Mm nipo kwenye hii biashara kitambo lkn sio sana kihivyo! Wengi wanadhani kununua gari bei kubwa ndio uzima wa gari wakati sio! unaweza ukanunua hiace 25ml na bado ikawa kimeo! Ngoja ni share jinsi mm navyoendesha biashara hii.
Kwa kifupi mm huwa sinunui hiace mpya ila nachofanya huwa nanunua bodi nzuri ya hiace kisha nafunga engine mpya pamoja na gear box yake kisha matairi mapya na service za bodi gari inasimamia 10-12ml, miezi sita tu kishaeleweka,kwa uzoefu wangu sitanunua Hiace mpya milele! Kama gari ni engine na engine complete ni 7.5ml, je ukinunua hiace 25ml ukitoa 7.5ml bodi utakuwa umenunua bei gani?
Japokuwa wapo wataoponda mchango huu lkn mm kila mwaka naona mambo yanajipa.....ni hayo2
Sikubaliani na Mtoto tajiri, hii njia anayoisema ni ngumu sana, tena utajuta. Kabla siajaanza kununua used kutoka Japan nilikuwa nafanya hivyo. Tofauti ni kubwa mno kwenye uendeshaji. Asikuambie mtu,gari hasa daladala ni zaidi ya injini. Wewe jipange nunua gari ambayo mafundi wetu hapa nyumbani hawajaigusa sana au used Japan. Zaidi ya hapo utanufaisha, dereva, konda, fundi na wauza spea na wewe hautapata kitu.
Legend,kuna uzi ulichambua magari hayo kwa kina sana,we search utaukuta umechambuliwa kitaalam.jaman mm nataka ushauri kuhusu magar aina ya eicher na tata, jinsi ya kuyahandle ndugu Zanzibar vp hapo una mchango wwte
Wadau nataka nifanye biashara ya Usafiri hapa mjini Mwenye uzoefu anipe Maujanja itani cost how much ili niweze kupata Two Used Costa kwa ajili ya kuanza biashara Pia naomba unipe Overview Costa moja inarudisha bei gani kwa siku... Nini matatizo yake hii biashara!
Wadau,
Nataka nifanye biashara ya Usafiri hapa mjini, mwenye uzoefu anipe maujanja itani cost how much ili niweze kupata two used Costa kwa ajili ya kuanza biashara. Pia naomba unipe Overview Costa moja inarudisha bei gani kwa siku na nini matatizo yake hii biashara.
Mm pia nipo kwenye biashara hii ya Daladala,kwa kifupi ukiogopa changamoto biashara hii utaona ni chungu sana,Ngoja ni share nanyi changamoto nilizopitia katika biashara hii,mara ya kwanza kabisa kununua hiace nikafanya taratibu zote vya vibali kisha nikaingiza barabarani gari ikafanya kazi siku mbili ya tatu ikapata ajali mbaya sana na baada ya hapo ikakaa gereji mwezi mzima niligharimu kama 1m kunyoosha bodi na mambo mengine,baada ya hapo gari ikaingia tena barabarani ikafanya kazi miezi mitatu ikaanza kula oil nikaifanyia overhaul ikagharimu kama Laki7,baada ya hapo gari ikaingia tena mzigoni ikafanya kazi miezi miwili ikanok engine ni mengi tu nayoweza kushare na ninyi lkn kwasababu ya muda naachia hapo,lkn hadi sasa nipo kwenye hii biashara ya Daladala
Natoa shukurani zangu kwa wote waliochangia mawazo. Nakubaliana na ukweli kuwa biashara ya daladala kwetu tunaofanya kazi ni ngumu mno.
Nimeanza kufanyia kazi wazo la kutafuta tenda za shule, so km kuna mwenye link si mbaya akaniunganisha.
Changamoto tuliyonayo ni kufahamishana juu ya ni biashara gani mfanyakazi anaweza kufanya na ni zipi amabazo zitamuweka katika wakati mgu kama mfanyakazi (I.e. zinahitaji very close supervision)
Naendelea kupokea mawazo yenu wakuu.
Hongera sana mkuu, unaweza ku share nasi jinsi ulivyoweza kuisimamia biashara yako vizuri hadi mpaka sasa inakuwezesha kupata gari ya tatu. Pia naomba kujua Zanzibar unanua sh ngapi, gharama zote hadi inaingia barabarani kuanza kazi ina range kwenye sh ngapi na pia kwa siku dereva analeta sh ngapia. Pole kwa maswali mengimkuuBiashara ya usafirishaji ni ngumu sana.,usipoielewa na ukaingia kichwa kichwa..,
Vitu vilivyowafanya watu weng kukwama katika hii biashara ni
1. Dereva makini
2.usimamizi wako katika gari lako
3. Services
4. Kula yako na maisha yako kutegemea kipande cha siku....
Niliiogopa sana hii biashara but namshukuru mungu nilikwenda Zanzibar nikapata Nissan Carvan used safi.,nikaiweka barabara leo ni mwaka wa 3.,cjagusa engine wala gear box,wala diff,na imeshanipa gari nyingine Nissan carvan ya pili na najiandaa kutoa ya 3 mwezi may mwaka huu 2016.