MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,239
- 50,420
Aliyekua mgombea urais kwa chama cha upinzani Uganda, amefunguliwa mashtaka ya uhaini, hii ni baada ya video inayomwonyesha akiapa kiapo cha urais ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii.
Wakili wake amedai kuwa serikali imegoma kuruhusu awakilishwe na yeyote kwenye kesi hii. Ni mara ya pili kwa kiongozi huyu kufunguliwa mashtaka ya uhaini, aliwahi kujikuta katika hali kama hii mwaka wa 2005.
Ni mpinzani sugu dhidi ya rais Museveni na amepitia makubwa kwa muda mrefu, ikiwemo kulazwa hospitalini baada ya kupigwa, amefungwa kwenye jela za serikali, amefungwa kwenye jela la nyumbani, amepigwa mabomu ya machozi n.k.
Adhabu ya uhaini inahusu hadi kunyongwa, japo Uganda haijamnyonga mfungwa yeyote kwa muda mrefu.
Rais Museveni ameapishwa kama rais wa awamu ya tano, itakayomwezesha kuwa kwenye madaraka kwa miaka 35
Uganda opposition leader charged with treason: lawyer