Biashara ya branding na marketing agency

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,144
Wakuu napenda wenye kuijua hii biashara ya branding na marketing agency/promotions.

Tupeane ujuzi maana ni biashara ninayotaka kuifanya maana makampuni mengi yana outsource marketing/ promotion ya bidhaa zao au uzinduzi wa chupa mpya na ukipata makampuni makubwa unavuta pesa ndefu.

Tupeane ma-idea ya namna ya kufanya hasa kwa tunaotamani kufanya hii biashara.
 
Focus katika ku solve matatizo ya wateja wako na utapata mafanikio makubwa.

Makampuni ya marketing agency yamejaa tele lakini wenye taaluma ya kuwaongezea wateja clients wao ni wachache mno.

Uki master How To Acquire customers for you target audience basi hutohangaika.
 
Thanks kwa insight Dr., nadhani wengi wakianza kufunguka inaweza kutoa mwanga zaidi hata kujua matatizo yaliyopo kwenye hii industry ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri kukamatia
 
maroon7 mkuu binafsi sijawahi kuifanya hii biashara lakini ninaomba nitoe input yangu kidogo kwa upande ambao binafasi nimewahi kuishiriki.

Kifupi ni biashara nzuri sana, kikubwa inahitaji ubunifu (creativity) kwa kiasi kikubwa. Lengo kuu la kuifanya hii kazi ni kuongeza ufahamu (awareness) ya huduma ama bidhaa kwa lengo la kuongeza wateja ama mauzo kwa mteja (client) wako. Hii inajumuisha vitu vingi ikiwemo promosheni (promotions), kampeni za kimasoko (marketing campaigns), mashindano (contests) na kadhalika.

Mimi nimewahi kushiriki hii kazi kwenye kampuni chache na hasa kazi yangu ni kubuni mawazo (ideas) na kuziandikia mapendekezo (proposals). Observation nilizoona mimi binafsi nilipofanya kazi kwenye hizi kampuni ni kama ifuatavyo:

1. Uwe umejipanga (Be organized). Kuwa na ofisi nzuri inayojiuza yenyewe. Ipendeze, iwe na mpangilio mzuri na kiofisi na kikazi, ikiwemo uwe na vitendea kazi vyote stahiki.
2. Kuwa na timu nzuri ya wabunifu. (Have a great creative team). Sio lazima uwe umewaajiri, unaweza kuwalipa kwa commission kila unapohitaji ushauri (consultancy) au ingizo/mchango wao (input). Kikubwa mtambue kila mmoja na mheshimu kwa nafasi (role) yake. Marketing inahitaji sana ubunifu ili kuliteka soko.
3. Uwe mbele hatua kadhaa (Be a few steps ahead). Hii biashara inahitaji uwe mchambuzi mzuri sana wa mwenendo (trend) ya vitu vingi hasa vinavyohitaji kufanyiwa marketing. Uwe mwepesi kuona mapengo (gaps) kwenye biashara kiujumla lakini katika upana wa kazi unayotaka kufanya. Uwe na taarifa za kutosha (be well informed) ili unapoingia kazini (field) ufanye kwa uhakika zaidi ili mteja (client) wako aweze kupata matokeo anayotarajia (expected results) kutokana na kazi yako.

Baaad ya hapa kuna kipengele cha KUTAFUTA NA KUPATA KAZI/TENDA. Hapa ni uwezo wako binafsi kupambana ili uweze kupata tenda kwa ajili ya kampuni yako. WOTE niliowafanyia kazi kwenye hizi kampuni wana mtandao mkubwa sana wa wadau wanaofanya hizi kazi. Wanawasiliana kwa karibu sana na Marketing Managers, Procurements Managers na wenye vyeo vinavyoweza kupitisha tenda ama kazi (in English: Decision Makers). Kuwa na kampuni nzuri iliyojipanga halafu tenda hupati itakuwa si jambo zuri.

Binafsi huu ndio mchango wangu mkuu, kiukweli nimeiona ni ni biashara nzuri na ninakutakia heri.
 
Mkuu asante kwa input yako muhimu....nimegundua pia lazma uwe na capital ya kutosha kutengeneza ofisi nzuri inayojiuza yenyewe na hapo ndio changamoto mojawapo maana huwezi kuwa na kaofisi ka chumba kimoja ukawavutia wadau hata kama unauwezo wa kuifanya kazi unaweza usiipate. Hapo kwenye kuwa creative ni kwamba wao ndio wanakuletea kazi mfano labda tigo wanavyopromote kifurushi kipya sio kwamba wao wanakupa namna ya kuipromote au ni wewe unacome up na njia effective ya kupromote wao waone matokeo tu.
 
Mimi ni mwanafunzi kutoka Street University. Naomba nafasi nipate shule hapa. Asanteni.
 
Mkuu asante kwa input yako muhimu....nimegundua pia lazma uwe na capital ya kutosha kutengeneza ofisi nzuri inayojiuza yenyewe na hapo ndio changamoto mojawapo maana huwezi kuwa na kaofisi ka chumba kimoja ukawavutia wadau hata kama unauwezo wa kuifanya kazi unaweza usiipate. Hapo kwenye kuwa creative ni kwamba wao ndio wanakuletea kazi mfano labda tigo wanavyopromote kifurushi kipya sio kwamba wao wanakupa namna ya kuipromote au ni wewe unacome up na njia effective ya kupromote wao waone matokeo tu.
Kwenye moja ya makampuni niliyowafanyia kazi wanachofanya ni kama ifuatavyo:

Mfano kampuni moja ya simu inahitaji kuingiza kifurushi kipya kwenye moja ya huduma zake, wanachofanya:
1. Marketing Manager wa kampuni anawasiliana na kampuni za marketing moja ama zaidi. Ataeleza Asili (nature) ya kifurushi chake halafu ataagiza kampuni ije na "concept" (samahani sijui neno "concept" kwa kiswahili wanasemaje). Concept inabeba dhima "theme" nzima ya kufanya promotion ya hicho kifurushi ili kitangazwe.

2. Kampuni ya marketing watatengeneza "concept" itakayobeba dhima (theme) ya hicho kifurushi, na kitagawanywa katika makundi ambayo ni i) JINGLE: hili ni tangazo la redio, ii) PRINT: Hili ni design ya tangazo la kuwekwa kwenye magazeti, majarida na vipeperushi, billboard n. iii) DIGITAL: Haya ni matangazo yatakayowekwa kwenye mitandao na ndani ya apps iv) BROADCAST: Hili ni tangazo ambalo hurushwa kwenye TV na "streaming" channels zingine. Angalizo ni kuwa matangazo yote haya yatalenga kutangaza kifurushi kimoja na yatatoa taarifa inayofanana.

3. Kampuni ya marketing itawasilisha "concept" waliyoandaa kwa kampuni ya simu, nao bodi yao ya masoko itajadili na aidha itapitisha, itarejesha kwa marekebisho ama itakataa kazi iliyoandaliwa. IWAPO kazi itakubaliwa basi utaratibu utafanyika ili matangazo yaende kwenye vyombo vya habari.

Naomba nidokeze tu kuwa hii ni moja ya mfumo (model) ambao unatumika kufanikisha lengo la kutambulisha kifurushi kipya cha kampuni fulani ya simu, kama nilivyoeleza kuwa ni mfano.

Natarajia utakuwa umepata chochcote hapo mkuu
 
Mkuu umetisha sana kwa haya maelezo yako hakika umenifungua sana kwenye hili.... Asante sana natumai hutochoka kushare zaidi experience yako. Maana umeniongezea kitu kikubwa kwenye ufaham kwamba ofisi lazma iwe na graphics designers mbali na kuwa na watu wengine wa kufanya promotion na ishu zingine muhimu...kwa hiyo mnaposubmit concept mnaweka na budget ya kazi nzima au mteja ndio anasema kazi iwe ya budget gani
 
Nitajitahidi kushare kadri navyoweza, mimi mwenyewe nipo JF kujifunza na kuongeza chochote kichwani.

Kuhusu budget mara nyingi kampuni inayotengeneza hayo matangazo wanapeleka "quotation" yao. Pia kampuni yenye uhitaji wa matangazo wanaweza wakawa na limited budget kwahyo kampuni ya marketing wanaweza kukubali kuifanya hyo kazi ama kuikataa kutokana na mchanganuo wao gharama na namna watakavyopata faida. Of course kwenye masuala ya kibiashara karibia kila kitu kiko negotiable.

Tuko pamoja mkuu.
 
Asante sana mkuu..stay blessed...nikipata ishu ntakuuliza kama utakua na experience nacho
 
Back
Top Bottom