beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Benki za Mwanga Community, Hakika Microfinance na EFC Tanzania Microfinance zimeungana na kuwa benki moja ijulikanayo kama Mwanga Hakika Microfinance Bank Ltd
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ridhuan Mringo, alisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja zenye kuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.
“Tunaamini kwamba huu ni muda wa kuimarisha sekta ya kibenki na hii imejidhihirisha kwa baadhi ya benki ambazo ziliamua kuungana na kuunda benki moja imara. Tumeamua kuungana ili kutengeneza benki kubwa na imara ambayo itasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara yetu,” alisema Mringo.
Aliongeza kuwa kupitia benki hiyo, wateja watapata huduma zilizoboreshwa zaidi na bidhaa zenye ubunifu katika mikopo na uhifadhi wa fedha ambazo zitakuwa nafuu na za haraka.
“Kuanzia sasa mahitaji ya kila siku ya kibenki ya wateja wetu yatatimizwa na benki hii mpya. Tunatarajia kukua kwa makusanyo ya akaunti za wateja kwa sababu benki hii itakuwa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedha,” alisema.
Kupitia muungano huo, benki mpya itakuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji huduma ikiwa na matawi saba ambayo yatakuhudumia wateja 105,000 nchi nzima.
Dk. Kibesse alipongeza hatua iliyochukuliwa na benki hizo na kwamba itasaidia katika uimarishaji wa sekta ya kibenki kwa kuhakikisha watu ambao hawajafikiwa na huduma wanapata nafasi hiyo.
Pia alisema itasaidia katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuwa benki hiyo itakuwa na wigo mpana wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati jambo litakalochangia kuleta ujumuishwaji wa uchumi.