Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Benki ya Exim imetangaza msamaha wa zaidi ya Sh bilioni 160 wa likizo ya malipo ya mikopo kwa wateja wake wakubwa, wa kati na wadogo waliopo katika sekta zilizoathirika zaidi kiuchumi kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na benki hiyo katika kuwasaidia kifedha wateja wake waliopo kwenye sekta ambazo zimeathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu, msamaha huo wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 160 umeanza Juni mwaka huu.
Msamaha huo unahusisha likizo ya malipo ya mikopo kwa wateja na nyongeza ya muda wa urejeshaji wa mikopo ili kusaidia wateja wa benki hiyo katika sekta mbalimbali kutokana na athari za janga hilo kwenye biashara zao.
“Benki inaelewa mahitaji ya wateja wetu wakati huu na tunafanya yote yanayowezekana kuwasaidia ili waweze kuvuka salama katika kipindi hiki kigumu. Jitihada hizi haziishii tu kwenye misamaha hii tunayoitoa bali pia kupitia huduma za ushauri kuhusu mikakati ya biashara ili kuhakikisha kwamba biashara za wateja wetu zinadumu na zinafanyika kwa mafanikio zaidi,” alisema Matundu.
Kwa mujibu wa Matundu, msamaha huo unazingatia vigezo mbalimbali kwa kila mteja kwa kuwa athari za Covid-19 hazikuwa sawa katika sekta zote.
“Tunafarijika kwa kuwa tayari wateja waliopo kwenye sekta zilizoathiriwa zaidi wameshaanza kusaidiwa. Mazungumzo na wateja wengine bado yanaendelea ili kutambua hatua mbali mbali zinazofaa kulingana na aina ya biashara,” alisema mtendaji huyo wa Exim.
Aliongeza: “Siku zote Benki ya Exim tunaamini katika kufanya kazi kwa bidii leo kwa ajili ya kesho bora kwa wateja wetu, biashara zao na jamii kwa jumla, ni kwa mtazamo huo tumepitisha hatua kama hii katika wakati huu mgumu. Tunaendelea kujitolea kushughulikia mambo haya na kupata suluhisho sambamba na mamlaka pamoja na serikali katika kuhakikisha uchumi wetu unaendelea kuwa thabiti wakati wa nyakati hizi ngumu.”
Tangu ugonjwa huo uingie nchini sekta zilizoonekana kuathirika zaidi ni utalii, hoteli, wafanyabiashara hasa wanaochukua bidhaa China na mashirika ya ndege.
HabariLeo