Bibi huyu amemla nyama mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi huyu amemla nyama mtoto

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Apr 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  bimchaw.jpg
  Stori na Makongoro Oging
  MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Mary Mbaga (70), (pichani) mkazi wa Kinondoni shamba jijini Dar es Salaam, amepata kipigo kikali kutoka kwa wananchi usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita wakidai kuwa amemla nyama mtoto aliyekuwa amefariki dunia wiki iliyopita.
  Mtoto huyo aliyefariki dunia aliyejulikana kwa jina la Sharon Kalinga mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili anayedaiwa kuliwa nyama na bibi huyo, alifariki katika mazingira ya kutatanisha na kuzikwa siku hiyo ambayo bi mkubwa huyo alikutwa katika chumba cha wazazi wa marehemu akiwa uchi saa saba usiku.
  Chanzo chetu cha habari kimesema mara baada ya bibi huyo kukutwa ndani akiwa katika hali hiyo, wenyeji walipiga yowe wakisema ‘mchawi, mchawi’ hali iliyofanya watu kujazana nje.
  bimchawi2.jpg

  SHANGAZI WA MAREHEMU ANASEMAJE?

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi shangazi wa marehemu Sharon aliyejitambulisha kwa jina la Stella Kalinga, alisema kwamba alishangaa kumuona usiku huo bibi Mary akiwa uchi wa mnyama.
  “Nilishanga sana kumuona bibi Mary usiku huo kwani mara baada ya kuzika tulishawatangazia majirani kuwa hakutakuwa na matanga, iweje aje tena akiwa katika mazingira hayo ya kuwa mtupu?
  “Mbaya zaidi kwa nini alikuja na kujificha ndani na wakati anaingia mbona hatukumuona?” alihoji mama huyo.
  Aliendelea kusema kwamba watu walipombana bibi huyo kwa maswali alisema hakuwa peke yake bali alikuwa na wanawake wanne lakini watatu alidai walitimua mbio wakati wa sekeseke hilo.
  Hata hivyo, Stella alidai kwamba bibi Mary hakuwa na nia nzuri kwani licha ya kuwa uchi baada ya kubanwa alikiri kwamba watoto wote wawili wa Kalinga (Sharon na Sesi Kalinga aliyefariki mwaka juzi) amewala nyama.
  Stella alidai kwamba siku ambayo Sharon alifariki Alhamisi iliyopita saa 5 asubuhi, bibi Mary alifika nyumbani kwao saa 2.45 usiku na alipoingia alienda moja kwa moja kwa mama wa marehemu na kuanza kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili.
  Aliongeza kusema kwamba aliwaeleza wenzake kwamba bibi Mary hakuwa na nia njema kutokana na vitendo alivyokuwa akivifanya, hivyo alianza kumkemea kwa maombi ambapo baadaye aliondoka.
  Aidha, alisema kwamba siku hiyo alipoonekana kwa mara ya pili akiwa ndani, aliondolewa hadi nje huku akiwa anatetemeka ambapo alidondosha gauni na chupi ya marehemu alizoshika mkononi.
  Alisema kitendo hicho kikatafsiriwa na wananchi kwamba ni mchawi ndipo walizidisha kumpa kipigo na kumgalagaza kwenye tope.
  Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo waliohojiwa na gazeti hili walisema kwamba mara baada ya bibi Mary kukamatwa akiwa uchi, alishurutishwa kutembea mtaani tangu usiku huo wa manane hadi saa 12:00 asubuhi alipookolewa na polisi wa doria huku mwili wake ukiwa umelowa damu.


  bimchawi03.jpg  NYUMBANI ANAKOISHI

  Gazeti hili lilipofika anakoishi bibi huyo eneo la Kinondoni Shamba lilimkuta wifi yake aliyejitambulisha kwa jina la Loveness Mbaga, ambaye alisema kwamba yeye ni mgeni na alifika hapo siku ya Ijumaa iliyopita akitokea Kijiji cha Mbaga, wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro.
  “Nilikuja kuwaletea taarifa bibi Mary na watoto wake kuwa kutakuwa na ubatizo wa watoto wangu mwezi wa sita mwaka huu.
  “Siku ya Ijumaa ilipofika saa 8 usiku majirani waliniamsha wakanieleza kuwa bibi Mary amekamatwa uchawi akiwa uchi wa mnyama.
  “Nilipotoka nje niliwaona watu wengi wamemzingira, hata hivyo, sikusema kitu kwa kuhofia kwamba ningeweza kuunganishwa naye, nilirudi ndani huku machozi yakinitiririka,“ alisema Loveness.


  MWENYE NYUMBA ANASEMA JE?

  Hasajeni Mwambonda ndiye mwenye nyumba anayoishi bibi Mary, alipohojiwa alisema kwamba bibi huyo amekaa kwake zaidi ya miaka mitatu bila matatizo yoyote.
  Hata hivyo, alisema siku hiyo ya tukio hakuweza kumsaidia kwa lolote.
  Habari zaidi zilieleza kuwa bibi huyo baada ya kupigwa mtaani alipelekwa kwenye uwanja wa mpira uliopo karibu na eneo la tukio ndipo polisi wa doria walipojitokeza na kumuokoa kwa kumchukua na kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay baadaye Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa.


  MGANGA MKUU MWANANYAMALA

  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk.Sophians Ngonyani alikiri kumpokea mgonjwa huyo na kulazwa wodi 3 ya wanawake anakoendelea na matibabu ya majeraha aliyopata.


  MTUHUMIWA WA UCHAWI

  Bibi Mary alipohojiwa akiwa wodini alidai kwamba kipigo alichopata toka kwa wananchi ni kwa kutuhumiwa kwamba ni mchawi na kuhusishwa na kifo cha mtoto Sharon na kumla nyama yake madai ambayo aliyakanusha.

  “Ni kweli nilipigwa sana na kutokwa na damu ambayo walinisingizia eti ni ya mtoto niliyemla wakati mimi siyo mchawi, hata hii khanga niliyonayo hapa hospitalini nilisaidiwa na mama mmoja. Mimi nina watoto tisa, najua watakuja kuniona,” alisema kwa tabu bibi huyo.
  Aliendelea kusema kwamba bila polisi kumuokoa wananchi wangemuua.

  Baadhi ya wananchi wa maeneo anayoishi bibi Mary walisema bi mkubwa huyo alikuwa anafanya biashara ya kuuza pombe.
  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema yupo nje ya ofisi lakini akaahidi kufuatilia. Hata hivyo, ofisa mmoja wa polisi alikiri askari wake kumuokoa bi mkubwa huyo na akasema upelelezi unaendelea.

  bimchawi mwisho.jpg

  Bibi huyu amemla nyama mtoto - Global Publishers

  HAYA MATATIZO YATAKWISHA KWELI HAPO KWETU TANZANIA?
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Aisee!
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mmmmm!!
   
 4. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ibilis! Kitu kimoja nashindwa kuelewa endapo watu wafanyao haya huwa wana-akili timamu ama ndo wanakuwa wanatumikishwa na nguvu za giza? Haiingii akilini mtu kutembea uchi wa mnyama!
   
 5. K

  Konya JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  OMG! tunakoelekea sijui wapi!
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu lazima atakuwa mwana CCM :A S 39:
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  :tape2:
   
 8. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duu... Nadhani hana akili timamu huyo bibi. Au Malaria imepanda kichwani!!!!!!!
   
 9. K

  Kamzuzu Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shindwa shetani,shindwa tena shindwa!umezidi
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kama serikali haitaweza kutambua kama uchawi upo,ilihali haohao viongozi wanao iongoza serikali wanashuhudia mambo ya kichawi ktkt mitaa wakaayo,basi mambo hayo hayatakwisha daima

  mbona baadhi ya nchi wana sheria zinazotambua uchawi? mfano Kenya
   
 11. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Imani za kishirikina zinalipeleka taifa pabaya.
   
 12. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Serikali yetu ni vigumu kuutambua uchawi japo VIONGOZI WAKE na WAFANYAKAZI WAKE (wengi tuu) ni washiriki wakubwa wa uchawi......Kwa kutoutambua SUPPORTERS wa uchawi wanatengeneza mazingira ya kuulinda uendelee kuwepo hasa ukitilia maanani kwamba KWAO WANAAMNI UNAWASAIDIA hasa katika KULINDA VYEO VYAO na KUSHINDA nafasi mbalimbali za uongozi:-(
   
 13. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  On top of that ni mwana CCM
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Eeh makubwa!!
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Wewe si umeona anatokea mkoa gani ? jibu unalo usiwasingizie CCM.
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  I tell you WHAT?

  Ni bora kutokuendekeza na kuutambua! Ni kuukataa kata kata na kuto kuu entertain kabisa hiyo dhana!

  Ni Imani! Na namna na kumanage imani ambayo ni negative ni kuikataa na kutoipa nafasi kabisa kwa imani.. How it works ... hata kama upo ... lakini ... ukiukabili kwa imani ya kuukataa technically hiyo ndio the best remedy ... hakuna dawa nyingine ..uwepo usiwepo ..dawa nimoja tu .. Imani ya Kuukataa na kuto ku deal dal nao!! Srtong NO kuwa upo ndio dawa kwa Uchawi!!
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mbaga iko Upareni na CCM iko upareni kwa wingi
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mchawi hawi tu Mwana wa CCM anawea kuwa Mwana Wa Chadema au CAFU usilete chuki zako kwenye mambo ya chama Uchawi hauna Vyama hata wewe au mimi tunaweza kuwa Wachawi mkuu samahani kama nitakudhi jaribu kurekebisha maneno yako .
   
 19. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Dah hii habari kumbe bado ipo tu aisee..Kaazi kweli kweli bado tunayo.
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Huyo josefina!!
  Bisha
   
Loading...