Bibi Kanikataza!

A.K.A.47

Member
Jan 27, 2013
56
6
Wana Jf
salaam ziwafikie..
Mpenz wangu tunapendana sana.Tatizo ni dini zetu yy baba ake alikuwa muislam,mm ni mkristu.

Ilifikia wakati,mm na yy tulikubaliana mahusiano yetu yawe rasmi.Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo.Baba ake mzazi hakuwa tayari bintiye kuolewa na mkristu.

Tulijaribu kila njia,ikafikia hatua tukaomba msaada wa wazee wenye hekima, ili tusaidiwe lkn jitihada zetu ziligonga mwamba.

Mpenz wangu aliamua kushika mimba ili kumshinikiza baba ake mzazi akubali.Thank God mambo yalienda km alivyo kusudia.

Niliitwa ili nithibitishe endapo nilihusika.Nilikubali hivyo nikatozwa tsh.500,000 km faini ya uchafuzi wa familia.Kisha nikakabidhiwa binti.

Siku chache zikiwa zimesalia kwa mpenz wangu kujifungua,aliamua kurudi kwao ili akajifungulie chini ya uangaliz wa mamake.Hakukaa hata siku moja baba ake mziza akajiua.

Nilienda nyumba kwao kumjulia hali ikiwa zimebaki siku tatu ajifungue.Dada yake alianza kunishambulia huku akinituhum mimi ndio niliyesababisha baba yake ajiue.

Alijifungua mtoto wa kiume baada ya miez 9 kutimia.Bahati mbaya mtoto alipoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Niliwaza sana sababu ya mtoto kufa.Kwakuwa wote tulipima maambukizi ya virus vya ukimwi na wote tulikuwa salama.

Labda mpenz wangu alipatwa na shock hivyo kuwa na psychological torture iliyopelekea kumuathiri mtoto? kwa kuwa hapakuwa na sababu yoyote waliyotoa ma nurse as to the reason why the child died shortly after birth.

Niliamua kurudi hospital nikiwa na mpenz wng,mamake mzazi pamoja na shangazi yake ili japo tukapewe clinical record card,in case ikitokea kapata ujauzito ni future iwe rahasi ku track record.

Daktri aliyekuwa zamu aligoma kutoa clinical record card kwakuwa aliyekuwepo shift wkt mpenz wangu anajifungua tayar alshaondoka.

Baada ya siku chache nikapata habari kuwa mtoto wangu alivutwa kitovu kusudi afe.Aliyefanya hivyo ni yule dada yake na mpenzi wangu alinishambulia mwilini na kunituhum kuwa mimi ndio chanzo cha baba ke kujiua.k

Naomba niishie hapa ntaendelea...
 
aah! we ndo utakua unatukomoa kabisa..mwaka mzima??
Aisee mmezidi nyie watu!



Ila hata mimi nitalipizia tu siku moja..ngoja nipate inspiration nzuri
nije kuwasimulia kisa changu hapa..Kitaanza 01/01/2014 hadi 31/12/2014
mtalia nawaambia!!!!!
 
Aisee mmezidi nyie watu!



Ila hata mimi nitalipizia tu siku moja..ngoja nipate inspiration nzuri nije kuwasimulia kisa changu hapa..Kitaanza 01/01/2014 hadi 31/12/2014 mtalia nawaambia!!!!!

Alafu unaishia kwenye utamu tu unakaa siku mbili unaendelea
 
Aisee mmezidi nyie watu!



Ila hata mimi nitalipizia tu siku moja..ngoja nipate inspiration nzuri nije kuwasimulia kisa changu hapa..Kitaanza 01/01/2014 hadi 31/12/2014 mtalia nawaambia!!!!!

hahaha! Aii wewe! Usitufanyie hvyo wendhio!!
 
Aisee mmezidi nyie watu!



Ila hata mimi nitalipizia tu siku moja..ngoja nipate inspiration nzuri nije kuwasimulia kisa changu hapa..Kitaanza 01/01/2014 hadi 31/12/2014 mtalia nawaambia!!!!!

sipati picha ndio ungekuwa shigongo ,kila siku unaweka paragraph moja unamalizia itaendelea kesho
 
Aisee mmezidi nyie watu!



Ila hata mimi nitalipizia tu siku moja..ngoja nipate inspiration nzuri nije kuwasimulia kisa changu hapa..Kitaanza 01/01/2014 hadi 31/12/2014 mtalia nawaambia!!!!!
He he he nasubiria kwa hamu!!!
 
...nilitaka kuua bibi akanikataza. FULL STOP. mnakera nyie watu.
 
embu tumuite Watu8 aje kututabiria mwisho wake binafsi nshachoka kusubiri.

Hahah...hebu kamata hii juice baridiii ya embe usichoke.

Jamaa mwishoni ataomba ushauri kuwa, bibi yake kamkataza kuendelea na huyo binti lakini yeye moyo wake bado unampenda...je afanyeje?
 
Wai

Mi sipendagi hizi mambo ya itaendelea

Sasa hapa mtu utatoa ushauri gani, acheni kukatisha bhanaa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom