LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 8,974
- 14,490
My take: Naona wakati wa kuanza kuishi kama shetani umefika, pia kuisoma namba
============
Michango mingine...
============
Ukifanya muamala wowote wa kutoa pesa benki kuna makato mfano kwa CRDB ni 2,200. Maana ya hii kodi ni kuwa sasa utakatwa TZS 2,596. Vile vile ukifanya malipo kwa njia ya TISS makato yalikuwa ni TZS 10,000; kwa sasa utakatwa TZS 11,800.
TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA NCHI YETU
Mwalimu usiogope sana, sio kweli kwamba kila unapochomeka kadi kwenye ATM basi utakatwa 18%,yani ukitoa 400,000 ukatwe 18% ambayo ni sh 72,000? Haipo hivyo
Ukweli ni kwamba, kutakuwa na VAT ya 18% kwenye tozo ya kila huduma, Mfano km hapo awali tozo ya huduma ya kutoa sh 400,000 ilikuwa ni sh 3,000 basi kuanzia kesho kutakuwa na ongezeko la 18% kwenye hiyo sh 3000
Hivyo, 18/100×3000=540
Kwa msingi huo, muamala ambao ulikuwa unakatwa sh 3000 hapo awali, sasa hivi utakuwa umeongezeka kwa 18% ambayo ni 540,
Kwa hiyo, badala ya kukatwa 3,000 sasa hivi utakatwa sh 3,540 kila unapoenda kutoa sh 400,000
Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa lako!
Makato ni 10% + 18% (VAT)
KWA KIREFU
(Endelea Kusoma)
Kuhusu makato kwenye kutuma na kupokea pesa (kutoa kwa wakala)
Kwenye hotuba ya waziri wa fedha na mipango alisema hivi:
" (iv) kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee. Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hvyo kuwa nje ya wigo wa kodi."
***MAELEZO**
Ipo hivi, kwa hali ya sasa unapomtumia pesa mtu, lets say 20,000 unakatwa kama Sh 500/-.
Serikali inachukua kodi kwenye hiyo mia tano tu.
Wakati huo huo ukitumiwa pesa, lets say 20,000. Ukienda kutoa kwa wakala wanakata sh 1,200.
Kwenye hiyo 1,200 serikali ilikuwa haipati kitu.
*****
Na ndio maana waziri akasema hivi:
Na nukuu:
" Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hvyo kuwa nje ya wigo wa kodi."
KWA MUJIBU WA BAJETI HII.(2016/17)
Kwa utaratibu wa sasa, serikali itachukua kodi ya 10% ya makato wakati unatuma pesa na kupokea pesa pamoja na VAT (18%)
Ngoja nikupe mfano.
Umetuma 20,000. Afu makato yakawa 500.
Serikali itachukua kodi asilimia 10 ya hiyo 500, yaan itachukua sh 50/-
Na pia itachukua VAT ambayo ni 18% ya hiyo 500, ambayo ni sawa na Sh 90/-
Kwahiyo kwenye kutuma pesa, una katwa 500, kwenye hiyo 500, serikali inachukua (50+90=140)
Unapopokea pesa, ukaenda kutoa kwa wakala, lets say umetoa 20,000. Unakatwa 1,200.
Serikali itachukua asilimia 10 ya hiyo 1,200. Yaani sh 120/-
Pia VAT ambayo ni 18% ya 1200, ambayo ni sh 216/-
Kwahiyo, makato yanakuwa (216+120 =330)
Huo ndo ufafanuzi sahihi.
#Elimisha na wenzako
========
Updates;
========
Serikali/TRA yazitaka Benki kutopandisha viwango vya tozo/ VAT katika miamala yake