Biashara magendo ya fedha za kigeni inashamiri kwa kasi !

Watu walitajirika sana enzi za magendo zama za Giza naona wamerudishiwa kutajirika tena
 
Jinga kweli wewe,hujui lolote zaidi ya kula na kulala sebuleni kwa Shemeji yako
 
I wish unipatie na mimi hiyo namba namba maana ninashida kinoma ya kupata dollar!!!Kama hautojali nicheki PM tuyajenge maana mzee baba kashafanya yake huku kwenye njia halali
 
Export ya bidhaa zisizo na kodi itashamiri sana mipakani watu kwenda kubadili DOLA na safari manunuzi bidhaa nje ya nchi. Hata China Kuna bureal mtaani za kutosha. China hawateseki sana na thamani Pesa yao,wao focus yao balance of trade.
Pia hawatumii nguvu kubwa kuthibiti wafanyabiashara wadogo ndio maana copy ni nyingi, hasa kwa bidhaa nchi maskini.
 
Arusha ndio michezo yao. Mwisho was siku, utakuta dola zipo mtaani na mabank hayana dola
Wafanyabiashara wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni walianzia kwenye black market serikali ilichowafanyia ni kama mmewasaidia kukuza biashara zao😎
 
Jiulize tu mitutu ya bunduki na biashara wapi na wapi
Kwa kweli inahitaji elimu ifanye kazi badala ya mitutu.
Huwezi amini kuna watu wanaishi ulaya huku wakiishi Tanzania kwa sababu ya technology ukitumia mtutu huwezi tambua.
Come on leaders wake up!
Kuna elimu kubwa sana mtaani imezagaa bila matumizi unadhani watakula vipi hawa na maelimu yao kama sio huku.
Think wide
 
Hahaha serikali imeshtuka watu wananunua dollar wanafukia, ukitunza shilingi inakula kwako.
 
Ngoja ukishikwa na hizo dollars halafu hauna risiti ya manunuzi yake. Ndiyo utaelewa uzuri wake.
Ndiyo wanakuja kulia humu sijui serikali iache unyang'anyi wa kidola..!! mara wanachukua hela za watu kimabavu kwenye A/C zao yaani sijui Watanzania tupoje..!!
 
The best solution ni kuhakikisha inawekea mifumo sahihi na thabiti ya kuzuia biashara hii ya magendo kwani kwa asili binadamu kaumbwa na ubinafsi. Sheria, taratibu, kanuni na miongozo viliwekwa ili kudhibiti mienendo ya mwanadanu ikiwemo ubinafsi
 
Wanyonge kwanza wale waliotupora kwenye EPA, IPTL, ESCROW, MEREMETA, RADAR, FERRY, MAJUMBA YA SEREKALI NK, kisha ndio mje mumalize na huyo, hapo ndio tutakuelewa. Vinginevyo ni unafiki tu hamna lolote.
 
Sasa mkuu, how would you know kuwa fedha ukizouziwa sio feki? Nadhani moja ya vitu vinavyochochea rushwa/uhalifu ni willful participation kama yako
 
Kama vya halali hatuvipati bora twende na vya haramu tu hakuna namna.
 
Kufurahia nchi kukosa mapato ni upunguani. Hata Mtanzania kukwepa kulipa kodi ni uhujumu uchumi. Kwa nini hatujifunzi kuwa wazalendo kwa taifa letu? Shame on you uliyejisifu kwa kuikosesha nchi mapato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…