aminiusiamini
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,577
- 2,224
Awali ya yote.Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi hii.
Pili,nina imani nitaeleweka na maamlaka husika itatoa au kufanya maamuzi sahihi juu ya kero hii na swala hili.
Kero yangu leo hii ni uwepo wa maduka na mabar na kila aina ya biashara sehemu ambazo sio rasmi.Hapa naongelea zaidi mkoa wa dar es salaam.
Naomba mkuu wa mkoa Mh Paul Makonda uingilie hili jambo.
Sehemu ya makazi zimekuwa kona ya kila uovu na hasara na zisizo salama kabisa kutokana kwamba watu wa waina mbali mbali kujikusanya sehemu moja na kusababisha usumbufu wa kila aina kama makelele na hata barabara kuendelea kuharibika.
Uharibifu,foleni nk ndio zao la hizi biashara ambazo zimetapakaa kila kona ya mtaa wa jiji haswa kwenye makazi ya watu.
Naomba jiji liwe na utaratibu. Haiwezekani mtu kuanzisha bar mbele ya jumba lake au genge. Nenda maeneo ya Mbezi utaona hili.Unakuta mtu jumba zuri kaweka genge na duka hapo.
Nathani pia watu hawajui thamani ya real eastate inatokana na kitu gani. Mfano kuna watu wameharibu masaki kama ilivyopaswa kuwa. Sasa hv masaki ni kama uswahilini. Jamani watz tunaenda wapi?
Ni jukumu la kila mmoja kuhifathi mazingira yake na yale yanayomzunguka.
Naomba kutengwe sehemu maalumu kwajili ya maduka na kuwe parking na vyoo.
Naomba serikali ingalie hiili sana tutakuta tunapunguza uhalifu na kubanana pasipo ulazima wowote.
Ukienda nchi za watu hata hapo Kenya hawana ujinga kama wetu katika sehemu za makazi ya wtu yaliyo rasmi.Huko mbele ndio kabisa.
Makonda naomba usikie kilio changu.
Wako Mfia nchi.