Nasikiliza..endelea
Unanisikiliza nini? Btw nshamaliza
Wapendwa leo niliandaa maandazi matamu balaa haya nlitumia hivi vipimo....jaribu na wewe uje uniambie kama hutashibia jikoni
Mahitaji
Unga kg 1
Sukari robo ila usijae
Samli 5 tablespoon + I tablespoon ya siagi (unaweka kwa sufuria inakua yamoto) siagi ni kwa ajili ya ladha nzur zaid
Hiliki 1teaspoon
Tui la nazi
Yai 1
Hamira 1 tablespoon
Mafuta ya kukaangia maandaz
Namna ya kutaarisha
Kwanza kabisa weka tui robo kikombe add sukar 1tablespoon na hamira (hiki ni hatua ya kuumua hamira na kuitizama kama bado ipo active ili usije haribu upishi wako kama itakua imeshapita mda) itafanya bubbles kwahiyo bado ipo active
Weka unga changanya na sukar na hiliki...changanya vizur
Mimina samli yamoto kiasi kwenye unga..changanya kwa mikono safi
Weka yai then tui
Kanda hadi iwe laini...
Subiria 30 minutes iumuke
Katakata maandfazi yako
Acha yaumuke
Weka karai mafuta yakipata moto kaanga hadi yawe brown..
Maandazi tayar kwa kuliwa.
asante farkhina sasa bado nakula mtori next week ntayaandaa haya..nilikuomba receipe ya half cake laini tamu ukanibania farkhina.mwenzio nikipika huwa hazilainiki na ninazipenda kweli..
Thanks for whetting my appetite. I haven't had them in a long time and it's about time now.
Mi huwa napenda kuyakata katikati halafu napaka red plum jam.
Ya hivyo naweza kumaliza hata kisadolini kizima!
Farkhina yaani mie bila kuona picha sijaridhikaaa....
Pls weka picha ili niigizie .
Hahaha hivi umeshamaliza? I ment nasoma maelezo yako not kusikiliza 🙊
Best umesahau kuweka hatua ya kuchanganya hamira. mdogo wangu Eiyer atapika bila kutia hamira hapo lol. na utukumbushe kuweka samli ya moto kabla hatujaweka hamira kusudi isife nguvu.
asante mamito, hadi likizo iishe mmh! maandazi na mie huwa nashibia jikoni, lol