kujali dini au rangi walimueka Nyere mbele na kukiunda chama cha TANU. Sitaandika mengi ila kuwa nafasi ya huyu Bibi kitaifa imedhalilishwa kiasi kuwa historia imsahau.
   
 16. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii ni kamba, mwongo mkubwa!

  Kwanza, Bibi Titi hakumleta Nyerere TAA, na wala si Kawawa. Pia, Waislam na Wakristo ni wote walishiri kwenye harakati za Uhuru.

  Bibi Titi hakuwepo kwenye picha wakati wa TAA, wala TANU ya mwanzo.
  Bibi Titi ndio aliletwa kukutana na Nyerere, 1955, na dereva Taxi aliyejuana na shemeji wa Bibi Titi. Baadae, shemeji wa Bibi Titi akawa anamsukuma Bibi Tibi ahudhurie mikutano ya Nyerere, na baadae akavutiwa nae, akapewa kadi namba 16. Nyerere alikuwa na kadi namba moja.

  Na Kawawa alikuja TANU akitokea vyama vya wafanyakazi mwaka 1958, four years behind the curve!


  Na madai yako mengine ya Wakristo vs Waislam ni uwongo wa kuchomwa moto. Wakristo na Waislam walishiri bega kwa bega katika harakati. Walionzisha TANU wako 17, wa dini zote:

  (1)Mwalimu J.K. Nyerere – Mwenyekiti
  (2)Geremano Pacha
  (3)Joseph Kimalando
  (4)Japhet Kirilo
  (5)C.O. Milinga
  (6)Abubakari llanga
  (7)L.B. Makaranga
  (Saadani A. Kandoro
  (9)Suleman M. Kitwara
  (10)Kisung’uta Gabara
  (11)Tewa Said Tewa
  (12)Dossa A. Aziz
  (13)Abdu Sykes
  (14)Patrick Kunambi
  (15)Joseph K. Bantu
  (16)Ally Sykes
  (17)John Rupia

  Na ukienda nyumba zaidi, hata viongozi wa Kitaifa wa TAA walioanza kutuma madai ya kimaandishi ikulu ya Sir Edward Twinning kudai chama kitambulike kwa uwakilishi Bungeni walikuwa ni Mwenyekiti na Katibu Mkuu, TAA Taifa, Abdulwahid Sykes na Vedastus Kyaruzi respectively.

  Hiyo ni kabla na wakati wa uundwaji wa TANU. Baada ya kuundwa, TANU ili recruit viongozi wa harakati kutoka viongozi wa vyama vya ushirika, Nsilo Swai, Sir George Kahama, Jeremiah Kasambala, Paul Bomani, John Mhavile, na wengine.

  Kwa hiyo, kusema TANU ilikuwa ya Waislam waliokaribisha Wakristo ( or vice versa ) ni urongo, uzandiki.
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......heshima mbele Mkuu.......hii sio kumkoma Nyani....hii ni kuweka record straight.......
   
 18. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Baada ya kufahamiana na Mwalimu alipewa uongozi katika Women Wing ya TANU ambapo alishiriki katika kuhamasisha wanawake kuunga mkono harakati za TANU za kudai uhuru. Hata hivyo kwa mujibu wa Bibi Titi mwenyewe, (Kwa jinsi alivyowahi kuniambia) ni kwamba tofauti za msingi kati yake na Mwalimu zilianza mwaka 1958 ambapo Mwl. alimpeleka, kwa maelezo ya Bibi Titi, Demu wake masomoni Ulaya kwa kutumia Fedha za Umoja wa Wanawake badala ya mwanamke aliyekuwa amendekezwa na Umoja huo. Mwanamke huyo wakati huo alikuwa ni Nesi katika Hopitali mojawapo iliyokuwa mikoa ya kusini.

  Japokuwa hakueleza, bayana kwa nini alichukizwa na kitendo kile cha Mwalimu, wadadisi wa mambo wanadai kuwa, chuki hiyo ilitokana na wivu wa kimapenzi kwani inadaiwa kuwa hata Mwalimu na Bibi Titi walikuwa................
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mie sio mtaalamu wa historia ya Bara ila kuna kina Jumbe Tambaza, Sheikh Ramiya, Mzee Mtemvu na wengine hawajatajwa?
   
 20. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  it seems there is more to this,then sees the eye.Tunaomba historians mutuweke sawa. Na huyu TAMBAZA,is it true kwamba kuanzia muhimbili primary school mpaka aga khan hospital eneo lote hili lilikuwa coconut plantation yake?
   
Loading...