Abu Haarith
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 314
- 165
Vipimo
Vikombe 3 vya unga
Kikombe 1 maziwa ya dafudafu (warm)
½ kikombe sukari
½ kikombe maziwa ya unga
Mayai 2
Kijiko 1 cha chai baking powder
½ kijiko cha hiliki ya unga
1/3 kikombe mafuta
Mchanganyiko wa hamira
2 vijiko vya kulia hamira
1 kijiko cha kulia unga
½ kikombe maji
1 kijiko cha chai sukari
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Weka mchanganyiko wa hamira katika bakuli dogo kisha koroga na acha uumuke kiasi dakika 5.
Kidokezo: Ukitaka hamira iumuke haraka: Washa microwave kiasi dakika 3 bila ya kitu ndani yake. Kisha weka mchanganyiko wa hamira ndani uache uumuke basi mara moja utaumuka.
Mchanganyiko Wa Maandazi
- Changanya vitu vyote katika bakuli la kukandia unga la umeme kisha tia mchanganyiko wa hamira.
- Washa mashine ikande unga kwa mpigo wa wastani (medium speed) kwa muda wa dakika 8 takrbian mpaka donge la unga liwe laini.
- Paka mafuta au unga mikononi kisha toa donge la unga ugawe madonge 9.
- Tandaza kila donge huku unanyunyizia unga ili usigande. Likisha tandazika likawa duara ya kiasi lisiwe nene, kata donge sehemu 4 za shape ya pembe tatu.
- Pakaza mafuta katika treya na nyunyizia unga kisha panga maandazi uwache nafasi yasije kugandana yatakapoumuka.
- Funika kwa karatasi ya plastiki au kitambaa kusikuweko na uwazi wa kuingia hewa. Acha yaumuke muda wa saa 1 au 1 ½ kutegemea hali ya hewa.
- Yachome (bake) katika moto wa wastani kwa dakika 10 takriban huku unaangaza mpaka yageuke rangi khafifu ya dhahabu.
- Epua yakiwa tayari panga katika sahani
Kupata maelezo ya mapishi mbali mbali bonyeza hapa Muislamu: Mapishi