Biashara ya daladala(hiace) Zimbabwe

the-true-wash

Senior Member
Oct 14, 2012
142
107
Guys juzi juzi nilikua Zimbabwe napenda ku-share nanyi kwamba kule biashara hii inalipa sana.
Kwa siku hiace (high/super roof) inaingiza 80$ na flat base inaingiza 60$.
Changamkieni.
 
Kabla ya kuwaza Zimbabwe, ebu mwenye data za hapa hapa Tanzania atuambie hice inawezakuingiza ngapi. Hapo tungeweza kulinganisha
 
Hapa Tanzania unanunua hiace milioni 25, inachukua watu 15 wakilipa nauli ya tshs 400,
hapo toa hesabu ya mafuta, service, mshahara, mapato, bima, road licence, faini na rushwa,
mpaka urudishe hela yako uliyonunulia nadhani ni miaka 2 (hapo hujaipunguza kwa kuzingatia ile kanuni ya time value of money)

mara 10 hiyo hela ukafanyie kilimo
 
Duuuuh! Bei ya hiace imefika huko kweli?

Hapa Tanzania unanunua hiace milioni 25, inachukua watu 15 wakilipa nauli ya tshs 400,
hapo toa hesabu ya mafuta, service, mshahara, mapato, bima, road licence, faini na rushwa,
mpaka urudishe hela yako uliyonunulia nadhani ni miaka 2 (hapo hujaipunguza kwa kuzingatia ile kanuni ya time value of money)

mara 10 hiyo hela ukafanyie kilimo
 
washona na wandebere wenyewe tuu wanabaguana na sheria ya Mugabe huwezi fanya biashara mpaka uwe na ubia na Raia wa pale nadhani ni ngumu kidogo kwa mgeni kufanya local business pale labda uwe ufanye ya kuwatoa South Africa na Tanzania kwa bus kubwa izo pia rushwa barabarani utasumbuliwa sana..
 
Kule ninayo moja. Kuhusu ubaguzi usiwaze. Hawana ubaguzi wale. Ukiwa na hiace drivers kibao watakuja. Weka target yako kwa siku basi mambo yanaenda.
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Hiace inakulipa ndani ya Mwaka na nusu tu tusitishane.
Na sio kwamba kila bishara mtu afanye,unafanya unayopenda,sasa jiulize inakuwaje mtu ananunua moja then anaongeza nyingine?ukiwa bahili wa kuhudumia gari basi itakushinda na wengi wanafeli hapo.
Pia,mleta uzi umekurupuka,hakuna sheria itakuruhusu kirahisi Foreigner kufanya biashara ya Kidalala chako cha mawazo,inaruhusiwa ni Kampuni tu na lazima uonyeshe Mtaji wa kutosha na mipango ya Kampuni,so ni mamilioni ya pesa.
 
Zanzibar spices mbona unamvamia jamaa katoa wazo zuri tuu kuwa kuna biashara kule wewe unakujana maneno mengi mbona watanzania wengi tuu wapo Harare na Bulawayo wana miradi midogo na mikubwa kama haujui kitu usijibu kwa uhakika mimi binafsi nawajua watu waliounga unga mpaka sasa wana mabus yanatoka Harare to jozi na harare mpaka messina...
 
Hiace inakulipa ndani ya Mwaka na nusu tu tusitishane.
Na sio kwamba kila bishara mtu afanye,unafanya unayopenda,sasa jiulize inakuwaje mtu ananunua moja then anaongeza nyingine?ukiwa bahili wa kuhudumia gari basi itakushinda na wengi wanafeli hapo.
Pia,mleta uzi umekurupuka,hakuna sheria itakuruhusu kirahisi Foreigner kufanya biashara ya Kidalala chako cha mawazo,inaruhusiwa ni Kampuni tu na lazima uonyeshe Mtaji wa kutosha na mipango ya Kampuni,so ni mamilioni ya pesa.
Acha mambo yako ya Kijinga jinga watu wasifanye Business kisa Mitaji afu PIA Kama hujui au hizo hela za kununua Hiece soma Comments za wanaume wenzio sepa .
 
Guys juzi juzi nilikua Zimbabwe napenda ku-share nanyi kwamba kule biashara hii inalipa sana.
Kwa siku hiace (high/super roof) inaingiza 80$ na flat base inaingiza 60$.
Changamkieni.
Ahsante Sana Mkuu hata mi nasikia inalipa Sana per day Unacheza na 100$ mpaka 80$ ngoja kwanza nistue wenye Nazo wachangamkie fursa.
 
Wakuu nitukaneni mjuavyo
Lakini mjue kwamba hata hao wanaofanya ni kwamba wameishi muda mrefu na wanavibali maalum ikiwemo Residents permit,na kama hawana basi ipo siku tu watajua nini ninachoongea.
Ni Sawa na Zanzibar,ni kwamba hata Mkenya haruhusiwi kufungua hata Salon,na hizi zimeacha ku protect Local People waweze kuzifanya wao wenyewe.La sivyo Nchi ikiruhusu kila kitu mgeni afanye basi itakuwa Nchi ya kihuni .
Ulizeni sheria za nchi mtajua hilo msifanye biashara kwa mazoea mwisho wa siku mtakuja kuchekea macho.

Back
Top Bottom