Biashara ya FUSO ikoje wadau?

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Habari zenu wana JF
Naomba kuuliza kwa mwenye uzoefu na biashara ya FUSO. Nataka ninunue Fuso lianze kufanya kazi ya kusafirisha mizigo mikoan. Lakin kabla sijanunua ningependa kujua kwa kina zaidi jinsi biashara hii ilivyo.
 
Habari zenu wana JF
Naomba kuuliza kwa mwenye uzoefu na biashara ya FUSO. Nataka ninunue Fuso lianze kufanya kazi ya kusafirisha mizigo mikoan. Lakin kabla sijanunua ningependa kujua kwa kina zaidi jinsi biashara hii ilivyo.

Inalipa kama utakuwa msimamizi mwenyewe vinginevyo unawapa ulaji dereva na konta.

Unatakiwa umakini wa hali ya juu na uwe mchungu na mkali kweli kweli ukiwa lege lege utaletewa pesa kidichu.

Ni biashara nzuri kwa wale ambao hawana majukumu mengine
 
usijaribu biashara ya Transportation kama unafanya part time,i.e umeajiriwa mahali pengine na hii iwe kazi ya pembeni.
utapata hasara kubwa mnoo.na usisikilize ushauri wa Dereva/fundi/utingo ukiambiwa kuwa inalipa sana.biashara hii inalipa kwa wao wanaofanya kazi ktk chombo na siyo mmiliki.

watafute wamiliki wa fuso/basi watakwambia ukweli.na wengi waliofanikiwa ktk hii biashara ni wale wanaofanya hii biashara on full time basis.
kwani gari likiharibika -wanasimamia kwa karibu matengenezo,limepata ajali anakwenda mwenyewe or anamtuma mtu wa karibu.kutafuta mizigo/wateja unakomaa mwenyewe.ukifanya hivyo ndo utaona biashara hii inalipa na utaweza kuzalisha pesa nzuri.
 
Back
Top Bottom