Benno Malisa awa jasiri, awageuka CCM na kuwatetea CHADEMA Arusha

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Baada ya kupigwa stop jana kufungua matawi hapa Arusha Kambi ya Edward Lowassa leo imefanikiwa kufanya ufunguzi wa matawi kwenye kata mbalimbali hapa mjini ARUSHA huku ikiwa chini ya ulinzi mkali wa kampuni binafsi ya ULINZI Interegency Security na FFU wakiwa kwenye gari PT 1844, lakini katika kuonyesha watu wa Arusha hawataki kusikia mdudu CCM kila kona walikokuwa wanapita walikuwa wakizomewa wakiambiwa mnaenda kuiba wapi na kuonyeshwa vidole viwili yaani V alama inayotumiwa na CHADEMA .

Kambi hii ya Lowassa wanajinadi watafanya mkutano pamoja na kwamba polisi wamezuia wasifanye mkutano kwa kisingizio cha Interejensia za polisi zinaonyesha kutatokea na uvunjifu wa amani. Mvutano wa ufunguzi wa matawi ulianza tangu jana baada ya katibu wa UVCCM wilaya ya Arusha (Ezekiel Mollel ) kukataa kata kata kuwaruhusu kufungua matawi kwa madai hana taarifa lakini baada ya kufatilia ukweli ni kwamba aliambiwa na Riziwani Kikwete ambae ndiyo aliyepiga simu polisi kuzuia mikutano ya kambi ya Lowasa hapa Arusha ambae yeye, Mary Chitanda na Ezekiel Mollel wako kambi ya Benard Membe…na waliko kambi ya Lowawana na wanaoongoza harakati za ufunguzi wa matawi ni :

  • Beno - kaimu mw/kiti UVCCM -Taifa
  • Catherine Magige -MB
  • Fred Lowasa
  • James Milia
  • Mwalusambo –UVCCM (Wilaya Arusha)..
Nawasilisha….
 
Mpambano huo wa ccm wenyewe kwa wenyewe ndiyo utakaendelea kuididimiza hawa magamba huku A town, endeleeni tu ningependekeza iongezeke tena na kambi ya Sita
 
Mpambano huo wa ccm wenyewe kwa wenyewe ndiyo utakaendelea kuididimiza hawa magamba huku A town, endeleeni tu ningependekeza iongezeke tena na kambi ya Sita
Mkuu hapa Arusha hawana mvuto wajaribu mikoa mingine siyo Arusha mjini.....
 
Huyu Lowasa anazidi kujizika kisiasa, ngoja tuone kama kweli T.B Joshua aliyemwombea ana uwezo kweli wa kumsafisha Lowasa kama nywele zake au vp!!!! Big up kwa vijana wa Arusha kwa kuwakataa hawa jamaa wanaotuharibia taifa letu!!
 
Mtifuano Huo hauna athari,,,,,wacha watifuane tu kwa tamaa na uchu wa kupigiwa ving'ora
 
Vita ya CCM wao kwa wao inaua kuliko vita ya upinzani na CCM.
 
  • Beno - kaimu mw/kiti UVCCM -Taifa
  • Catherine Magige -MB
  • Fred Lowasa
  • James Milia
  • Mwalusambo –UVCCM (Wilaya Arusha)..
hapo kwenye red,...kwani yuko kambi tofauti na swahiba wake R1?
 
Huyu Lowasa anazidi kujizika kisiasa, ngoja tuone kama kweli T.B Joshua aliyemwombea ana uwezo kweli wa kumsafisha Lowasa kama nywele zake au vp!!!! Big up kwa vijana wa Arusha kwa kuwakataa hawa jamaa wanaotuharibia taifa letu!!
Afya iliteteleka mpaka hata kutembea ilikuwa shida ikabidi akimbilie kwa Joshua...
 
  • Beno - kaimu mw/kiti UVCCM -Taifa
  • Catherine Magige -MB
  • Fred Lowasa
  • James Milia
  • Mwalusambo –UVCCM (Wilaya Arusha)..
hapo kwenye red,...kwani yuko kambi tofauti na swahiba wake R1?

Ndiyo mkuu,, haka kajamaa Beno malisa kalihongwa na kambi hii pesa ya kutakata kamesaliti rafiki yake wa damu aliyembeba sana. Jamaa hana faadhila kabisa huyu beno ni ndumilakuwili
 
Ukianza dhambi huwezi kuiacha kamwe, na wizi ukianza nayo huwezi kuiacha tena....! hadi nyumbani kwako utaanza kuibia....! Ona sasa, baada ya ufuatiliaji kuwekwa kwenye wizi wa rasimali za umma, wameanza kupigania rasimali za Chama...! Hivi wanadhani hicho chama ni cha kwao tu?
 
Ndiyo mkuu,, haka kajamaa Beno malisa kalihongwa na kambi hii pesa ya kutakata kamesaliti rafiki yake wa damu aliyembeba sana. Jamaa hana faadhila kabisa huyu beno ni ndumilakuwili
.....mkuu hata siamini Benno huyu huyu..ninayemjua mie..maana hawa jamaa walikuwa mabest sana chuo,na hata hiyo nafasi yake UVCCM..R1 alihangaika sana....kweli PESA mbaya...
 
nimepishana na msafara wa bernadi membe hapa kwa ngulelo na mabasi mawili yamewasha taa na mwendo mkali sijui wanaenda moshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…