Biashara imekuwa ngumu kuliko kawaida!!!

rbsharia

Member
Sep 14, 2011
41
6
Inasemekana hapa Tanzania biashara imekuwa ngumu kuliko siku za nyuma.
Hii inaweza ikawa kweli au la.
Kwa ninyi wenye ufahamu na uzoefu wa biashara, je suala hili ni kweli?
 
Inasemekana hapa Tanzania biashara imekuwa ngumu kuliko siku za nyuma.
Hii inaweza ikawa kweli au la.
Kwa ninyi wenye ufahamu na uzoefu wa biashara, je suala hili ni kweli?

Inategemea biashara unayofanya; kama ni ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Tanzania au imported from Europe and America biashara ni ngumu kwa sababu ya bidhaa za bei nafuu (fake products) toka bara la Asia - China, Singapore na kwingineko. Wanaoingiza bidhaa toka bara asia, mambo ni mazuri sana kwao na ghorofa zinaota kama njugu
 
Kwa mgao huu wa umeme biashara zilizo ngingi haziwezi kuwa rahisi hata kidogo kwa umeme/power unaeffect nyingi kwenye shughuli za biashara
 
si mlichagua maisha bora kwa kila mtanganyika -- sasa mnaanza kulalamika nini - tulieni mliwe.
 
kwakweli suala la umeme limeathiri biashara nyingi sana ukizingatia auna ratiba kabisa nfano kkoo wiki nzima kuna lina aipati umeme siku nzima jumapili tu ndio unakuwepo siku nzima siku nnyingine unarudi ucku ebu fikiria hali kama hyo
 
Hauna.... Haipati.......
 
mkilindy umeamua kumkomoa rbsharia?
Unamshauri afue umeme wa upepo, je mtaji wa ankara anao?
 
Inategemea biashara unayofanya; kama ni ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Tanzania au imported from Europe and America biashara ni ngumu kwa sababu ya bidhaa za bei nafuu (fake products) toka bara la Asia - China, Singapore na kwingineko. Wanaoingiza bidhaa toka bara asia, mambo ni mazuri sana kwao na ghorofa zinaota kama njugu
Mkuu umenena, umeweka ujumbe mfupi lakini ni zito sana kwa wafanyabiashara na wateja.
Siku moja nilikuwa naongea na mtaalamu mmoja wa marketing, nikamweleza juu ya China et al na bidhaa zinazotengenezwa kwa ajili ya afrika, yeye alisema "for consumers in africa who cares if the product is of hight quality, or last longer rather than the lowest possible price" kwa hiyo kwa wale wafanya biashara waliong'amua mapema juu ya hili wametengeneza pesa kweli.
 
Tatizo la ugumu wa biashara Tanzania linasababishwa na mambo mawili makuu, kwa wale wanaonunua biashara nnje kikwazo kikubwa ni Dola,Nitatoa mfano:Ukinunua bidhaa nje kwa dola 100USD,ambayo nisawa na 150,000Tsh. tujaalie ni mwezi wa may, 2011,uliuza bidhaa hiyo kwa 180,000.utaona umeingiza faida 30,000, sio mbaya.lakini mwezi wa oct, 2011 unataka ukanunue tena hile bidha ili uje uuze tena ukienda kununu dola utaikuta imepanda kutoka 150,000 hadi kufikia 180,000 kuinunua wewe ,inamaana ile fada amboyo iliipata imekufa na umerudisha gharama tu kama hujala hasara. sasa unakua unafanya kazi bure au kwa hasara, kwa mpango huu lazima biashara iwe ngumu.

kwa wale wenye mitaji mikubwa ndio huendelea kwa sababu wao hununua vitu bei ya chini pengine kwa order ya kontena moja au mawili sasa lile tatizo la dola kupanda wao huwaathiri gidogo sana.

Ama kwa wafanya biashara ya ndani ni mitaji huwa ndio tatizo,kwa mfano: mahidi yanapokua kwa wingi hua yanashuka bei,sasa faida hua ndogo sana kwani ushindani huamkubwa,na mahindi yakiisha msimu yanakua ghali sana kiasi ambacho wafanya biashara wadogo wanashindwa kuyanunua na hata akiyanunua kwa kutumia ule mtaji mdogo basi atashindwa transport, sasa hapa ndio biashara hua ngumu, lakini kwa wenye mitaji hupeta kwa kua wao hununua kwawingi hule muda wa msimu na msimu ukimalizika yeye ndio anauza mali yake.

Kwa kujibu kwakutumia neno moja linalo yaunganisha maelezo yangu nikua MTAJI NDIO TATIZO katika biashara za kibongo.

mambo mengine madogo madogo ndio hayo ya umeme,kuenea kwa bidhaa feki pia kunachangia biashara kua ngumu,udhibiti wa bei serekalini pia huchangia,rushua pia nitatizo kwasababu mwenye makontena matano ya atatoa rushua bandarini alipe milioni tano ambayo sisawa na ushuru wa kontena moja,lakini mwenye kontena moja atalipa hio hio milioni tano,sasa yule mwenye kontena tano atakushinda uwanjani,wewe utauza bidhaa kwa 1000 na yeye bidhaa hio hio atauza 300 sasa kwanini biashara isiwe ngumu? na yako mambo mengi mengine pia ufahamu wa wateja mtu atahiari anunue feki kwa rahisi kuliko kununua original kwa kwa bei kubwa kidogo.
 
Back
Top Bottom