Biashara ya Juice & Bites

Nasiche

JF-Expert Member
Jun 18, 2019
291
732
Wajasiriamali wafanya biashara na wachumi nishaurini kuhusu hii biashara

Nina idea ya kufanya biashara ya juice,bites,maziwa fresh,mtindi ,maji ,soda na matunda

Kodi ya frem nimeambiwa Ni 50k kwa mwezi nilipie miezi 6 ambayo Ni 300k

Friji ninalo
Brenda ninalo
Madeli ya kuwekea bites ninayo
Glass za juice ninazo
Mtaji wa kumnunulia matunda na maziwa soda na maji Nina 100k
Natafuta kijana ambaye nitamlipa 50k au 60k Mimi nitakuwa najoin kuanzia saa Tisa

Kwa harakaharaka hii biashara itanilipaa ,eneo ni nzuri movement ya watu Ni kubwa Mana ni Maeneo ya chuo.

Kama una ushauri wowote Nini niboreshe Nini nipunguze karibu
 
Kwa habari ya kijana utajifunza somo zuri la management of people,It is very crucial issue which you will be expossed to. Biashara itakulipa kulingana na huduma zako pamoja na mteja atathaminiwa vipi. Uboreshe nini na upunguze nini hayo yanakuja kadiri unavyooendelea na huduma,maana kama utawajali wateja utapewa mapendekezo yao ukiwazingua wanapotea kimya kimya.
Kila la kheri katika kutekeleza mpango wako
 
wawekee mchezo huu, atakayekunywa juice glass moja kila siku jumatatu hadi jumamosi, kwa mfululizo,basi anapata offer ya glass moja ya juice.NB hakikisha kuwa aupati hasara.lengo hapa ni kuwezakutengeneza volume ya mauzo kwa mtu mmoja kwa wiki.
 
Wewe ndio unajua mkuu.., mtu hawezi kukwambia kama inalipa au hailipi mfano maziwa tu hatujui unanunua kiasi gani unauza kiasi gani..,

mfano soda faida yake ni kama tshs 98 kwa kila chupa, kwahio kama una kauzembe ka kupoteza chupa ambayo ni kama 250/ kwa kila chupa mpya utaona matokeo..na fridge yako ni energy efficient au kwa siku inakula unit kama imechanganyikiwa ?

Juice inalipa sana kuliko soda ila unauza bei gani 500/= au 1,000/= na shelf life ya juice zako ipoje zinalala au zikilala zimekula kwako ?

Vitafunwa hali kadhalika shelf life ipoje na zinakwisha au zinalala, kwahio mkuu dunia hii hakuna biashara mbaya ubaya au uzuri ni ufanyaji kazi wako wewe, mimi naweza nikasema inalipa na kweli ikalipa wewe ukafanya ikawa ngumu kwako..., pia usisahau kujilipa mshahara kama utakuwa unakaa hapo kuanzia jioni mpaka usiku na ujilipe accordingly sababu kama utapata faida laki 3 kwa mwezi na unakaa siku zote 30 hio ni elfu 10 kwa siku if its worth the hassle kwako basi itakuwa inakulipa
 
Kasema ana hajiri mtu ,Soma vizuri juu
 
Kasema ana hajiri mtu ,Soma vizuri juu
Natafuta kijana ambaye nitamlipa 50k au 60k Mimi nitakuwa najoin kuanzia saa Tisa

Pia hakuna wafanyakazi ambao hawajitambui kama watanzania hapo ajira ni kucheki tu ukiwa haupo ila preparations zote na kila kitu ni wewe, kuanzia kumchunga asikuibie, quality ya products na kumchunga kama mtoto mdogo...., hapo lazima ukabe mpaka penalty
 
Wewe ndio unajua mkuu.., mtu hawezi kukwambia kama inalipa au hailipi mfano maziwa tu hatujui unanunua kiasi gani unauza kiasi gani..,

mfano soda faida yake ni kama tshs 98 kwa kila chupa, kwahio kama una kauzembe ka kupoteza chupa ambayo ni kama 250/ kwa kila chupa mpya utaona matokeo..na fridge yako ni energy efficient au kwa siku inakula unit kama imechanganyikiwa ?

Juice inalipa sana kuliko soda ila unauza bei gani 500/= au 1,000/= na shelf life ya juice zako ipoje zinalala au zikilala zimekula kwako ?

Vitafunwa hali kadhalika shelf life ipoje na zinakwisha au zinalala, kwahio mkuu dunia hii hakuna biashara mbaya ubaya au uzuri ni ufanyaji kazi wako wewe, mimi naweza nikasema inalipa na kweli ikalipa wewe ukafanya ikawa ngumu kwako..., pia usisahau kujilipa mshahara kama utakuwa unakaa hapo kuanzia jioni mpaka usiku na ujilipe accordingly sababu kama utapata faida laki 3 kwa mwezi na unakaa siku zote 30 hio ni elfu 10 kwa siku if its worth the hassle kwako basi itakuwa inakulipa
Juice nitauza Mia tano per glass kwa sababu wanafunzi wanapenda vitu cheap,Ila pia nitaweka glass kubwa za elfu moja ili kumpa mteja option

Maziwa kikombe kimoja mtindi au fresh nitauza elfu moja
 
wawekee mchezo huu, atakayekunywa juice glass moja kila siku jumatatu hadi jumamosi, kwa mfululizo,basi anapata offer ya glass moja ya juice.NB hakikisha kuwa aupati hasara.lengo hapa ni kuwezakutengeneza volume ya mauzo kwa mtu mmoja kwa wiki.
Asante kwa idea nzuri
 
mwanzo tu unawaza asimamie mtu wewe zuzu,anza kwa kusimamia wewe mwenyewe kuvuta wateja na kuwajua na kuwa handling,mfanyakazi siyo mambo yote atakuambia wateja wanataka nini,Ijue biashara kwanza muda wateja wanakuwa wengi ,muda wateja wanapungua ,wateja wa aina gani kama wa smartphone weka WI-FI internet bure kwisha habari yao watajaa hapo hata kama hawana fweza
 
Juice nitauza Mia tano per glass kwa sababu wanafunzi wanapenda vitu cheap,Ila pia nitaweka glass kubwa za elfu moja ili kumpa mteja option

Maziwa kikombe kimoja mtindi au fresh nitauza elfu moja
Maziwa na mtindi hapo great margin ya kutosha hususan ukipata sehemu kwa wakulima ununue maziwa kwa bei ya jumla lita moja upate kwa 1000/=, (isizidi 1700/=) hapo juice 500/= utapata pia ingawa margins sio kubwa sana epuka kutumia disposable cups kama unaweza (zinakula faida) na glass tafuta mifupa (sio vya kioo) as zitavunjika na hii itakucost pia ku-replace glass kila siku..., pia juice inategemea unaweka nini na unapata hayo matunda wapi na kwa bei gani...
 
mwanzo tu unawaza asimamie mtu wewe zuzu,anza kwa kusimamia wewe mwenyewe kuvuta wateja na kuwajua na kuwa handling,mfanyakazi siyo mambo yote atakuambia wateja wanataka nini,Ijue biashara kwanza muda wateja wanakuwa wengi ,muda wateja wanapungua ,wateja wa aina gani kama wa smartphone weka WI-FI internet bure kwisha habari yao watajaa hapo hata kama hawana fweza
Dah hiyo idea ya free WIFI kwa wanafunzi bonge LA idea
 
Back
Top Bottom