Bia Tamuuuuuu!

Offline User

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
3,828
Reaction score
2,396
Mbona mimi nikinywa naona chungu? Na asubuhi naamka nimechoooooka hata taste ya kula nakua sina! Utamu wake uko wapi? Nijuzeni wadau!
 
We una bahati sana na usichezee hiyo bahati. Wote tumetoka hukohuko hiyo ndio nafasi yako ya rahisi kushinda zote kwa ajili ya kuacha pombe, shauri yako.
 
Ukiwa nywaji bia, na Jehanum pia utazinywa sanaaa. Kama kwa mwezi hapa duniani unakunywa 40 basi baada ya kufa utakunywa 200. Fanya uchafu uwezavyo ili upate kulipwa kwa kadri ya matendo yako.
 
utamu wake unajikuta unaweza kuongea lugha yoyote hata kama wewe mwenyewe huijui.
Nalog off
 
Sio kuongea tu, bali unaweza kumpa mtu tigo akapiga mpaka salio likaisha bila wewe kujua
 
bia au pombe zote si nzuri ingawa tunazinywa , hapo shetani ndiyo ametushika pazuri kweli kweli na ujanja wetu wa elimu lakini kwa bia hatuachi . kuhusu kupata uchovu na mafinyo finyo ya pombe ni kwamba mwili wako uko fiti kila sector yaani hautaki sumu na ndiyo maana wengine wanatapika ,kwa wale magwiji utasikia hata hangover hawana hapo ndipo ujue ini lipo katika hatari kubwa yaani halichagui tena (detoxification) vinaingia vyote na hapo ndipo mara nyingi unakuwa katika absolute cheers na mwanzo wa kunywa you dont find inebriated after few beers , inabidi uache mara moja kwani ugonjwa wa cirhosis unakunyemelea
 
Walevi mbwa lazima wafurahie hii kitu... Utamu hutestiwa na ulimi na utamu ni kitu kilicho kitamu sweets sasa bia haiwezi kuwa tamu Bia ni Chungu mwanzo mwisho... ila Tatizo Shetani ndio huwaduwaza na kuwashawishi wanywaji wabadilishe jina la uchungu kuwa Tamu kwa sababu Shetani ni Kinara wa Kubadilisha Majina au maelezo.... so Wanaosema Bia ni Tamu ni watu wa Shetani....

Watoto wadogo huitwa Malaika na ili kuthibitisha hilo Mpe Mtoto aonje bia kisha muulize Bia ni Tamu? Lazima akatae kwa sababu ni Malaika wa Mungu na Jitu zima la Shetani lilevi liulize Bia kama Ni Tamu litakuambia ni Tamu lol
 
Ukiwa nywaji bia, na Jehanum pia utazinywa sanaaa. Kama kwa mwezi hapa duniani unakunywa 40 basi baada ya kufa utakunywa 200. Fanya uchafu uwezavyo ili upate kulipwa kwa kadri ya matendo yako.

amina umesema kweli ubarikiwe
 
Ukiwa nywaji bia, na Jehanum pia utazinywa sanaaa. Kama kwa mwezi hapa duniani unakunywa 40 basi baada ya kufa utakunywa 200. Fanya uchafu uwezavyo ili upate kulipwa kwa kadri ya matendo yako.

hayo uliyoandika ni kwa mujibu wa dini ipi!?
 
MASHAIRI YA YOUNG KILLER - DEAR GAMBE.

VERS 1;

Dear gambe umefanya maisha yangu ya yumbe,
MI nimpambe wako leo nimekutumia ujumbe,
MI ndugu yako nipe ukweli usini fumbe,
Uwepo wako karibu vp unafanya ni yumbe,
Kila muda kwene friji unajipoza,
MI domo zege nikisha kutumia natongoza,
Nalewa usiku kucha jua lina chomoza,
Nasindikiza na supu asuhi njema unaniongoza,
We ni nani unaiyendesha hi akili,
Nnikiwa na mawazo unanitoa stress nisifikili,
Ukiwa mezan chupa kadhaa sijiwezi,
Mpaka mtaani washa nipa jina jingine la mlevi,
Unafanya nafubaa mi mwenzako,
Hadi kazini naiba chapaa nije kwako,
Dear gambe mitaa ipe ukweli wako,
Nakila ugomvi wa baa kwanini chanzo ni chako..

VERS 2;

Unafanya ndoa nyingi zinavunjika,
Hasi chanya we na msosi nikichanganya na tapika,
Aukatai kila mteja anae kuarika,
Unafurahi na ubaridi wa maji una chilizika,
Likitokea tatizo we ndo kimbilio,
Nakutinga nakua muongeaji bila mpangilio,
Nasahau kinga tamaa ndo kimbilio,
We ni funda la ziada unaniumbua mi mwenzio,
Unarainisha koo kifikla unani bembeleza,
Unani kontro sijasoma naongea hadi kingereza,
Usha niweza nani aliye kutengeneza,
Na nini aliwaza nawe ni mbaya kwa wasio jiweza,
Sa najinyea nanilikunywa kwa furaha,
Najikojolea unani athiri na ninatoa cha paa,
Dear gambe mitaa ipe ukweli wako,
Nakila ugomvi wa baa kwanini chanzo ni chako..

VERS 3;

Dear gambe unanichanganya sana,
Unamajina mengi mpaka ya mbuga za wanyama,
Nashangaa,mengine yanatia kinyaa,
Mfano mzuri nigongo chimpumu hata cha ng"aa,
Kwenye ubongo umetawala kila secta,
Niukweri siwezi kua nawe bila pesa,
Watu wengine wana kula ada kisa wewe.
Unawafanya wanasahau ibada,
Na juzi juzi tu nimepata khabari,
Kuna mwana ulikua nae ameshapata ajaLI,
Dear gambe nikweli unanichosha,
Napenda kua nawe ila nyumbani mboga wanakosa,
Nawaza jinsi gani ntakuacha,
Mpaka wazalendo wa dini bahadhi kwako wame data,\
Hakuna utata poa sasa najikata,
Kapuku nikizipata ntakufata...mia
 
Bia ni kiboko kwa Jinsia yeyote asipitiwe na kiumbe mwingine wa jinsia tofauti lazima kitawaka
Sasa wewe mwenzangu TINGs sijui usingizi unakujaje wakati nahisi wa pembeni huna au unapendelea kilevi gani, kuna majani, (bhangi) Sembe, gahawa totos, taarabu na ili upate usingizi huwezi niambia eti ni Novel, magazeti na ya udaku au hapa JF
lazima kapo kaulevi fulani kanakoshtua ubongo ukanena lugha nyingi bila ya aibu
 
Last edited by a moderator:
We una bahati sana na usichezee hiyo bahati. Wote tumetoka hukohuko hiyo ndio nafasi yako ya rahisi kushinda zote kwa ajili ya kuacha pombe, shauri yako.

Kweli mkuu! Dawa ni kuacha tu! Leo siku nzima nmeshinda kwa bed hata kula shida! Kweli pombe sio chai!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…