Kuna rafiki yangu anatafuta soko la mafuta ya alizeti pamoja na soko la mashudu/makapi - hapa anataka kuingia mkataba na viwanda vinavyohitaji mashudu kwa ajili ya kutengeneza vyakula vya mifugo.
Yeyote mwenye mawasiliano ya manager/mfanyakazi wa kiwanda ambacho anafikiri kinahitaji mashudu kwa ajili ya kutengeneza vyakula vya mifugo naomba anipe.
Sio mimi, ila nilivyomwelewa ni kwamba anataka soko la kudumu sio kukuuzia mara moja. Hapa sio swala la kwamba ana tani au dumu ngapi tu, ni lazima pia muelewane bei, ingawa inabadilika kulingana na msimu.
Kuna jamaa anaitwa samson kishimba,huwa anatafuta sana mashudu ya alizeti.hata kama una tani 500.anaweza kubeba zote.
Samson 'kishimba'ngwalida wa NYANZA COTTON GINNERY.rockcity.