SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,117
- 8,096
Ilikuwa July 1982 ambapo vijana watano marafiki wa damu waliokuwa wanasoma high school moja, John Wardlaw, John Dickson, Mark Rumer, Dallas Burney na John Molony walipopiga picha ya kumbukumbu ya pamoja Copco lake, California Marekani wakiwa na umri yapata miaka 19 hivi.
Bila kujua kwamba siku moja picha hiyo itakuja kuwa picha bora (official vacation photo of the five teens), achilia mbali kuja kuwa ndio utamaduni wao hapo baadaye kwani kila baada ya miaka 5, kwa miongo 3 sasa, marafiki hao wamekuwa wakikutana Capco lake na kupiga picha ya pamoja katika pozi lile lile.
Ukitazama vizuri katika picha hizo John Molony, anayefahamika katika group hilo kama Belves, anaonekana amebeba glass ya kahawa ambamo ndani mwake amemweka mende na kuamua kumfuga kama utamaduni wake.
Hiyo ndio imekuwa kama njia ya kudumisha urafiki wao, kwani achililia mbali kukutana kwao kila summer baada ya miaka 5, bali pia wamekuwa wakiwa pamoja katika shida na raha.
Je wewe unawaenzi vipi marafiki au company yako?