Biashara ya soko la mtandao (network marketing)

Biashara ya soko la mtandao (network marketing)

bereng

Senior Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
114
Reaction score
21
Biashara ya Mtandao ni njia ya kisasa ya usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani hadi kumfikia mteja au mtumiaji moja kwa moja. Hivyo, kiwanda kinazalisha bidhaa tu. Halafu kuna mtu mmoja tu ambaye ni msambazaji anayehusika na kufikisha bidhaa kwa mteja. Katika mfumo wa biashara za kawaida, kiwanda huzalisha bidhaa kasha huwauzia labda Depot au mawakala wakuu. Hawa huwauzia tena wasambazaji au wauzaji wa jumla, nao pia huwauzia wauzaji wa rejareja ambao watamfikishia mteja. Kwahiyo, bidhaa inaweza kuzalishwa kiwandani kwa tsh 380 lakini mteja ataipata kwa tsh 600. Kuna tsh 220 inagawanywakwa watu wa katikati. Lakini hapo hapo utagundua kiwanda hakipati faida kubwa sana kwa sababu, katika hiyo hiyo 380 kuna gharama za usambazaji, kuwalipa macelebrities kwa ajili ya matangazo, radio, television, mabango, magazeti na hata mitandao ya kijamii, pamoja na gharama za sales department na mengineyo. Mwisho wa siku, utakuta kiwanda unaweza kukuta katika 380, baada ya kutoa gharama zote labda 180 ndiyo inaweza kubaki kama faida.

Katika biashara ya mtandao, ile 220 ambayo inagawanywa kwa watu wa katikati, anapewa mtu mmoja tu ambaye ni msambazaji atakayenunua bidhaa toka kiwandani kwa tsh 380 na kumfikishia mtumiaji kwa tsh 600. Hivyo, kiwanda hakitalipia tena gharama za matangazo, mabango pamoja na nyingine ila kitamuelimisha huyo msambazaji kuhusu bidhaa ili yeye sasa aweze kumfikishia mtumiaji moja kwa moja. Hivyo kiwanda kinampa msambazaji uhuru wa kuwashirikisha watu wengine ambao watakuwa washirika wake katika biashara ili aweze kukuza biashara yake. Atawafundisha hao washirika wake katika biashara ili nao wawe na uwezo wa kufanya kama yeye. Lakini atanufaika kwa kila mtu anayemshirikisha katika biashara kwa kupata asilimia za mauzo ya hao pamoja na timu zao

Atakuwa amegawa muda wake vizuri na kutengeneza kipato kizuri hata yeye asipofanya kazi, endapo atajenga timu. Lakini tambua kila mmoja ana fursa sawa ya kutengeneza kipato. Kipato kikubwa hutegemea jinsi mtu atakavyokuwa na timu kubwa kwa kuwashirikisha watu wengi katika biashara. Msingi wa hii biashara ni kushirikishana habari kuhusu bidhaa au huduma inayotolewa na kampuni halafu unanufaika na kutengeneza kipato. Lakini una uhuru wa kuanzisha kampuni yako `invisible company` ambapo utafanya biashara na kampuni na kutanua wigo wa biashara yako kwa kuwekeza muda wako kuwafundisha wengine biashara ambao watakuwa washirika wako kwenye biashara kwa kuwa na kipato kisichokuwa na kikomo.

Hayo ni maelezo mafupi tu kuhusu biashara ya mtandao japo ni biashara kubwa sana na inahitaji kujifunza kwa kina na kuielewa kwani ili ufanikiwe katika biashara ya mtandao lazima ujifunze upate kuielewa vizuri, hapo utafanikiwa. Nimekutana na watu wengi walioshindwa hii biashara, karibia wote nimegundua hawakuwa na uelewa mzuri wa biashara. Hapa huhitaji pesa ili utengeneze pesa, ila unahitaji maarifa. Kama huna maarifa ya kutafuta pesa unaweza leo ukashinda tuzo ya shilingi million 100, lakini baada ya miez 3 ukawa kapuku wa kutupwa!.

Kuna watu wengi maarufu duniani wanaoamini katika hii biashara akiwemo Robert Kiyosaki Mwandishi wa vitabu vya Rich dad poor dad pamoja na vingine kama The business of 21[SUP]st[/SUP] century. Ameelezea vizuri sana hii biashara. Lakini yupo Professor Pat Utomi wa Pan African University anasema `Network marketing is the futuristic way of doing business now`. Bwana Bill Clinton pia katika hotuba yake alikuwa akiyashukuru makampuni ya network marketing kwa kuwapa watu fursa sawa na kubadilisha maisha yao. Lakini pia Bill Gates, aliwahi kuulizwa kama angefilisiwa na kuanza upya angefanyeje?. Yeye alisema tu kwamba angechagua biashara ya mtandao. Lakini wapo wengine wengi wanaoiamini na kuwashauri watu wanaotaka mabadilko waifanye.

Kuna makampuni zaidi ya 5,000 yanayofanya biashara ya mtandao duniani. Hivyo unapotaka kufanya jaribu kuangalia kampuni bora. Mimi kampuni ninayofanya nayo, iko katika kumi bora kidunia kwa miaka mingi sana. Kwa Afrika na Tanzania ni namba moja. Nakushauri pia wewe unayependa hii biashara, usikurupuke ilimradi biashara ya mtandao, ila angalia kampuni itayokufaa. Lakini biashara ya mtandao sio `get rich quick scheme`, japo kuna watu wanatengeneza pesa nyingi ndani ya muda mfupi sana na kubadilisha maisha yao. Ni kitu ambacho kwa wakati mwingine kitakuchukua muda kuyapata mafanikio. Inaweza kukuchukua pengine hata mwaka mmoja kuanza kuona matokeo makubwa/kutoboa kama waswahili wanavyosema. Ila mafanikio yakija/ ukitoboa tambua huwa ni ya kudumu.

Unapoamua kufanya biashara hii usimsikilize mtu, ielewe biashara halafu uamue kama inakufaa kwa kulinganisha marketing plan na ndoto zako. Ukiona inakufaa, nakushauri anza maramoja. Ukitaka ushauri kutoka kwa watu utakutana na watu wa aina 3. Aina ya 1 ni wale wasiojua lolote kuhusu hii biashara na watakwambia haifai. Kundi la 2 ni wale waliowahi kuisikia, huenda hata kuifanya halafu wakashindwa. Hao watakupa sababu za kushindwa. Aina ya mwisho ni wale wanaofanya na wamefanikiwa na wanakushauri uifanye na kukuahidi sapoti ya kutosha. Nakuomba usikilize hili kundi la mwisho. Tambua hili ni kundi dogo sana kwani dunia imegawanyika, wengi ni watu wenye mtazamo hasi, waoga na hawana ndoto kubwa, au wana ndoto kubwa ila huacha hofu kuwazuia kufanya maamuzi sahihi.

Mi nakumbuka nilipoambiwa mara ya kwanza kuhusu hii biashara, kuna rafiki yangu wa karibu sana nilimshirikisha. Lakini alinivunja moyo na kunikatisha tamaa. Mimi sikumsikiliza kwa sababu nilijua maisha ni yangu na nimeshaona fursa. Nilianza kuifanya na baada ya muda mi sikumwambia kitu kuhusu pesa ninayotengeneza kwa mwezi ila aliona mabadiliko. Alikuja na kunambia anataka kuanza naye biashara, hadi leo yuko kwenye biashara na anafanya vizuri sana, anafurahia kipato. Hii hunipa picha kwamba, hii biashara inaweza kumtimizia mtu yeyote ndoto zake endapo atakuwa na fikra sahihi na kujifunza biashara. Ila sisi tuko tayari kutoa sapoti kwa yeyote anayetaka kuanza hii biashara ili kuhakikisha anafanikiwa nasi tuweze kufanikiwa pia kwani huu ndio msingi wa biashara hii. Kama una roho mbaya huwezi kufanikiwa hata kidogo na hii biashara haikufai, nakushauri tafuta biashara nyingine. Hii ni biashara ya watu wanaopenda kuwasaidia wengine pia wafanikiwe. Mimi nilipoanza biashara nilianza kuwashirikisha Ndugu, jamaa na marafiki, leo hii nimegusa maisha yao kwa kiasi kikubwa sana na wananishukuru na kuniombea.

Hizi ni baadhi ya sababu, kwanini ufanye biashara ya soko la mtandao: 1. Mtaji kidogo. Hii biashara haihitaji mtaji mkubwa sana. Mtaji unaoweza kuanza nao ni M. 1. 5 kima cha juu. Lakini haihitaji duka, wala haihitaji kutembeza bidhaa mtaani kama machinga wala haihitaji vibali. Kampuni imeandaa mfumo mzuri wa kuuza bidhaa ambao tunautumia. Lakini unapofanya nasi unapata free license ya kufanya biashara ktk nchi zaidi ya 160 duniani.

2. Mafunzo ya biashara bure na usaidizi. Kampuni imeandaa mfumo mzuri wa biashara ambapo utapata mafunzo ya biashara na usaidizi wa karibu hadi uwe na uwezo wa kusimama na kuitanua biashara yako kitaifa au hata kimataifa.

3. Flexibility. Hapa nazungumzia uhuru wa kupanga muda wako katika kuifanya biashara yako. Unaweza kuifanya kwa muda wako wa ziada angalau masaa 10 kwa wiki au unaweza kuamua kuifanya kwa muda wako wote. Watu wengi huanza kwa muda wa ziada, wakiona wamefanikiwa hufanya kwa muda wote.

4. Vipato vikubwa. Ni biashara ambayo itakupa vipato vikubwa ndani ya muda mfupi sana ukilinganisha na biashara zingine nyingi. Jitihada zinahitajika ili kuijenga biashara yako iweze kukua na kukupa faida kubwa. Kitu cha msingi ni kuwa na uelewa mkubwa wa hii biashara. Lakini ukifanya nasi biashara katika kampuni yetu utakutana na njia zaidi ya 10 za kutengeneza vipato katika kampuni. Ndiyo maana watu wanatengeneza vipato vikubwa sana.

5. Uwezo wa kuikuza biashara yako mahali popote pale duniani. Hii ni fursa ambayo unaipata katika hii biashara bure kwa kufanya biashara na watu sehemu nyingine duniani bila ugumu hata pengine wewe usipokuwepo huko. 6. Inarithika. Kitu ambacho nakipenda sana katika hii biashara ni kuweza kuirithisha. Utakapoishia ndipo yule mrithi wako ataanzia na kuendeleza. Hivo unapofanya hii biashara tambua umefanya investment ya maisha yako na vizazi vyako.

7. Ina rasilimali muda `leverage` hii ni siri kubwa sana ya mafanikio katika biashara yeyote kubwa na ndio msingi wa mafanikio. Watu wote waliofanikiwa katika biashara zao kubwa ni wazi kuwa wamewekeza katika rasilimari muda.

8. Ni njia pekee ya kumiliki biashara kubwa duniani. Hii biashara ina sifa zote za biashara kubwa, biashara yeyote kubwa ina mambo makuu 3 yafuatayo; Bidhaa/huduma, mfumo pamoja na Timu au watu wanaofanya kazi. Kwa Tanzania ili biashara iitwe kubwa lazime uwe na watu kuanzia 100 wanaokufanyia kazi. Kidunia idadi inayotakiwa ili iitwe biashara kubwa ni kuanzia watu 500. Lakini hii biashara unaweza kuwa idadi kubwa zaidi ambapo utakuwa na watu ambao hujawaajiri wala huwalipi mshahara ila umewekeza muda wako kuwafundsha biashara ili wafanye kile unachofanya waweze kufanikiwa nawe ufanikiwe maradufu.

9. Ni biashara ya kisasa ambayo inakwenda na wakati. Kila fursa ina wakati wake. Huu ndio wakati muafaka wa hii fursa. Hapa kwetu Tanzania imeanza muda sio mrefu sana lakini imebadilisha maisha ya watu wengi.

10. Imejengwa katika dhana ya DUPLICATION ambayo kwa mujibu wa Mwanasayansi Robert Einstein aliandika katika moja ya vitabu vyake kuwa; mfumo wowote unaobeba dhana hii itakuwa ni maajabu ya 8 ya dunia. Ziko faida nyingi sana na kuna picha kubwa sana ya biashara ambayo unatakiwa kuielewa kama wewe ni mtu makini, una ndoto kubwa na unahitaji mabadiliko ya kweli katika maisha yako.

Jukumu letu ni kukusaidia na kukuongoza ili kuhakikisha unafanikiwa. Kama umevutiwa na unapenda kujua zaidi kuhusu biashara hii. Ni PM, ili nikuoneshe marketing plan yetu, ukipenda tuanze biashara. Ila nahitaji watu ambao wako serious tu, wenye ndoto kubwa na mtazamo sahihi, ambao wako tayari kujifunza kupitia wengine ambao wanafanya hii biashara na wamefanikiwa.

Hii biashara sio ya kila mtu, hivyo ndivyo mimi naamini na ndivyo ilivyo. Hii ni biashara ya watu ambao wanahitaji mabadiliko katika maisha yao. Mabadiliko huanza na kubadili fikra. Tuna msemo kuwa, huwezi kubadili maisha yako ikiwa hauko tayari kubadili fikra zako. Huwezi kufika sehemu tofauti endapo fikra ni zilezile na matendo ni yaleyale. Watu waliofanikiwa wanafikiria tofauti, eti?. Asante kwa kusoma.
 
Toka zako apa...upuuzi huu peleka facebook mana kule ndo kuna standard seven wengi
 
This business is not for you. Halafu unadharau standard seven sana, unahisi wewe elimu yako imekusaidia kuishi ndoto zako au unatimiza ndoto za wengine?. Lakini ujue tu kwamba watu wenye elimu kubwa wengi maskini na daraja la kati. Hao standard seven wengi ndo matajiri na wanawaajili watu kama nyie wasomi. Lakini ujue hii biashara wanafanya hadi wasomi zaidi yako.
mi nahisi hujaijua network marketing
 
This business is not for you. Halafu unadharau standard seven sana, unahisi wewe elimu yako imekusaidia kuishi ndoto zako au unatimiza ndoto za wengine?. Lakini ujue tu kwamba watu wenye elimu kubwa wengi maskini na daraja la kati. Hao standard seven wengi ndo matajiri na wanawaajili watu kama nyie wasomi. Lakini ujue hii biashara wanafanya hadi wasomi zaidi yako.
mi nahisi hujaijua network marketing

IQ yangu ni kubwa kuliko unavyofikiri...sitapeliwi kijinga even a single day
 
This business is not for you. Halafu unadharau standard seven sana, unahisi wewe elimu yako imekusaidia kuishi ndoto zako au unatimiza ndoto za wengine?. Lakini ujue tu kwamba watu wenye elimu kubwa wengi maskini na daraja la kati. Hao standard seven wengi ndo matajiri na wanawaajili watu kama nyie wasomi. Lakini ujue hii biashara wanafanya hadi wasomi zaidi yako.
mi nahisi hujaijua network marketing

Naijua kuliko wewe unavyoijua...ni ujinga kwa kwenda mbele...nani wa kuzurura na alloe vera products...nyambaf
 
hii bness niliwahi kuhudhuria semina yake.kinachonifanya niichukie,ni kiwango cha kuanzia hiyo bness,1.5mil...ss km wanavyodai ni kwa ajili ya kuwakwamua wa2 wa chini kabisa,..hyu m2 wa chini,atatoa wapi hyo capital?
Unless wanaofanya kazi 2 ndo wataweza!
..kitu kingine kinachonifanya nisiingie,ni process ya kutafuta watu wengine ili waje uwaingize huko,manaake bila hivyo unakuwa umepoteza hela yako.
 
Sio Ustaarabu kabisa mtu kaweka post yake ukiona haina mashiko kaa kimya sasa unapotukana na kuwa ona lasaba hawana maana wakati ndio watakao kuosha ukifa sio utu huo. Nadhani usomi ni kuongea lugha zenye kuonesha umesoma na si matusi kama shabiki wa timu ya mtaani. mtoa mada usivunjike moyo unapokuwa Networker kukutana na masahibu haya ni moja ya faida maana unaona ni jinsi gani jamii bado haitambui uzuri wa MLM/NM wao waliingizwa ili waliojuu wapate CC, na ndio maana wanatumia nafasi hii kutoa machungu yao. Nakupongeza pia hujapanick hongera sana
 
Network business ni poa sana, na jamaa ameeleza kwa uzuri but problem is forever their loosing track try this on other business like azam, MO, food products hapo utawin but not umachinga huuu
 
Ndugu zangu sio kila biashara ni ya kufanya.Mimi binafsi ni mjasiriamali lakini biashara ya mtandao siiwezi.hivyo kama wewe huwezi biashara fulani usiwaponde wenzako.ni kama shule sio wote wasiojua hesabu ni mambumbu kuna malawyer wengi hawajui hesabu.hivyo kama unataka kufanya biashara angalia wapi unafiti.na sio kuangalia biashara gani imemtoa mwenzako.wengine mnaweza kufanya biashara ya kuuza utaalam kama bness consultant,tax consultant n.k sio lazima wote tufanye trading business wengine mnaweza kuishia kufanya service business
 
Kauli za mvivu utazijua tu! kwanza matusi,dharau kuponda. ENTREPRENEUR siku zote ni risk TAKER! Usitegemee tambarare katika safari yako utaishia 2km
 
hivi kunamtu anaweza kustahimili kusoma thread ndefu kiasi hiki!? Muwe mna summarize bhana.
 
Endeleeni kupiga kelele na kupondea mkisubiri ukawa wawaletee maisha mazuri watu wenye guts wataendelea kupiga hela
 
mpendwa Christine Hi biashara mtaji wake in mdogo mno ukiamua kuifanya. mtaji wake ni 750,000/= na kwakua waeona sio wote wanao weza lipa hiyo hela kwa mkupuo hivyo wameamua ruhusu watu kulipa nusu na kisha kumalizia nusu mwezi unaofata. tuseme januari unalipa 375,000/= na kumaliza nusu 375,000/= yako februari. Mimi kama mjasiriamali ningemshauri kila mtu ajaribu kuifanya. kuna hela kama ukiwa Una bidii na msimamo na malengo. na hiyo hela yako unapata kuchagua bidhaa yeyote unazo taka za thamani ya hiyo mtaji wako wote. utaamua uuze hizo bidhaa au utumie mwenyewe. kama Mimi kwa mtu ambae atajiunga no vyema atumie ili ajue ubora Wa bidha za forever living ili ndivyo ataweza mshauri mteja wake atumie nini. embu fikiria unalipwa hela kuleta watu wapya kwenye biashara na bado mauzo ya hao watu ulio waleta unapata % yake. sijawahi on a biashara kama hii. siisifii kwakua ninaifanya ila kwa anae ijua atanielewa.
 
Network business ni poa sana, na jamaa ameeleza kwa uzuri but problem is forever their loosing track try this on other business like azam, MO, food products hapo utawin but not umachinga huuu

mavado this is not umachinga. huzunguki na bidhaa na kuuza bidhaa ni kama faida nyongeza tu usikose pocket money mfukoni. ila nikuulize huna ndugu wenye matatizo ya mifupa, pressure, INI, ngozi? hautumii dawa ya mswaki nyumbani? perfume? lotion? sio mpaka ujitangaze. unaangalia mahitaji ya walio Karibu na wewe na kuwashauri na unavyo kijua kitasaidia tatizo ni kitendo cha kushare faida za biashara. hizi bidha no asilia sio chemical oriented. unatumia Huku ukijisikia afya inakua nzuri. ngozi inabadilika na kuwa halininayo takiwa. meno kuwa masafi na kamwe hutosikia jino likiuma kama ukitumia forever tooth gel. embu naomba utumie hata dawa ya mswaki tu. mda Wa mwezi uniambie
 
hii bness niliwahi kuhudhuria semina yake.kinachonifanya niichukie,ni kiwango cha kuanzia hiyo bness,1.5mil...ss km wanavyodai ni kwa ajili ya kuwakwamua wa2 wa chini kabisa,..hyu m2 wa chini,atatoa wapi hyo capital?
Unless wanaofanya kazi 2 ndo wataweza!
..kitu kingine kinachonifanya nisiingie,ni process ya kutafuta watu wengine ili waje uwaingize huko,manaake bila hivyo unakuwa umepoteza hela yako.

mamii Christine kutafuta mtu aingie chini yako ndio biashara yenyewe ni kama ilivyo kwenye office ni lazima ufagie au u process files ndo mshahara ulipwe. huwezii kaa chini kisha utegemee hela mwisho Wa mwezi huo ni wizi. na kwanza kampuni kama hiyo itakufa tu. na ndio maana inaitwa biashara ya mtandao. wewe umeingizwa na wewe uingize ndivyo matokeo utaona. ni kama ushirikiano. anachokifanya chini yako unapata faida. ni kama wewe bosi Wa kampuni umeajiri watu Mia na kila kila mtu afanye ma SAA 8 hizo ni SAA 800 kwa siku huoni ni kazi kubwa inafanyika kwa mkupuo ndivyo ilivyo na hii. kwa jinsi utakavyo kua na watu wengi na kwa bidii zao na zako unapanda cheo na mshiko pia
 
Back
Top Bottom