Heri ya Mwaka Mpya wajasiriamali..!
Kwa yeyote mwenye uzoefu kuhusiana na Biashara ya kuuza mkaa tafadhali naomba anisaidie yafuatayo;
~Namna ya kupata vibali
Hapa naomba kuelekezwa ni wapi naweza pata vibali ambavyo naweza pata vibali vya kuendeaha biashara hii.
~Sehemu ambako unapatikana mkaa kwa wingi
Kwa sasa nipo Dar es salaam huku maeneo ya Mji Mwema-Kigamboni, pamoja na kuongezeka kwa natumizi ya gesi hapa Dar lakini kaya nyingi za uswahilini zinatumia nishati ya mkaa. Hivyo ni mkoa upi tofauti na pwani ambapo mkaa unapatikana kwa wingi na ni bei rahisi, Pia naweza kusafirisha mpaka Dar.
~Namna ya kusafirisha
Ukiachilia mbali vibali vya kuuzia mkaa katika eneo husika, Je hivi vibali vya kusafirishia bidhaa kutoka mkoa mmoja mpaka mwingine ina gharimu sh ngap kwa lori la tani 4..? Na sehemu gani naweza pata vibali..?
~Mwisho kwa mtaji wa milioni moja mpaka mbili naweza kuanza Biashara mpaka ikasimama na kuanza kuuza mkaa..?
Karibuni sana kwenye mjadala kwa michango mbalimbali