Benki ya Kilimo yajizatiti kusaidia upatikanaji wa Masoko nchini

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
IMG_1562.JPG

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, yenye Mada Kuu ya Warsha hiyo, “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima umekuwa ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Bw. Samkyi amesema kuwa ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo Serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.

“Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Bw. Samkyi.

Kwa mujibu wa Bw. Samkyi, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani, ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.

“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamban hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” aliongeza.

Mkurugenzi Samkyi, ameongeza kuwa Benki imejipanga kutoa mikopo ya ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi pamoja na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao

Pia, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo ambapo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji, ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko.

Akizungumzia aina ya mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal amesema kuwa Benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupi (Short term loans), mikopo hii ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili (au miezi 24), Mikopo ya muda wa kati (Medium term loan), mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na Mikopo ya muda mrefu, mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uwekezaji mkubwa kwenye kilimo na ambazo marejesho yake yatafanyika katika kipindi cha miezi 60 hadi 180 (yaani kati ya miaka 5 hadi 15).

Bw. Pascal ameongeza kuwa riba itozwayo kwa upande wa Mikopo ya muda mfupi (Short term loans) ni riba ya asilimia saba (7%) mpaka (8%) kwa mwaka. Ambapo mikopo hii Hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Kwa mfano, kugharamia shughuli za kilimo zinazofanywa kabla ya mazao kuvunwa, na mara baada ya kuvunwa, ununuzi wa mazao, ununuzi wa zana na mashine za kilimo na mahitaji mengine ya kifedha katika mnyororo wa thamani.

Ameongeza kuwa mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na hutozwa riba ya asilimia tisa (9%) mpaka (10%) kwa mwaka. Na mikopo hii hutolewa ili kufanikisha mahitaji maalumu, mathalani: kupanua mashamba, kuzalisha aina mpya za mbegu, mifugo, na samaki na kuongeza kiwango cha rasilimali au uwekezaji, kuboresha miundombinu, pamoja na kuziba pengo la mahitaji mengine ya muda wa kati kwenye mnyororo wa thamani.

Na kwa upande wa Mikopo ya muda mrefu hutozwa riba ya asilimia kumi na moja (11%) mpaka (12%). Mikopo hii hutolewa kugharamia mahitaji ya muda mrefu, mathalani: gharama za kupata rasilimali, kujenga miundombinu mikubwa ya kilimo, kupanua mashamba makubwa na ya kati, pamoja na shughuli nyingine za kilimo zinazohitaji mikopo ya muda mrefu. Mikopo ya muda mrefu inalenga kufanikisha uwekezaji kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na mahitaji mengine ya muda mrefu.

“Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu katika sekta ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani, kwa mfano: skimu/mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu ya kilimo,” aliongeza Bw. Pascal.

TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
 
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia upatikanaji wa masoko ili kuongeza mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini.

Dhamira hiyo inalenga kufanya mabadiliko kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam, Thomas Samkyi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, amesema kuwa kukosekana kwa masoko ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Kwenye warsha hiyo yenye mada kuu isemayo: ‘Wazalishaji Tuanze na Soko,’ Samkyi amesema serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo.

Sababu kuu ni kusaidia kukabiliana na upungufu huo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo na hatimaye kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.

“Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo.

“Mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini,” amesema Samkyi.

Kwa mujibu wa Samkyi, TADB inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi, viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi.
Pia ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.

“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shambani hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba.

“Kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” amesema.

Samkyi ameongeza kuwa benki imejipanga kutoa mikopo ya ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi.
Pia mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao.

Amesema, benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo.

“Inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji, ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko,” amesema.

Robert Pascal, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo amesema kuwa benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni mikopo ya muda mfupi (miezi 24), mikopo ya muda wa kati (miaka miwili hadi mitano) na mikopo ya muda mrefu(miaka mitano hadi 15).

“Riba itozwayo kwa upande wa mikopo ya muda mfupi ni asilimia saba 7 mpaka 8 kwa mwaka. Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani,” amesema.

Source: Mwanahalisi Online
 
Nyie oneni tu hili bandiko hapa mkasifia,hawa jamaa wanamasharti magumu sana,hawana tofauti na taasis zingine za kifedha zinazowanyanyasa wananchi,
Eti mpaka muwe group na muwetna expirience zaidi ya 3years,lakini pia ardhi mnayolima lazima iwe mali yenu pia muimiliki kwa hati ya serikali.
 
DUUUUH TENA KO BINAFSI HAWATOI
 
View attachment 333596
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, yenye Mada Kuu ya Warsha hiyo, “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima umekuwa ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Bw. Samkyi amesema kuwa ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo Serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.

“Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Bw. Samkyi.

Kwa mujibu wa Bw. Samkyi, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani, ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.

“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamban hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” aliongeza.

Mkurugenzi Samkyi, ameongeza kuwa Benki imejipanga kutoa mikopo ya ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi pamoja na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao

Pia, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo ambapo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji, ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko.

Akizungumzia aina ya mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal amesema kuwa Benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupi (Short term loans), mikopo hii ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili (au miezi 24), Mikopo ya muda wa kati (Medium term loan), mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na Mikopo ya muda mrefu, mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uwekezaji mkubwa kwenye kilimo na ambazo marejesho yake yatafanyika katika kipindi cha miezi 60 hadi 180 (yaani kati ya miaka 5 hadi 15).

Bw. Pascal ameongeza kuwa riba itozwayo kwa upande wa Mikopo ya muda mfupi (Short term loans) ni riba ya asilimia saba (7%) mpaka (8%) kwa mwaka. Ambapo mikopo hii Hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Kwa mfano, kugharamia shughuli za kilimo zinazofanywa kabla ya mazao kuvunwa, na mara baada ya kuvunwa, ununuzi wa mazao, ununuzi wa zana na mashine za kilimo na mahitaji mengine ya kifedha katika mnyororo wa thamani.

Ameongeza kuwa mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na hutozwa riba ya asilimia tisa (9%) mpaka (10%) kwa mwaka. Na mikopo hii hutolewa ili kufanikisha mahitaji maalumu, mathalani: kupanua mashamba, kuzalisha aina mpya za mbegu, mifugo, na samaki na kuongeza kiwango cha rasilimali au uwekezaji, kuboresha miundombinu, pamoja na kuziba pengo la mahitaji mengine ya muda wa kati kwenye mnyororo wa thamani.

Na kwa upande wa Mikopo ya muda mrefu hutozwa riba ya asilimia kumi na moja (11%) mpaka (12%). Mikopo hii hutolewa kugharamia mahitaji ya muda mrefu, mathalani: gharama za kupata rasilimali, kujenga miundombinu mikubwa ya kilimo, kupanua mashamba makubwa na ya kati, pamoja na shughuli nyingine za kilimo zinazohitaji mikopo ya muda mrefu. Mikopo ya muda mrefu inalenga kufanikisha uwekezaji kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na mahitaji mengine ya muda mrefu.

“Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu katika sekta ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani, kwa mfano: skimu/mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu ya kilimo,” aliongeza Bw. Pascal.

TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
Mikoani wapo? Mfano mwaza wako wapi?
 
Nyie oneni tu hili bandiko hapa mkasifia,hawa jamaa wanamasharti magumu sana,hawana tofauti na taasis zingine za kifedha zinazowanyanyasa wananchi,
Eti mpaka muwe group na muwetna expirience zaidi ya 3years,lakini pia ardhi mnayolima lazima iwe mali yenu pia muimiliki kwa hati ya serikali.
Mkuu unachosema ni kweli kabisa, mimi binafsi niliwatembelea kuangalia uwezekano wa kupata mkopo maelezo niliyopata ya jinsi ya kupata mkopo na vipaumbele vyao yalinikatisha tamaa kabisa, masharti na vigezo ni magumu na si rafiki na kama vile hawana nia ya kusaidia wakulima wa kawaida lakini ukisikia matangazo yao unaweza fikiri hiyo ni fursa. Kwa mwenendo huu wakulima wa Tanzania wataendelea kuwa masikini
 
Naweza kusema kwenye kilimo bado kabisa hajapatikana mzalendo mwenye nia ya dhati ya kuinua mkulima mdogo.
 
Hayo masharti ndio yanawafanya vijana wanashindwa kabisa kujiajiri
 
ni mikopo mizuri sana mm pia mama yangu ni mnufaika wa hii mikopo

Huyo mama yako alipata peke yake au kwenye kikundi? Comments za wadau humu zinaonesha masharti ya mikopo ni magumu sana, ni kama vile hakuna tofauti na benki zingine kitu ambacho kama ni kweli ni nonsense. Sioni sababu ya kuanzishwa kwake kama haina tofauti na benki zingine zilizopo, imekuja kufanya nini sasa kuongeza idadi ya benki?
 
Zote hizo ni majipu tuu, hakuna Benki yoyote inayoweza kukopesha mkulima wa kawaida bila masharti magumu
 
Mkuu na hitaji kufanya kilimo cha mboga mboga naweza wapata wapi hapa dar je kwa waliowatembelea mashart yako coz last week nilikuwa benk ×nilipewa mashart mpaka kweli nikaona hpa uwezi chomoka hata kwa dawa Nina thamana yangu lakini niliambiwa et kama nahitaji walau hizo mil80niwe na uwezo walau wakupitisha 10mil kwa mwaka imagine mm napata wap hizo pesa wakati ndo nataka nianze na dhamana yangu ya shamba inazidi hizo pesa nilizoomba kwahyo kiukwel mabeki ayako tiyali kuwasaidia Vijana kwahyo style tutaendelea kulia kila siku
 
Nimeshaenda kuwatembelea hawa jamaa.

Kwa masharti walioyaweka, vijana walie tu.

Hakuna cha kuwa mkombozi wa wakulima.

Mkuu Bavaria, vp khs dhamana shamba likiwa na hati wanaikubali kama dhamana? Ktk masharti yao, kipi ni kigumu zaidi?
 
Nenda kawaone utajua zaidi. Sahivi ntakudanganya. Na hata maswali utawauliza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom