Biashara ya Hamahama:Tayari hii ni kashifa nyingine kwa CCM kama zile za EPA, Richmond, Escrow, Meremeta na nyingine nyingi za siku za nyuma

Una bint au alafu unakuja kulalama kwamba kuna jirani anammega?

Mimi nafikiri wewe ndio wa kujiuliza kwamba huenda hujawajibika ipasavyo!
 
Misuse of resources, tena za walala hoi, wakina mama wanakufa kwa kukosa nk. Halafu jiwe anazitumia kununua binadamu wenzake, wewe unaona sawa tu, tuwe na huruma na fedha za wananchi, hivi hizo za kurudia kila mara tena bado chaguzi fake.
Hivi hao watu wanaojiuza wapo chadema tu?

Nyie chadema mna nini mpaka wanaume wazima mnajiuza?

Badilikeni
 
haa haa kwa sasa tumeshapata majibu ya matumizi ya 1.5 trilioni. nimeamini ccm ni mama wa rushwa. nilikuwa na imani sana kwamba chini ya magu rushwa itabaki historia. lakini ndo kwanza inapamba moto.
 
Mwambie Mbowe agawe ruzuku mpaka mikoani kwenye matawi... Sio kugawana na Lowasa kila siku kwa kisingizio cha kujilipa madeni hewa
NARUDIA KUULIZA HILI SWALI TENA, HIVI MBOWE ANA NGUVU GANI HADI SERIKALI ISHINDWE KUMCHUULIA HATUA KWA KASHFA ZOTE MNAZOZIELEKEZA KWAKE IKIWEPO HII YA KULA RUZUKU AMBAYO NI PESA YA SERIKALI? UKINIJIBU SWALI HILI KWA UFASAHA NAHAMIA CCM MIMI NA KIZAZI CHANGU CHOTE LEO HII
 
Mwambie Mbowe agawe ruzuku mpaka mikoani kwenye matawi... Sio kugawana na Lowasa kila siku kwa kisingizio cha kujilipa madeni hewa

Kacheze kamari kwa Ontario wewe una Dili yoyote town zaidi ya kubwabwaja tu



Swissme
 
Ufisadi awamu ya 5 ni mkubwa kuliko jumla ya ufisadi wa awamu zote zilizotangulia kwa pamoja.
Ccm na ufisadi ni sawa na mwili na moyo, haviwezi kutengana, maana vikiachana tu chama kinahamia makumbusho
 
CCM ina kashfa nzito sana. Hii awamu imeamua kuziba watu mdomo ili zisijulikane. Hakuna kitakachofichwa milele
 
Nimelubaliana na wewe
Mara kwa mara nimekuwa nikisema humu kuwa Mungu kawanyima maarifa CCM ili waanguke na kwa hakika wataaguka tu.Ni swala la muda.

Hamahama hii ni ushahidi mwingine ni jinsi gani CCM walivyokosa mbinu ya ku-deal na upinzani na matokeo yake hamahama hii sasa imegeuka kashifa kwa serikali ya awamu ya tano na ambayo wapinza wataitumia vizuri huko mbeleni.

Tuhuma zilizopo sasa ni wanasiasa hawa kunuuliwa na chama tawala (rushwa) kwa ushawishi wa fedha, vyeo, n.k na ushahidi wa kimazingira unathibitisha madai haya kwani ni kweli tunaona baadhi wanazawadiwa vyeo, wengine wakidaiwa kulipiwa madeni yao, n.k.Hii teyari ni kashifa kubwa kwa serikali hii ambayo inajinadi kupambana na rushwa.

Na katika mazingira yanayothibitisha kuwa ni kweli kuna biashara haramu inaendelea, katibu mwenezi wao,bwana Polepole; ametangaza deadline ya kukamilika kwa biashara hii(December mwaka huu) kwa awamu ya kwanza ambapo itaendelea tena 2020.

Tangazo hili pia ni ushahidi mwingine wa kimazingira kuwa ni kweli kuna biashara inaendelea maana kama ni kuunga mkono juhudi za Raisi, kwanini kuwe na deadline ya kuunga mkono hizo juhudi? Hapa ndio ile dhana yangu ya hawa watu kukosa maarifa inapojithibitisha kwa mara nyingine kwani wanajiumbua wenyewe.

Mwisho wa siku ni kuwa, hata wale ambao mwanzoni walikuwa hawataki kuamini kuwa kuna rushwa inaendelea, sasa nao wataanza kuamini kwa kuunganisha dots na matokeo yake "hamahama" hii sasa inageuka kuwa ni tuhuma (kashifa) ya rushwa kwa serikali hii ya awamu ya tano.

Kwa kifupi, hii ni kashifa walioitengeneza kwa mikono yao wenyewe kutokana na wao kukosa maarifa na kwa hakika itawatafuna siku zote za maisha yao kama zile za EPA, Richmond, Escrow na nyinine nyingi zilizowahi kuikumba CCM.

Nimalize kwa kusema, hamahama hii kwa upinzani is "a blessing in disguise" and nothing else.

Muda utathibitisha ni nani mnufaika wa hii hamahama kati ya CCM na upinzani.

Note:Baadhi ya hawa mamluki (mercenaries) mnaotuhumiwa kuwanunu, ndio watakaokuja kutoa siri (kuwahujumu) huko mbeleni na kuwaweka katika wakati mgumu sana na miongoni mwao ni wale mtakaokuja kuwatema.

Tuombe uzima.
 
Sasa hivi mambo yamekuwa magumu sana hususani kama ulikuwa kabiashara na wewe ni mbunge wa upinzani basi utasumbuliwa na kutishiwa kufilisiwa. Pili unatishwa kwamba usipohamia ccm haurudi tena bungeni kwa nguvu zote za dola. Sasa hivi nchi imegeuka cosovo haya ney wa mitego ameanza kuogopa ametunga wimbo ambao kwa mara ya kwanza amemsifu jpm kwamba maendeleo yako mbele. Nchi sasa imepigwa ganzi usiposifu tu mkulu utakuwa na hali ngumu!!!! E mungu kwa nini umetuingiza kwa giza hili nene na majanga makubwa!!!!
 
Katibu mkuu alimaliza kila kitu, ccm siyo chama cha siasa tena.
Screenshot_20181006-113049.jpg
 
Back
Top Bottom