Biashara ya kuuza kuku kijiweni

xYz07

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,065
5,890
Wakuu nisi wachoshe saana, nataka kuanza kufanya biashara ya kuuza kuku, niwe na kijiwe changu, niwe naenda vijijini hasa kwenye minada nakusanya kuku then nawaleta mjini kuwauza rejareja kijiweni.

Naombeni ushauri kwa alie wahi kufanya hii biashara na kama nitapata picha ya banda zuri na bora kabisa la kuwaweka hao kuku nitashukuru wazee.
 
Ni biashara nzuri. Ila kwann hujafikiria kuwapeleka sokoni moja kwa moja. Mtaani si wataondoka taratibu sana na inabidi wale.
 
Mkuu ni biashara nzuri ila kama ndugu hapo juu kashauri uwapeleke sokoni moja kwa moja itakuwa njia iliyo bora.
Kama unataka kuweka mtaani uangalie sehemu yenye makazi ya watu au njia waipitayo watu mara kwa mara itakusaidia kuwapata wateja wengi na tofauti kwa ujumla wake. Ujitahidi uwe na chanzo kizuri cha kuwakusanya hao kuku ili kuweka imani kwa wateja wako, barikiwa sana ktk wazo lako hilo.
 
Wakuu nashukuruni kwa ushauri wenu but hapo mnapo sema niwapeleke sokoni moja kwa moja mna maanisha sokoni kiaje?

@ths
jiwe angavu

MUBENDE
Waweza uza kwa jumla au kwa reja reja yote ni sehemu ya biashara ndio maana tunasema wapeleke moja kwa moja sokoni, mf mtu anachukuwa viazi mviringo mbeya akifikisha sokoni moja kwa moja basi anauza kwa jumla kwa wale madalali yeye haangaiki na kutafuta wateja. Hapo unaonaje?
 
Waweza uza kwa jumla au kwa reja reja yote ni sehemu ya biashara ndio maana tunasema wapeleke moja kwa moja sokoni, mf mtu anachukuwa viazi mviringo mbeya akifikisha sokoni moja kwa moja basi anauza kwa jumla kwa wale madalali yeye haangaiki na kutafuta wateja. Hapo unaonaje?
Okk, nimekupata mkuu. AHSANTE
 
Okk, nimekupata mkuu. AHSANTE
Karibu sana na kwauzoefu wangu ktk ufugaji Faida ya biashara ya mifugo huja taratibu siojambo la haraka na uangalie pia swala la magonjwa ya ndege maana kila uwachukuwapo wnakutana wakiwa tofauti na kuku ni jamii ya ndege inayoambukizwa magonjwa haraka sana, nakiombea kila la kheri Mungu akujaalie ufanikiwe ktk hilo.
 
Anza taratibu taratibu biashara ya aina hii inahitaji muda mrefu wa miaka hata kadhaa ili kufanikiwa kupata riziki ya uhakika
 
Back
Top Bottom