Kwa maoni yangu unaanzia mbali mno ndugu, ni kheri ungeanza na hizi hizi za humu nyumbani (bado still ni hot cake), na za nje ila uwe distributor mkubwa wa jumla, ukisha master hiyo utajiongeza na hzo imports. Tafuta chimbo, miji iliochangamka na inayokua kwa kasi, mfano kahama, chunya, mbeya city, tunduma-songwe. Anza na products za TBL na zngne ambazo ni common nchini. Bia za kopo zote kama safari, klmanjaro, redds, fish, castle lite Konyagi, kvant, valeur, choice, Tzee, black&white, redlebell, brand tofauti za wine za dodoma, 4cousins, autumn harvest, drosthof, bia za cane za nje km windhoek, heineken, savanna, desperados, etc(list ni ndefu). NB. Ukitaka kuwa agent wa TBL (kwa bia za kreti) ni kipengele chenye mchakato mgumu na uvumilivu na itahitaji mtaji si chini ya M100, hawatoi kizembe uwakala pamoja na kuwa na hyo fedha ila ukiupata umeula. Utahitaji pia uwe na nyenzo za kazi kama magari na vyombo vdgo vya usafiri kwa usambazaji.
Kupata jina kubwa kwa biashara ya pombe ni kugusa tu.