sijawahi kubet ila natrade forex zaidi kwenye stocks( 6 years in a row tangu nimemalize chuo mi ofisi yangu ni chumbani kwangu) kama leo asubuhi nimefungua positions za kubuy uber. Nikifungua position yoyote either a buy/sell huwa na analyse mda mwingine hata mwezi kwa small cap stocks na miezi miwili kwa large cap sasa sijui kama kwenye kubet huwa wanafanya hivyo. Alafu forex imegawanyika katika vipisi pisi vingi tu, kuna wanao trade currencies, indices, indexes, stocks na commoities. Naamini katika Forex kila mtu anakuwa na style yake unique ambayo huwa anaitumia ambayo ipo suitable kwake yeye, hayo mambo ya mentors na kununua signals tupilia mbali kabisa asilimia 90% ya mentors wabongo ni matapeli. Kama unataka kuzama kwenye forex ntakupa ushauri wa bure ufuatao.
1. Anza kutrade Demo account kwa atleast mieze minne, hii itakupa picha ya jinsi masoko yanavyoenda na kama kweli umeamua kuinvest mda wako wote kwenye hili then ndani ya mwaka ni lazima uwe umefanikiwa. Hakikisha hiyo demo account utakayo fungua balance yake ni ile ile utakayo deposit, sio unafungua demo account ya usd 1 mil then unakuja deposit 100$.
2. Soma, narudia tena soma. Knowledge is power. Kuna pdf kibao online fanya research yako, telegram kuna magroup mengi tu ya traders library unaweza pata vitabu vya bure huko ambavyo vitakusaidia mbeleni. Fuatilia habari sana tu kama huna tabia hiyo ndo uanze lipia dstv angalia Bloomberg masaa yote kuna insights za kutosha sana .
3. Wakati ukiwa unatrade hiyo demo account andika each and every single position utakayo fungua na kufunga, kuanzia mda uliofungua mpaka uliofunga pamoja pips ulizopata ama ulizopoteza na hii tabia usiache hata uje ufanikiwe vipi. Na ili ujue na uweze kufuatilia vizuri inabidi hizo notes zako zicover 24 hours kwa siku tano kwa mda wa miezi mitatu ambayo ni Q1 hii itakusaidia kujua ni mda upi ambao upo most volatile na mda gani masoko hayatembei. Pia hili litakusaidia kujua ni pairs zipi zina hela na pairs zipi ni kimeo na pair zipi zenye correlation pia itakupa mwanga mpana zaidi wa kutengeneza trading plan yako ambayo usijethubutu ukaenda against nayo ikija kukamilika, Plan your trade, Trade your plan always.
4. Patience na emotion elimination. Kwakuwa unaanza na demo hivi vitu hutavijua, ila siku ukifungua real account ukaweka pesa zako then ukafungua positions hii ndo utakuja kujua maana yake ni nini. You have to experience this on your own ili uweze kujicontrol. Naweza andika mpaka mwaka ujao ila hivi vitu viwili vipo damuni kwa kila binadamu na kuviacha huwezi ila tunachofanyaga ni kuji fine tune tu.
5. Tafuta strategy. Usinunue kwa mtu utauziwa utumbo uliooza (wakati naanza nilipigwa karibia 2000$ kununua strategies that never worked na robots zilizochoma account tu).
6. Forex si kwa watu wenye roho nyepesi, ila ukisha kamilisha hivyo vitu vyote na ukaona upo fresh fungua cent account deposit dola 4 nadhani ni kama buku 10 tu ambayo itakuwa kama cent 400 hii itakusaidia kukujenga kwenye point zangu za number 4.
Forex unaweza anza na 1$