Biashara ya kuuza genge

Mchango mzuri sana, kwa uzoefu wako ni maeneo yapi ambayo unadhani kwa biashara hiyo ndani ya Dsm kuna mzunguko mzr wa pesa
 
Wakuu za muda huu
naombeni ushauri wa jinsiya kuanzisha genge la kisasa
ambalo nitaweka ndani ya fremu
nataka kuuza mbogaamboga zote
dagaa wa aina zote
matunda
mafuta ya kupikia
nafaka zote
na vinginevyo
mwenye mchanganua wa biashara hii na bei naomba msaada
 
Hakuna kitu inaumiza jf kuona nyuzi kama hizi na forum kama hii vijana wanapita kushoto, unakuta replies tatu over ila kwenye forum za siasa,udaku vijana wanajitutumua mno huko pahala,hakika kwa mwendo huu vijana tutazidi kuwa vibaraka wa wanasiasa ba celebrities
 
Safi sana mkuu hili ni wazi zuri sana, ushauri wangu kwanza angalia location ina walaji? Kisha fanya utafiti kwa competitors wako alaf zingatia sana ubora na usafi katika biashara yako.
 
Mkuu biashara ya Genge inalipa sana..

Zingatia eneo lisiwe "Ushuani" sana, weka eneo la wakazi wenye kipato cha kati. Nakuhakikishia baada ya miezi minne utakuja na Uzi Wa ushuhuda mwingine. Kuna MTU namfahamu ana genge kama hilo amejenga Nyumba yake ya kuishi hapa hapa Dar. Bidhaa kama nyanya,karoti,vitunguu,pilipili n.k huwa namuona anaenda kulangua ilala na siku nyingine temeke stereo.


Zamani alikuwa anaenda kulangua alfajiri sana ila siku hizi huwa namuona anaenda asubuhi SAA tatu au NNE , sababu yake anasema wafanyabiashara huwa wanawapindishia bei ya kununua kwa jumla wale wanaoenda asubuhi kwa sababu wanajua wanawauzia wafanyabiadmshara wanaoenda kuuza tena mitaani. Na pia alfajiri mrundikano ni Mkubwa sana. Ila anasema ukienda asubuhi bei mnapanga vizuri na yeye siku zote kwa muda huo huwa ananunua bidhaa kwa bei nafuuu saaaaaaana


Maelezo mengine wadau watatoa
 
hebu namba ulielezee hilo genge la kisasa mwonekano ake ukoje nje na ndani ili nikushauri
 
Asante
 
hebu namba ulielezee hilo genge la kisasa mwonekano ake ukoje nje na ndani ili nikushauri
GENGE LA KISASA NAMAANISHA
NAKIDI FREMU NZURI AMBAYO IPO SEHEMU NZURI NA BARABARANI
NAWEKA MBOGAMBOGA
HOHO
KAROTI
VITUNGUU NK
NAWEKA MATUNDA MBALIMBALI
DAWEKA DAGAA AINA MBALIMBALI
BILA KUSAHAU KUWEKA UNGA
MCHELE
NA HATA SAMAKI WABICHI SATO NA SANGARA
 
Naomba kujua bei ya vitunguu pale Iringa kwa gunia, lita 10 na kisado cha lita 4.
Pia bei hizo hizo kwa Dar es Salaam.
Nafikiria kufanya hii biashara.
 

Dooh! Mkuu ,hivi ule usemi wa kidhungu "many are invited but few are chosen" hujawahi kuusikia
 

Mkuu ulifanikiwa kufungua?
 
Genge la kisasa mtaji anzia 2m ikiwemo kodi na kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…