Beware with this

ERoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
52,419
Reaction score
118,935
"Habari, Naitwa Rachel from Nexon International hapa dar, nipo kwenye kikao tunapitia cv tupate people to interview for program officer post, i like your cv na nitakusaidia upate hii kazi kwa sharti lifuatalo, mshahara ni 1.5million tshs ukilipwa mwezi wa kwanza utanipa sh.laki 3 for helping you, kama upo tayari do the following, by saa 11 jioni uwe umetuma scanned copy ya vyeti vyako to visionafrica@gmail.com na sh.elfu 40 by tigo pesa kwenye hii namba au m-pesa 0767208704 ili nimpe mtu wa interview anipe maswali ntakutumia by email. nikitoka kikaoni utapigiwa sim lini uje for interview"

Be very careful when receiving this msg, this is rubbish and conning.

Truly Tanzanian.
 
Hii Nexon nilitafuta hata sikuona inahusika na nini.Hakuna kazi hapo,kaa chonjo!
 
Hii Nexon nilitafuta hata sikuona inahusika na nini.Hakuna kazi hapo,kaa chonjo!

Baadhi ya waTanzania wanaishi maisha ya utapeli tu
 
kuna best yngu yamemkuta hayo arusha km wk 2 zilizopita aliapply kaz word vision jion yake wakamwambia haya haya jamaa akanicheki nkamwambia matapeli aachane nao......yaani hii nchi sasa muamini baba yko na mama yko tu.
 
heh!jamani kuna rafiki yangu wa karibu yalitaka kumkuta haya haya siku 2 au 3 zilizopita, hao jamaa ni mafundi balaa ilibaki kidogo wampige kama laki tano akastuka daah..wanasema akili kumkichwa
 
hii dunia simuamini mtu hata mimi mwenyewe sijiaminiamini, suspect everybody, trust nobody including you!!
 
Hii ni moja ya sababu kubwa nchi hii itaendelea kuwa maskini, hamna hata jambo moja linalofanyika ka haki, kuanzi ofisi kubwa za serikali mpaka raia aliye masikni kabisa...tusipobadilika tunaelekea pabaya sana
 
dah watu hawana utu kabisa, ilimtokea rafiki yangu hiyo kwenye kazi za exim bank, jamaa tapeli anaitwa john malondo kwenye mshahara anataka laki tatu, alafu anajifanya anafanya kazi hapo kumbe alishafukuzwa kazi kitambo kwa sababu ya utapeli wake. Kuweni makini.
 
kuna best yngu yamemkuta hayo arusha km wk 2 zilizopita aliapply kaz word vision jion yake wakamwambia haya haya jamaa akanicheki nkamwambia matapeli aachane nao......yaani hii nchi sasa muamini baba yko na mama yko tu.

saa nyingine hata hao baba na mama yako wanaweza kukutapeli pia...muamini God pekee yake hata wewe usijiamini
 
Huu uzi ufufuliwe watu walete shuhuda za utapeli, binafsi kuna jamaa alitapeliwa atapatiwa kazi kwenye shirika moja(NGO'S) akampa mchizi vyeti, baada ya miezi kama mitatu akiwa hana hili wala lile akapigiwa simu na mdada anaongea kingereza balaa, basi akumuuliza wewe ni fulani, uliomba kazi fulani shirika fulani, jamaa akawa so excited. Yule dada akamuuliza are you comfortable hapo ulipo tuanze interview kwa simu, then ukiqualify tutakuita ofisini kwa interview zaidi, jamaa akamwambia am very ready kuanza interview, this time akazima gari kabisa ili asitetereke kwenye kujibu maswali. Akapigwa maswalii wee kama 20-30' then yule dada akamwambia tutakujulisha kwa direct call or via email.
Ile wamaliza kuongea akamvutia wire yule mchizi aliedai kumuunganisha, huwezi kuamini jamaa akajifanya alishasahau kuhusu iyo issue, akadai mwana mimi nilipeleka Cv zako kama masihara kumbe imekua kwelii, imepita kama week, one of the cool weekend jamaa yangu akamvutia wire jamaa akamwambia njoo hapa element tulainishe koo.... Hahahahaaaa hii ndo ilikua kilio chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa akaibuka mida ya kama saa 10 jioni anagonga soft drinks, he never touched alcohol, ila rafiki yangu anatandika Jameson whisky balaa, story zikawa zimenoga kichizi, jamaa akaanza kuchombeza unajua salary yako kama degree holder itakua 2.5M,and above akaanza kumwonyesha rate za salary kwenye simu,rafiki yangu akapagawa kichizi akipiga mahesabu alipo anakinga 960k take home akazidi kupagawa, yaani akawa anawaza vitu lukuki vya kufanya akipata hiyo job.... Palepale akamchomekea unajua mjini kazi kujuana, mi naweza kukulink na mtu pale ambaye asilimia 200 akikurecomend unaajiriwa, Daaah jamaa akazidisha mchecheto tunafanyajefanyaje sasa kukutana nae, akatulizwa relax nimpange akiwa tayari nitakushtua.Rafiki yangu hakua na wasiwasi naye kabisa kwakua hakuonyesha dalili za tamaa....Wakamalizia gambe wakaagana, rafiki yangu akawa akilini mwake ana 40% kazi anaipata, so akamtia Jamaa 20k akamwambia hii utaweka mwarabu kwenye ndinga yako.
Kufika home anawaza amuhadithie mkewe au ampe surprise akipata kazi, jibu likaja surprise itakua mukide, si kwa wife tuu hata kwa washikaji zake hakuwaambia, akawa anasikilizia awasuprise mazee..ofisini kwake ndo aliwaona wachawi kabisa wanaweza wakamwaribia hahahahahaa.........kosa la pili......(DON'T HIDE A CLEAR/CLEAN DEAL TO YOUR partiner-wife/husband neither a close friends utajutaaaa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa hiyo jamaa alilizwa kiasi gani cha fedha sasa...?
 
mjini kuna watu wana akili za mbali
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee watu wanakuja na mbinu mpya kila siku

Sent From Galaxy S20 Ultra
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…