Biashara ya Duka la Jumla

Habari zenu wanaJF

Natumaini kila mtu yupo salama, Naombeni msaada wenu kuhusiana na biashara ya Duka la jumla la vyakula..vitu kama mchele, unga wa sembe na ngano, pasta, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi...n.k

yaani vitu vyote vinavyohusiana na maakuli..kama kuna mtu anauzoefu na hii biashara nilikuwa naomba ushauri, kuhusu changamoto zake, faida zake na upatikanaji wa mzigo kutoka kwa wasambazaji wakubwa, maana mimi nipo mwanza na sina muda mrefu sana huku..pia minimum capital ambayo unaweza ukaanza nayo..

Ahsanteni sana kwa mchango wenu.....
 
Mimi pia mkuu nataka nianzee hii biashara ya duka la jumla maeneo ya ubungo. Nina 18 mills, ila bado nafanya uchunguzi wa biashara hii.
 
Kwa uchunguz bidhaa zinazotoka sana kwa jumla jumla. Unga, mchele, sabuni, mapampers, maji ya azam, juice za azam na mo, mafuta ya madumu lita 3,5,20
 
Amani iwe kwenu wadau. Naomba msaada kwa wenye uzoefu. Nimejibana hadi nimedikisha m20. Nataka nianzishe bihashara ya duka la jumla la vyakula mf mchele, sukari, mafuta....nk. Inawezekana? Duka atalisimamia wife. Niaaidie mawazo au idea nyingine nione km naweza kutoka kimaisha. Karibu sana wadau na wataalamu wote. Duka nalifungua mkoani. Hiyo m20 ni mtaji kodi ya frem na tra na leseni ya bihashara ni nje ya mtaji. Asante
 
Inatosha kabisa mkuu Utaanza na vile vya msingi ukipiga faida siku nyingine ila cha msingi tu usisahau kuweka pombe inatoka fasta na sigara. Nina uzoefu na hii kazi sister angu alifungua mwaka juzi mpk kesho analo.
 
Mkuu pata ushauri kwanza humu then ntakupm...nataka kusupply ikiwa umeshasema unalima mwenyewe
 
Asante sana kwa ushauri,mimi mchele nalima mwenyewe mpunga nalimia mbeya,hivo nakuwa nauza mchele kutoka mbeya.

Pia sijakuelewa kuhusu wenyeviti wa masoko..kwamba wao watanisaidia kujua bei za mchele kwa soko husika,hao wenye viti wanakuwa na uzoefu wa kiasi hicho, of course its true unavoniambia nisifungue kwanza duka nifanye survey ya bei kwani nnaweza nikauza kwa jumla moja kwa moja sokoni kuliko kutafuta frame.


Pia nilikuwa naomba kama kuna mtu yyte ana connection na watu wa mashule ya boarding niweze kusupply mchele.
Tuwasiliane 0763370175
 
Natamani sana kuanzisha biashara ya duka la jumla lakini sijajua kwamba ni mtaji kiasi gani natakiwa niwe nao ili niweze kuanzisha biashara hyo

2. Changamoto za biashara hyo
 
Natamani sana kuanzisha biashara ya duka la jumla lakini sijajua kwamba ni mtaji kiasi gani natakiwa niwe nao ili niweze kuanzisha biashara hyo
2.changamoto za biashara hyo
Rafiki kuna siku utajua kuandika vyema tu. Maana na mimi nilianza hivi hivi kuboronga hadi sasa sijajiamini lakini naelekeza kidogo.
 
Back
Top Bottom