Better being Single-Ndoa majanga tu

Better being Single-Ndoa majanga tu

Gracious

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
1,889
Reaction score
1,083
Wadau;

Ndoa ni ndoano.kwa maisha ya sasa ni vigumu sana kuwa na ndoa yenye furaha,ni bahati.Usanii umekuwa mwingi sana.Uongo ndo routine,sio kwa mke wala kwa mme.Kinachotofautiana ni uwezo wa watu kuhimili mikiki ya ndoa hizo.Lakini zote ni majanga tu.

Mfano.Mimi na mchumba wangu kwa wiki sasa namwona hayuko sawa ,nimetumia mbinu nyingi sana kujua ni nini shida,nimemuuliza taratibu kwa mapenzi ya hali ya juu.Lakini best ananiambia hana shida yuko sawa tu.Sometimes namsemesha hasikii narudia kama mara tatu alafu anashtuka kwamba namuuliza yeye.Yaani hayuko na mimi.Hasa tukiwa kwenye gari nadrive namwona kabisa hayupo na mimi kimawazo.Hii ishu imenikwaza na kunifikirisha sana,Kwamba kama huu ni Uchumba tu,Je ndoa itakuwaje,Si majanga tu.Mtu hayuko sawa na hasemi,sasa mi ntamfanyaje jamani,hebu nishaurini,naogopa mwenzenu
 
Bora kuwa kwenye ndoa..... kuzinguana majanga tu

Ukiwa Single utazinguana na nani? Haya mahusiano ya siku hizi shida tupu....Ndo maana wazungu wana watotom wa Laboratory.....Hizi pressure zinakera ati
 
i totally agree with you wake wanachakachua ndoa zao wanatutongozea wanaume zetu wengine mpaka wanataka kuwabaka
wanaume ndo kabisaaaa mume wa mtu mda wowote unambeba juu juu
aiseee walio kwenye wanavumilia mengi khaaaa
hawataki tu kusema.
Halafu ukiwakuta sasa mume wangu ananipenda khaa kumbe mjini hapa wapo wenzio watatu na wao wanamuita hivo hivo na anawatunza kama wewe anavyokujali na pengine zaidi.
Kama ikitokea siku humu jf watu waelezee matatizo ya ndoa zao au wenza wao wawe wakweli. teh teh teh
 
Yaani amu NI MATATIZO TU ATI.WATU WANAKUFA NAYO KAMA TAI KWENYE SHINGO ATI.Hivi kwani ni lazima kuoa au kuolewa?
 
Last edited by a moderator:
ndugu heri usioe....

Yaani kwa kuwa mchumba wako yuko mbali kimawazo ndo yamekua yote haya?

Hujui kuwa atakwambia kinachomsibu kwa wakati wake? Sio kila jambo linalomsibu mwenza wako akakwambia hapo hapo....sometimes anahitaji muda...

Sasa uvumilivu mdogo umekushinda uvumilivu mkubwa utauweza ndoani?

Umefanya uamuzi sahihi wa kjwa single...na mueleze mchumba wako .apema atafute ustaarabu wake
 
Mkuu usiogope hata kidogo kwa hawa ndg zetu, mama zetu, wake zetu, dada zetu nk hicho ni kitu unaweza kusema ni common kwao. Binafsi ukiniuliza huwa ni kitu gani kwa kweli sujui hata kidogo na kwa sasa sidhani kama nahitaji kujua huwa wanasumbuliwa na kitu gani. Ila ukweli inasumbua sana, inakera sana pindi hiyo hali inapotokea na mbaya zaidi majibu yao ni kama ulivyomnukuu huyo mchumba wako, kwamba hakuna tatizo ili hali wewe unaona utofauti.

Iliwahi kunitokea mara ya kwanza kwa mke wangu bila experience yoyote kwa takribani siku mbili ama tatu, ilinikera, ilinikwaza. Sasa siku moja katika maongezi na mama mmoja mtu mzima mwenye age ya around 52, ni staff mwezangu lakini kama yangu na pia ni mama mchungaji, sasa katika maongezi tukafikia kuzungumzia hiyo situation kwa wanawake, alinihoji kwa ufupi sana kuwa "hivi hiyo hali huwa inawakera sana" mwisho wa kunukuu. Kumbe basi nikajua hii kitu huwa ni common kwa wenzetu na kuna kipindi inatokea na ni ya mpito, usihofu mkuu.

Aidha pia niliwahi kuambiwa kuwa Japan hakuna mameneja ama viongozi wa ngazi ja juu wanawake kwa level za maamuzi labda huyu mwanamke huyo awe wa umri mkubwa maana, kwa umri ,mdogo ama wa kati inasemekana (sina hakika hapo, naomba nisihukumiwe na wanawake) ya kwamba kuna kipindi fulani wanapatwa kama na ukichaa fulani hivi na baadaye hurudi kwenye hali ya kawaida, sasa basi kwa kuwa wao wanataka positive output kwenye kazi zao hawataki kusikia hizo excuse na mambo kama hayo hivyo wanawekwa pembeni.

Mwisho kabisa, narudia usigope, kama una wito wa ndoa itika na Mungu atakuwa pamoja nanyi hizo ni changamoto ambazo ukiwa mwenyewe zitakuwa zaidi ya hapo.
 
Yaani amu NI MATATIZO TU ATI.WATU WANAKUFA NAYO KAMA TAI KWENYE SHINGO ATI.Hivi kwani ni lazima kuoa au kuolewa?
ona ndugu ila mpe mkeo principle na wewe ishike mwambie ''NISIKUFUMANIE USINIFUMANIE, USIFANYE NIKUHISI UNAMWANAUME MWINGINE NA MIMI SITOKUFANYA UNIHISI NINA MWANAMKE MWENGINE NAOMBA USINIPE STRESS NISIKUPE STRESS, NAJIHESHIMU NAOMBA JIHESHIMU PIA TUHESHIMIANE''
Kuchakachuana ni kawaida ila ukizingatia hayo wala hamtoumizana
 
Umefuatilia kwa muda gani, na yuko na hayo mawazo tele kwa muda gani

Asante Lyagwa kwa ushauri mzuri.....Ni tangu jumatatu ya wiki hii.Kiukweli sija mcheat wala kumtendea lolote baya ,ninamjali sana hadi mimi najikubalki kwamba najitoa kwake when she needs me....Niko msikivu sana kwake.....anachokitaka nampatia nikiweza....sasa mi sielewi mtu anabadilika tu ghafla bila sababu...nimekuwa nae kwa mwaka wa tatu sasa
 
Last edited by a moderator:
ona ndugu ila mpe mkeo principle na wewe ishike mwambie ''NISIKUFUMANIE USINIFUMANIE, USIFANYE NIKUHISI UNAMWANAUME MWINGINE NA MIMI SITOKUFANYA UNIHISI NINA MWANAMKE MWENGINE NAOMBA USINIPE STRESS NISIKUPE STRESS, NAJIHESHIMU NAOMBA JIHESHIMU PIA TUHESHIMIANE''
Kuchakachuana ni kawaida ila ukizingatia hayo wala hamtoumizana

Hahahah....umenichekesha sana amu, I love ur principle......Ila mimi sio kumfanya asihisi ila sitakuwa na king'amuzi cha nje kabisaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
ndugu heri usioe....

Yaani kwa kuwa mchumba wako yuko mbali kimawazo ndo yamekua yote haya?

Hujui kuwa atakwambia kinachomsibu kwa wakati wake? Sio kila jambo linalomsibu mwenza wako akakwambia hapo hapo....sometimes anahitaji muda...

Sasa uvumilivu mdogo umekushinda uvumilivu mkubwa utauweza ndoani?

Umefanya uamuzi sahihi wa kjwa single...na mueleze mchumba wako .apema atafute ustaarabu wake
BADILI TABIA,Kwangu mimi hii ni ishu kubwa sana.....it means alot....na inafikirisha sana...kama mimi ndo furaha yake...kivipi hawezi ku share hard moments kama anazo....It is almost a week now...ni mda mrefu huo mkuu.

Mkuu,Kama utanihakikishia kwamba hili ni jambo la kawaida tu na lipo kwa wanandoa.Basi ni bora nisioe manake ntateseka sana
 
Last edited by a moderator:
Hahahah....umenichekesha sana amu, I love ur principle......Ila mimi sio kumfanya asihisi ila sitakuwa na king'amuzi cha nje kabisaaaaaaa

ha ha ha uchumba raha sana ila wewe najua kwa sasa upo na vijimawazo mpe mda mwenzio ujue si kila saa unajisikia kuongea au kusema tatizo lako sometimes unashirikiana na ubongo wako tu.
Na saa nyingine ukimbembeleza mtu akuambie tatizo ndo unazidisha ujue.
Mpe mda atakuambia tu kinachomsibu.
Wala usimuhisi vibaya ndo maisha ya wawili yalivyo
 
Asante Lyagwa kwa ushauri mzuri.....Ni tangu jumatatu ya wiki hii.Kiukweli sija mcheat wala kumtendea lolote baya ,ninamjali sana hadi mimi najikubalki kwamba najitoa kwake when she needs me....Niko msikivu sana kwake.....anachokitaka nampatia nikiweza....sasa mi sielewi mtu anabadilika tu ghafla bila sababu...nimekuwa nae kwa mwaka wa tatu sasa

Ni mapema sana na huo muda ni mfupi sana kwa hiyo judgement uliyofikia na kuita ndoa ni majanga, kama hakuna tatizo zaidi tarajia kumuona mwenzako katika hali ya kawaida very soon, hawa watu wana vitu fulani common, usiogope.

Ni jambo jema mkiwa wawili kuliko mmoja na apataye mke apata kitu chema.
 
pole yako mbona mi nafurahia ndoa loh utamu wa ngoma ingia ucheze😛ray2:😛ray2:
 
tulia wewe, wenzako wanandoa wakiona hivyo wanajua 'kifuatacho i.t.v'...jikague kague kama huna kosa ulilomfanyia, huna siri uliyoificha(labda kaijua) hapo ujue kuna BONGE la mzinga wa hela unakuja.... Au la sivyo ni ule ustaarabu 'I don't feel the same way i used to feel about you, i need some time out'....kibuti cha kizungu hicho.
 
pole yako mbona mi nafurahia ndoa loh utamu wa ngoma ingia ucheze😛ray2:😛ray2:

Hongera Asnam ,Na wewe sometimes hua unakuwa na tabia kama ya huyu bibie wangu?
 
Last edited by a moderator:
tulia wewe, wenzako wanandoa wakiona hivyo wanajua 'kifuatacho i.t.v'...jikague kague kama huna kosa ulilomfanyia, huna siri uliyoificha(labda kaijua) hapo ujue kuna BONGE la mzinga wa hela unakuja.... Au la sivyo ni ule ustaarabu 'I don't feel the same way i used to feel about you, i need some time out'....kibuti cha kizungu hicho.

Sina kosa dhamira yangu iko safi...nadhani kati ya watu waaminifu duniani mimi ni mmoja wao
 
Back
Top Bottom