C.K
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 394
- 163
Salaam!
Naomba anayejua kibali cha kuuza mkaa kinapatikanaje - wapi na kwa bei gani kwa muda gani (miezi 6 na mwaka). Pls help me with relevant info.
Asante!
==============================================
MAJIBU NA MCHANGANUO WA BIASHARA
===============================================
Naomba anayejua kibali cha kuuza mkaa kinapatikanaje - wapi na kwa bei gani kwa muda gani (miezi 6 na mwaka). Pls help me with relevant info.
Asante!
Habarini?
Ninaomba kuifaham hii biashara nina mpango wa kufungua stoo ya mkaa nimuweke mtu aniuzie kwa jumla na rejareja.
Naomba kufahamishwa kwa mwenye ujuzi na hili itanigharimu shilingi ngapi hadi kufanikisha hili?
Na je zipi changamoto kubwa nitakazo kabiliana nazo?
Nawasilisha.
Asanteni.
==============================================
MAJIBU NA MCHANGANUO WA BIASHARA
===============================================
Uko mkoa gani? Kila mkoa na kanuni zake. Mfano dar usajili unapatikana halmashauri unayotaka kufanyia biashara yako.
Pwani usajili unapatikana halmashauri pia lakini lazima uwe na mukhtasari wa kijiji unachovuna mkaa, moro sasa hivi wamezuia vibali na usajili.
Vibali vya pwani ni 4200 ya maliasili kwa gunia na 1000 ya halmashauri kwa gunia, hivyo basi kila gunia litakugharimu 5200, hiyo ni baada ya kuwa na usajili ambao ni 205,000 kwa mwaka.
Kwa Dar ni hiyo hiyo 205,000 kwa mwaka, lakini sijui kama kuna vibali vya mkaa hapa kwakuwa sidhani kama kuna sehem wanaruhusu kuchoma mkaa.
Morogoro ni 6000 kwa gunia, ambayo 4000 maliasili na 2000 halmashauri.
Unazo taarifa za usafiri? (Kila gunia litakugharimu 6000) kama unavyo vibali mwenyewe. Ila hiyo isikusumbue, tafuta fuso au canter yenye vibali we unalipa unaweka kishoka mkapa unafika, dereva atahusika kila sehemu ya maliasili na ukaguzi. Ila hakikisha tu ni vya kweli. Usije kulaza mzigo barabarani kwa kupitisha mzigo na vibali feki.
Mkuu salaam!
Niliwahi kufanya hii biashara ikafika wakati nikaacha na kujaribu ya Mbao.
Utaratibu uko hivi:
1. Hakikisha unajua ni wapi utauzia mkaa wako.
2. Utatakiwa kufanya usajili (registration) tsh 261000 ktk ofisi ya wilaya unayouzia. Usajili huu utakuwezesha kukusanya mkaa halali popote pale tz na kupeleka site kwako.
3. Hakikisha mkaa wako ni halali mf. Umekata leseni ya kuchoma mkaa au unanunua kwa watu binafsi ambao watatakiwa kuwa wamelipia ushuru (tsh14,400/90kg).
4. Ukiwa navyo hivyo vitu utatakiwa kupewa kibali cha kusafirishia (TP) na ofisi ya wilaya ulipo mkaa wako (tsh 6500) kwa kila gari kwa trip moja.
Kuna vitu viwili vya kuelewa
1. Kuna kibali na usajili
Ili uweze kuifanya biashara hii ya uvunaj mazao ya misitu lazma uwe na usajili toka maliasili via TFS ........baada ya kupata usajili ukitaka kwenda kuchukua mkaa wako kuuleta mjini utakat T.P (transit pass ) umeita kibali ..
2. Wachomaji mkaa kule vijijin ambao huchoma na kuutayarsha kuwauzia watu wenye usajili kwa ajili ya kupeleka mjin wao huwa wanakata na kuchoma bila kibal huko kijijin (nani anawaona TFS wako mjin tu )ila inatakiwa wew ukiwa na usajili uwapatie lesen ambayo utapewa ukienda TFs kulipia kwaajili ya kutoa mzigo ......
Kwa ujumla haya ni maelezo ya kina ila kule kijijin wanaokata hawana kibali na shughuli hufanyika msituni