Bibi Harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa, kisa tumbo

Bibi Harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa, kisa tumbo

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,289
Kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo August 2, 2017 Mtangazaji Geah Habib ameifikisha Hekaheka iliyotokea Mtoni Kijichi DSM ambako nyumba ya Harusi iligeuka kilioni baada ya mwanamke kuolewa na kufariki saa 11 baadaye.

Tukio hilo linatajwa kutokuwa la kawaida baada ya ndoa kufungwa saa Kumi Alasiri na Bibi Harusi kufariki saa Kumi na Moja Alfajiri huku ikidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa Miezi Sita.

Inaelezwa kuwa siku ya tukio Bwana Harusi aliwapigia simu ndugu wa mkewe kuwapa taarifa ya kuumwa ghafla mkewe ambapo alikuwa analalamika kuumwa tumbo na kumkimbiza Hospitali usiku huo ambako baadaye alifariki.
 
  • Thanks
Reactions: lup
Kifo ni mipango ya mungu...ukianza kuamini imani zetu za kiswahili ktk haya mambo utapoteza muda wako sana. I knw how it feels to lose a mother n a child sio kitu rahisi kuhimili lkn u av to find a way to deal with it



Mungu amlaze huyo marehemu panapostahili
 
Mtu keshafanya yake,.. Mim ndo maana siwez kuishi uswahilini,
 
unashangaa vipi mtu kufa?
kila mtu anastahili kufa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Dah! Inasikitisha sana. Yaani hata ndoa hajaifaidi.
Hiyo ni mipango ya Mungu, lakini kwa hulka yetu binadamu tutahusisha na imani za kishirikina.
R.I.P bi harusi.
Pole sana bwana harusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahadi yake ilishafika.
Haina tofaut na wale wanaoenda kufunga ndoa mji mwingine,ila wakat wanarud kwenye makaz yao wanapata ajali na kupoteza maisha

May Allah bless Me and You
 
Kifo ni mipango ya mungu...ukianza kuamini imani zetu za kiswahili ktk haya mambo utapoteza muda wako sana. I knw how it feels to lose a mother n a child sio kitu rahisi kuhimili lkn u av to find a way to deal with it



Mungu amlaze huyo marehemu panapostahili
Usikariri vifo vingine ni mipango ya wanadamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apumzike kwa amani.

Ni ngumu kwa watu wa karibu kuamini kifo chake ila kwa upande mwingine katika siri kubwa tusiyoijua ni siku ya kufa na kila mwanadamu ana siku na saa aliyopangiwa kufa hivyo itakuwa siku yake ilishafika
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom