Biashara poa kabisa!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Njoroge alienda kijiji X kwa malengo ya kununua nyani. Alikuwa ananunua nyani mmoja kwa sh.10000.Watu kibao walivamia mapori kukamata nyani na kwenda kumuuzia huyu bwana.Baada ya wiki 2,wauza nyani wakaanza kupungua. Njoroge akaongeza dau mpaka 25000 kwa kila nyani. Wanakijiji wakavamia mapori na kuwasaka nyani kwa udi na uvumba.Lakini baada ya muda fulani kupita,supply ya nyani ikapungua kutokana na nyani kuadimika maporini.Baadaye akapandisha tena dau mpaka sh.50000 halafu akaenda zake mjini na kumwachia mlinzi wake jukumu la kununua nyani.Yule mlinzi akawaita wanakijiji na kuwapa dili la kuwauzia nyani waliokuwa wamehifadhiwa kwenye makontena ya bwana njoroge kwa sh.40000 ili siku njoroge akirudi,wale wanakijiji wamuuzie tena wale nyani kwa sh.50000.Wanakijiji kibao walifurika na kuwanunua nyani karibu wote ili waje wamuuzie njoroge kwa faida.Baada ya kuwauza wale nyani kwa sh.40000 kila mmoja,si yule mlinzi wala Mr.njoroge,hakuna aliyeonekana tena pale kijijini.Kijiji kizima kizima kilitawaliwa na makelele ya manyani yasiyokuwa na soko.
 
Hii ndio ilivyokuwa biashara ya Rupia na noti za zamani ya Shs. 100 zenye picha ya mmasai, mwisho wa siku walibaki na hela ambazo hawakujua pa kuzipeleka.
 
Biashara ya mtindo huu tanzania ilitokea. kuna watu walidai nchini kenya shilingi yenye sura ya mwinyi inatafutwa kwa fedha nyingi. Bei ikawa inapanda kila kukicha, watu wakanunu nyingi na baadae soko likawa hakuna. hakili kukichwa
 
Biashara ya mtindo huu tanzania ilitokea. kuna watu walidai nchini kenya shilingi yenye sura ya mwinyi inatafutwa kwa fedha nyingi. Bei ikawa inapanda kila kukicha, watu wakanunu nyingi na baadae soko likawa hakuna. hakili kukichwa
Tamaa mbaya.
 
Hii story naifananisha na ya aliyekuwa waziri wa maliyasiri Maige baada ya kupigwa chini kila siku hakosi la kuongea. Umenichekesha sana
 
Back
Top Bottom