Biashara ya salon za kiume na kike

Mkwanga

Senior Member
Dec 6, 2010
146
19
Jaman naomba mwenye kufahamu gharama ya kufungua saloon ya kisasa unatakiwa uwe na mtaji kiasi gani naumba mnisaidie....



 
Nataka kuanzisha biashara ya salon za kiume na kike, nifanye nini ili niweze kuhimili kwenye ushindani wa kibiashara hapa tz hasa mikoani kama moro?
 
Habari zenu wadau, nafikiria kujiajiri kwa kufungua saloon ya kike,naomba kwa mwenye uzoefu anisaidie ushauri naweza nikaanzia na mtaji wa shilingi ngapi ?
 
Nakushauri uingie dukani uulizie bei ya madraya, mastima, marolazi then jumlisha. uingie duka la furniture uangalie kama utahitaji sofa kubwa na viti kutegemea na ukubwa wa saloon yako upate gharama zake.

Tafuta location ujue na garama ya rent. baada ya hapo jumlisha vyote. usisahau kuingia madukani kuangalia gharama za madawa ya nywele, vitana, vioo, shampoo na mazaga zaga mengine ya muhimu kwa saluni.

Pia kuna gharama za awali kama za kufix vioo, kuchora jina la saluni, rangi etc. ukifanya yote hayo utajua unahitaji kiasi gani.
 
Habari wanajamvini?

Naomba mchanganuo wa biashara ya salon ya kike.

Asanteni
 
Duh...
Kwanza kabisa location does matter. Ushapata eneo lenyewe ambalo ni convenient?
Tuanzie hapo kwanza
 
Mtaji wako wa kuanzia(initial capital) ni kiasi gani? unahitaji mpango wa biashara (business plan) au? if yes check me
 
Hello wana JF Mimi nahitaji kufungua barber shop itakayotoa huduma zifuatazo: kunyoa ( viti vinne), scrubs , man cure and pedicure..... Nataka niiweke DSM (mwenge, sinza , kijitonyama) ......so kwa yeyote atakayeweza kunisaidia mchanganuo wa pesa zinazohitajika as well as return ntakayopata.....
karibuni
 
Habari za mchana wandugu,

Nilikuwa na wazo la kuwa na barbershop na kuwakodisha vinyozi wawe wananyoa afu mwisho wa wiki wanakuwa wananipa kiasi fulani cha pesa.

Kwa mwenye ujuzi wa hii biashara naomba anisaidie gharama za kuanzisha na return yake au malipo ambayo wanalipaga ni kiasi gani

Shukrani za dhati.
 
Mimi ninayo ya kawaida mtaji kama m3.{kodi inclusive
aisee ni bungua bongo....wananipa 60 kwa wiki!
mwanzoni ni lazima uwe karibu kuangalia mapato!
Pili,vijana wengi sana wanaofanya kazi hiyo upeo wao ni mdogo mno wana tamaa na hawaaminiki ...umakini wa hali ya juu unahitajika kuwachagua na kuwafuatilia
Hata hivyo ukiridhika inafaa kupatia hela ya mboga za majani
 
Mimi nimeshawaza kufanya high ending barber. Yaani hair cut kwa kichwa not less than 8000. Jee mnadhani hii inawezekanika? Nataka kusaka location either mitaa ya Morroco/ Kinondoni au upanga. Ninaposema high ending naamanisha high ending include valet parking.

Jee mnadhani hili linawezekanika? Jee kuna uwezekano wa kupata 20 customers a day?
 

inawezekana ila uweke na warembo wazuri wa kuosha kichwa cha mteja.

kwa sehemu ulizotaja kwa bei hiyo sawa lakin kwa 8000 ukaweka mbagala, manzese, tandale, mburahati, yombo etc jua utakula za uso.
 
kwa maana ya High ending,ni kwamba customers zaidi ya 20 utapata.

Watu Dar wanajipenda,na pesa mji huo ipo kwa wanaojijali.

Halafu sidhani kama Dar kuna Home Services.
Jaribu kuwa mbunifu juu ya hili.
Tafuta boda boda kama nne hivi.Ili Customers wako kama hawana muda basi kuwe na fees fulani hivi za usafiri na Kinyozi kumfuata mteja.
Kuna kipindi watu wapo makazini wamerudi wamechoka,na kuna wengine wana watoto wao wa kiume au mabinti zao wanataka pia kukata nywele kwa wale wanafunzi,wanaona tabu kuwapeleka salon,so unaweza kujikuta ikifika mida ya jioni unapata tenda nyingi.

Mie hiyo niliona nje ya nchi huko Asia,ila wao walizidi ,yaani unajua ukianza ni tabu ila ikichangaya kila mtu atafanya.
Ila hao jamaa wao wapo mbali zaidi na hiyo huduma,wao walikuwa na Mobile Van,yaani hii ni kama Dungu vile,yaani ukiingia ndani salon kamili,utashangaa mtu ameweka gari Parking kumbe anamnyoa mtu,maana watu wapo busy makazi na muda wa kusema atoke hapo afuate salon ilipo anona tabu na jioni mtu yupo mbioni kwenye mambo mengine.
Watu hawaoni tabu kulipa extras kama kazi ni nzuri.
We si unaona hata watengeneza kucha na wapaka rangi wanatembea mitaani na wanakula kazi kama nini,wapiga dawa viatu(Shoes Shiners) na the same.
 
Mkuu huo mtaji unahusisha vitu gani?

Je vifaa vya kunyolea, na madawa unanunua wewe au wao?
 
kodi na umeme juu ya nani?\

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…