Wana Jf
salaam ziwafikie..
Mpenz wangu tunapendana sana.Tatizo ni dini zetu yy baba ake alikuwa muislam,mm ni mkristu.
Ilifikia wakati,mm na yy tulikubaliana mahusiano yetu yawe rasmi.Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo.Baba ake mzazi hakuwa tayari bintiye kuolewa na mkristu.
Tulijaribu kila njia,ikafikia hatua tukaomba msaada wa wazee wenye hekima, ili tusaidiwe lkn jitihada zetu ziligonga mwamba.
Mpenz wangu aliamua kushika mimba ili kumshinikiza baba ake mzazi akubali.Thank God mambo yalienda km alivyo kusudia.
Niliitwa ili nithibitishe endapo nilihusika.Nilikubali hivyo nikatozwa tsh.500,000 km faini ya uchafuzi wa familia.Kisha nikakabidhiwa binti.
Siku chache zikiwa zimesalia kwa mpenz wangu kujifungua,aliamua kurudi kwao ili akajifungulie chini ya uangaliz wa mamake.Hakukaa hata siku moja baba ake mziza akajiua.
Nilienda nyumba kwao kumjulia hali ikiwa zimebaki siku tatu ajifungue.Dada yake alianza kunishambulia huku akinituhum mimi ndio niliyesababisha baba yake ajiue.
Alijifungua mtoto wa kiume baada ya miez 9 kutimia.Bahati mbaya mtoto alipoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Niliwaza sana sababu ya mtoto kufa.Kwakuwa wote tulipima maambukizi ya virus vya ukimwi na wote tulikuwa salama.
Labda mpenz wangu alipatwa na shock hivyo kuwa na psychological torture iliyopelekea kumuathiri mtoto? kwa kuwa hapakuwa na sababu yoyote waliyotoa ma nurse as to the reason why the child died shortly after birth.
Niliamua kurudi hospital nikiwa na mpenz wng,mamake mzazi pamoja na shangazi yake ili japo tukapewe clinical record card,in case ikitokea kapata ujauzito ni future iwe rahasi ku track record.
Daktri aliyekuwa zamu aligoma kutoa clinical record card kwakuwa aliyekuwepo shift wkt mpenz wangu anajifungua tayar alshaondoka.
Baada ya siku chache nikapata habari kuwa mtoto wangu alivutwa kitovu kusudi afe.Aliyefanya hivyo ni yule dada yake na mpenzi wangu alinishambulia mwilini na kunituhum kuwa mimi ndio chanzo cha baba ke kujiua.k
Naomba niishie hapa ntaendelea...