Biashara ya mchele toka Kyela, Kasumulu

Franky

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
2,023
2,231
Habari za mchana wakuu?
Moja kwa moja kwenye mada, hizi ni taarifa fupi nilizopata mpaka sasa kuhusu biashara ya mchele toka Kyela eneo la Kasumulu ndipo utaponunuliwa.

Mosi, plastick la debe moja ambalo linatoa kg 20 wanauza Tsh. 52,000/-

Pili, usafirishaji wa package ya kilo 100 toka Kasumulu mpaka Dar es salaam kwa lori ni Tsh. 15,000/-

Tatu, Ushuru ni Tsh. 1,500/- kwa kilo 100.

Nne, weka kupakia package ya kg 100 kwa Kasumulu iwe Tsh. 500 na kushusha Dar iwe Tsh. 1,000/-

Tano, gharama ya hapo mzigo utaposhushiwa mpaka kufika site utapouziwa iwe Tsh. 3,000/-

Jumla ya gharama zote ni Tsh. 281,000/- kwa mchele wa kilo 100. Sasa kwa bei niliyoambiwa jijini Dar kg 1 ni Tsh. 3,500/- kwa mchele super. Kwaiyo ukiuza kg 100 utapata Tsh. 350,000/- ukitoa utapata faida ya Tsh. 69,000/-.

Sasa nimekuja hapa wakuu niwaulize je kuna information gani sijaipata hapo na ni muhimu kuipata kabla sijajitosa?

Asanteni.
 
Mchanganuo mzuri mkuu
Nenda kathubutu na Mungu atakufungulia heri na Baraka.
 
Mjini mchele umeshuka bei, kwa sasa ni 3300 huo ni mzuri sana

Mchele hauuzwi Kasumulu bali Kalumbulu ambako ndo kuna mashine, pia njia panda ya Ipinda ukisogea mbele kama waenda Border kuna mashine 2 ila wao wamechangamka sana

Kama sio mzoefu unapigwa mchele wa mafuta.

Mchele kwa ajili ya biashara kanunue Mbalali au Ifakara au Kahama.

Hakikisha unanunua kwenye mashine zinazograde
 
Soko la mchele sio Kasumulu ni Kalumbulu, mkuu mambo sio mepesi hivyo, hata mchele wa hovyo upo pia pale, na kwenye vipimo ni wajanja wajanja pia.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Wewe kweli mwenyeji kule, nimempa tahadhari pia.

Vip mashine za kugrade zimeongezeka? Nakumbuka kuna moja ilikuwa maeneo ya Nkuyu kama sio Kikusya.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Mjini mchele umeshuka bei, kwa sasa ni 3300 huo ni mzuri sana

Mchele hauuzwi Kasumulu bali Kalumbulu ambako ndo kuna mashine, pia njia panda ya Ipinda ukisogea mbele kama waenda Border kuna mashine 2 ila wao wamechangamka sana

Kama sio mzoefu unapigwa mchele wa mafuta.

Mchele kwa ajili ya biashara kanunue Mbalali au Ifakara au Kahama.

Hakikisha unanunua kwenye mashine zinazograde
Mchele wa huko kalumbulu haufai kwa biashara mkuu?
 
Soko la mchele sio Kasumulu ni Kalumbulu, mkuu mambo sio mepesi hivyo, hata mchele wa hovyo upo pia pale, na kwenye vipimo ni wajanja wajanja pia.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Asante kwa tahadhari, hata nikiwepo nasimamia upimaji na uchaguzi wa mchele bado nitapigwa tu?
 
Habari za mchana wakuu?
Moja kwa moja kwenye mada, hizi ni taarifa fupi nilizopata mpaka sasa kuhusu biashara ya mchele toka Kyela eneo la Kasumulu ndipo utaponunuliwa.

Mosi, plastick la debe moja ambalo linatoa kg 20 wanauza Tsh. 52,000/-

Pili, usafirishaji wa package ya kilo 100 toka Kasumulu mpaka Dar es salaam kwa lori ni Tsh. 15,000/-

Tatu, Ushuru ni Tsh. 1,500/- kwa kilo 100.

Nne, weka kupakia package ya kg 100 kwa Kasumulu iwe Tsh. 500 na kushusha Dar iwe Tsh. 1,000/-

Tano, gharama ya hapo mzigo utaposhushiwa mpaka kufika site utapouziwa iwe Tsh. 3,000/-

Jumla ya gharama zote ni Tsh. 281,000/- kwa mchele wa kilo 100. Sasa kwa bei niliyoambiwa jijini Dar kg 1 ni Tsh. 3,500/- kwa mchele super. Kwaiyo ukiuza kg 100 utapata Tsh. 350,000/- ukitoa utapata faida ya Tsh. 69,000/-.

Sasa nimekuja hapa wakuu niwaulize je kuna information gani sijaipata hapo na ni muhimu kuipata kabla sijajitosa?

Asanteni.
Kwa hiyo huko kasumulu unaenda kwa ungo? Chakula unakula kwa anayekuuzia mchele? Utalala na kuoga sokoni?
 
Mkuu umeuliza kwa ukali kweli kweli. Nipo kasumulu, mm ndio nitakuwa nazunguka kutafuta huo mchele kama ni kalumbulu kama wakuu walivyosema hapo juu au lah.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom