melisafilbert
Member
- Sep 3, 2013
- 67
- 9
habari za mchana wana jamii hili ni angalizo tu kwa wale wenye watoto kwanza watoto wasizoee kufungulia watu milango muwafundishe maana kuna watoto wengine wakisikia mtu kagonga wanakimbilia geti wanafungua pili jamani watoto wafundishwe kutokuongea na watu wasiowajua zaidi ya salamu kwa ajili ya kuheshimu wakubwa lakini tatu jamani muwe sana makini na hawa watu ambao wanashughuli kama vile kuokota makopo au chupa hizi za maji especially kama humfahamu kuna watu wengi wanaofanya kazi kama hizi lkn wanakuwa na mambo yao mengine kuna watu huwa wanaonekana kama zimefyatuka hivi lkn huwa wanakusudi lao maalum kuna rafiki wa rafiki yangu yeye anasema mtaani kwao kuna bibi anaokotaga makopo na chupa kwenye mtaa wao sasa juzi kati hapa bibi akapita akamuita mtoto wake wa miaka 3 mtoto kwasababu anamuonaga bibi anapita kila siku akaenda kumfwata bibi jalalani mtoto alivyorudi nyumbani amekatwa hapa mbele ya ulimi anasimulia bibi akata hapa anaonyesha sehemu aliyokatwa mtoto kupewa chakula anatapika leo ni siku ya pili mtoto anatapika kila anachopewa na anakohoa mama mtu akaamua kwenda kwa bibi kumuuliza amefika kwake kaambiwa bibi kasafiri toka jana mama mtu saiz amechanganyikiwa tu hajui cha kufanya na mtoto ndo hivyo anakohoa na kutapika kila anachopewa anakitapika