Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 847
well kama ufujaji wa pesa ni sawa na UFISADI then this fits the bill
BODI ya Biashara ya Nje (BET) imekumbwa na mtafaruku kiasi cha Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kumwagiza mwenyekiti wa bodi, kuitisha kikao ili kujadili matatizo hayo yanayomgusa moja kwa moja Mkurugenzi Mkuu.
Wizara hiyo imemwagiza mwenyekiti wa bodi kujadili mapungufu ya BET, ambayo yamekuwa yakiwasilishwa wizarani kwa njia ya barua za wafanyakazi zenye malalamiko lukuki.
Malalamiko ambayo bodi imeagizwa kuyajadili ni pamoja na madai ya uongozi mbovu unaodaiwa kufanywa na Mkurugenzi Mkuu wa BET, ubadhirifu na ufujaji wa fedha unaodaiwa kufanywa na mkurugenzi huyo na kuwa na safari nyingi zisizokuwa za lazima.
Maeneo mengine yenye malalamiko ni ununuzi wa magari chakavu, kinyume na kanuni na sheria za manunuzi na fedha, na utawala wa kuwagawa watumishi na utawala wa mabavu, unaodaiwa kufanywa na Mkurugenzi Mkuu Ramadhan Khalfan.
Wakati wa majadiliano yetu nilikueleza kuwa barua kadhaa zimepokewa na ofisi yangu zikidai kuwa kuna mapungufu Baada ya majadiliano ya kina na kabla ya Wizara kuchukua hatua yoyote ningependa uitishe Bodi yako, iweze kumwita Mkurugenzi Mkuu ili aweze kutoa majibu kwa yaliyoelezwa, inasema sehemu ya barua ya Katibu Mkuu, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuona nakala yake.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya BET, Profesa Hasa Mlawa, alipoulizwa na Raia Mwema Jumatatu wiki hii, alisema kwamba malalamiko hayo hayajadiliwa na bodi yake, bali imekuwa ikishughulikia mkakati wa kuliboresha shirika hilo.
http://www.raiamwema.co.tz/08/04/09/6.php