Benki za Mwanga Community, Hakika Microfinance na EFC Tanzania Microfinance zaungana

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Benki za Mwanga Community, Hakika Microfinance na EFC Tanzania Microfinance zimeungana na kuwa benki moja ijulikanayo kama Mwanga Hakika Microfinance Bank Ltd

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ridhuan Mringo, alisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja zenye kuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.

“Tunaamini kwamba huu ni muda wa kuimarisha sekta ya kibenki na hii imejidhihirisha kwa baadhi ya benki ambazo ziliamua kuungana na kuunda benki moja imara. Tumeamua kuungana ili kutengeneza benki kubwa na imara ambayo itasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara yetu,” alisema Mringo.

Aliongeza kuwa kupitia benki hiyo, wateja watapata huduma zilizoboreshwa zaidi na bidhaa zenye ubunifu katika mikopo na uhifadhi wa fedha ambazo zitakuwa nafuu na za haraka.

“Kuanzia sasa mahitaji ya kila siku ya kibenki ya wateja wetu yatatimizwa na benki hii mpya. Tunatarajia kukua kwa makusanyo ya akaunti za wateja kwa sababu benki hii itakuwa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedha,” alisema.

Kupitia muungano huo, benki mpya itakuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji huduma ikiwa na matawi saba ambayo yatakuhudumia wateja 105,000 nchi nzima.

Dk. Kibesse alipongeza hatua iliyochukuliwa na benki hizo na kwamba itasaidia katika uimarishaji wa sekta ya kibenki kwa kuhakikisha watu ambao hawajafikiwa na huduma wanapata nafasi hiyo.

Pia alisema itasaidia katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuwa benki hiyo itakuwa na wigo mpana wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati jambo litakalochangia kuleta ujumuishwaji wa uchumi.
 
Yaani kipind cha mjomba magu taasisi za kifedha zipo hoi bin taaban.
 
HV kama hamjui Jambo si mnauliza...b3nki zimeungana kuwa kubwa na kufikia watu wengi zaidi na kuongeza mtaji... nyie mnasema zinaenda kufa..dah
 
HV kama hamjui Jambo si mnauliza...b3nki zimeungana kuwa kubwa na kufikia watu wengi zaidi na kuongeza mtaji... nyie mnasema zinaenda kufa..dah
Usikubali kutafuniwa, tafakari maandishi na dhumuni au mantiki. Kuungana kwa hizo benki ndogo 3 ndio kuepuka anguko.
 
Na bado, itafikia hatua benki zote zitaungana ndio wote tutaondoa ukimya.
 
Daah! Nilikuwaga banker wa Mwanga Bank two years ago pande za Mwanga township pale, maisha yanaenda kasi sana....!!
 
Sidhani kama yupo sababu baada ya MD kuwa muhindi wengi walipigwa chini,
Mimi nilikuwa HQ pale Mwanga, yeye alikuwa branch ya wapi mkuu kati ya hizi hedaru,same au moshi?
 
Kwa hiyo kuna kundi la watu linaenda kuwa jobless.....vip kwa FINCA nao wana hali gani??????

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

For almost 4yrs FINCA Tanzania inajiendesha kwa hasara. Ilibidi kuondoa ile top management karibu yote kuanzia CEO, CFO, CCO, HRM na Head of Risk Dept. Pia walipunguza staff ili kupunguza matumizi ya kampuni.

Bado hawajarudi kwenye reli ila nadhani kinachowabeba ni kwamba FINCA is International bank so nadhani wakipata hasara wanaongezewa mtaji kutoka makao makuu yao huko USA.
 
Maanake nasikia n shida uko.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ouky....kipind hich watu tuliokuwa taasisi za fedha tunapitia ubatizo wa moto....redundancy za kufa mtu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Kabisa Mimi nilihisi hii hali two years ago nikaona hapa bankers we are going to suffocate nikaanzisha biashara mapema,sababu hata wakati nipo Mwanga hali ilikuwa tete kinoma, mpaka tukapata notice toka BoT kuwa wanatuangalia kwa karibu,ila actual kinachoua taasisi za fedha ni NPL
 
For almost 4yrs FINCA Tanzania inajiendesha kwa hasara. Ilibidi kuondoa ile top management karibu yote kuanzia CEO, CFO, CCO, HRM na Head of Risk Dept. Pia walipunguza staff ili kupunguza matumizi ya kampuni.

Bado hawajarudi kwenye reli ila nadhani kinachowabeba ni kwamba FINCA is International bank so nadhani wakipata hasara wanaongezewa mtaji kutoka makao makuu yao huko USA.
believe me or not finca imeungana na Mwanga bank na hao hakika bank wanaenda kufunga bank yao, sababu wote walikuwa wana suffer loss sasa wote wako hoi nani wa kumuinua mwenzie, ni swala la muda tu
 
Back
Top Bottom