Biashara Ya MTUMBA Grade 1

Biashara Ya MTUMBA Grade 1

Joined
Jun 29, 2024
Posts
21
Reaction score
25
Habari wakuu,

Natumai wote ni wazima. Nimepanga kuanzisha biashara ya kuuza nguo (hasa T-shirts za kiume na kike - Grade 1 A). Lengo langu ni kuanzisha duka lenye muonekano wa kisasa na bidhaa bora kwa vijana wa mjini.
Nahitaji ushauri na mawazo mapya kuhusu mambo yafuatayo:

1. Njia bora ya kuendesha biashara hii ya nguo – hasa kwa wale walio na uzoefu, changamoto gani mmekutana nazo na mnaishindaje?

2. Wapi kuna machimbo mazuri ya kuzinunua hizi nguo za Grade 1 (A)? Sitaki kununua mzigo mzima wa belo, nataka kuchagua nguo moja moja (cherry-pick) ili kuhakikisha ubora.

3. Faida na hasara za kuchagua nguo moja moja kutoka kwenye belo – je, ni bora zaidi kulinganisha na kununua belo nzima?

4. Kama kuna mtu anajua wauzaji wa nguo za grade 1 kwa bei nzuri (Tanzania au hata nje), naomba contact au ushauri.

Niko tayari kujifunza na kushirikiana na yeyote mwenye nia ya biashara.

Ahsanteni sana wakuu. 0787117819
 
TAFUTA mshakji mwenye connection watu wanguo nguo even mawinga they are going to help you kama una investment yakutosha
 
Back
Top Bottom