Benki ya Dunia yaitaka serikali ipunguze posho, marurupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki ya Dunia yaitaka serikali ipunguze posho, marurupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 20, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Nora Damian
  Mwananchi
  20/2/2010

  BENKI ya Dunia (WB) imeitaka serikali ihakikishe kuwa inaacha matumizi mabaya fedha za maendelelo, kwa kupunguza posho na marupurupu mbalimbali kwa watumishi wake, ili kuimarisha sekta nyingine.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa mapitio ya matumizi ya umma, Mchumi wa benki hiyo, Emmanuel Mungunasi alisema pesa nyingi zimekuwa zikielekezwa kwenye posho na marupurupu, huku sekta muhimu kama za barabara zikikosa pesa za kutosha.

  Alisema kati ya mwaka wa 2008/09 serikali ilitumia Sh523 bilioni kama posho na marupurupu mbalimbali hasa katika sekta zinazohusiana na Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini (Mkukuta).

  Alisema posho nyingi zimeelekezwa kwenye wizara mbalimbali, Bunge, Hazina na Mahakama huku pesa hizo zikitolewa kwa kushiriki kwenye mkutano au kuandaa mradi fulani.

  Alisema suala la marupurupu kuongezeka kwa kasi si nzuri, kwani linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya nchi husika na hivyo wananchi wake kuzidi kuwa maskini.

  "Fedha nyingi zinakwenda kwenye allowance (posho) tujaribu kujibana ili tuweze kupata maendeleo," alisema Mungunasi na kuongeza:

  Nchi zenye mifumo ya fedha iliyoendelea vizuri hukua haraka kuliko zenye mifumo duni ya aina hiyo.

  Mchumi huyo alisema Benki ya Dunia imekuwa ikifanya tathmini kila mwaka kuhusu mapato na matumizi ya serikali ili kuweza kujua kama fedha zao na zinazotolewa na wafadhili wengine zinatumika ipasavyo.

  Hata hivyo, alisema kwa kiasi kikubwa serikali imekuwa ikijitahidi kwa kuhakikisha pesa zilizopangwa zinaenda vizuri hasa katika sekta za elimu, afya na kilimo.

  Mchumi huyo aliitaka serikali kuongeza bajeti hasa katika kuimarisha miundombinu kama ya barabara, reli na bandari kwa sababu sekta ya usafirishaji inachangia kukua haraka kwa uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo.

  Benki hiyo pia imeishauri serikali kuimarisha uwezo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kubuni na kutumia sera endelevu ili kuongeza ukusanyaji wa mapato bila kukwaza shughuli za sekta binafsi.

  Katika hatua nyingine, benki hiyo imesema inatarajia kutoa Sh1,000 bilioni katika bajeti ya mwaka 2010/11 zitakazoelekezwa katika sekta za barabara, elimu, afya na maji.

  Kwa mujibu wa Mchumi huyo, mdororo wa uchumi uliozikumba nchi nyingi umesababisha kuongezeka kwa msaada huo kutoka Sh800 bilioni katika bajeti iliyopita hadi Sh1,000 bilioni.

  Mara kwa mara nchi wahisani ambao huchangia bajeti ya nchi wamekuwa wakitoa malalamiko kuhusu matumizi mabovu ya fedha hizo na wakati mwengine hufikia hatua ya kutishia kutochangia bajeti hizo iwapo serikali itashindwa kudhibiti matumizi yake.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wanampigia mbuzi guitar?!! There is a lot more the WB can do, if they are really serious and mean/stand by their statements. But of course...they like and 'fund' mafisadis to keep Africa undeveloped...in order for the western countries to remain on top!!!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,120
  Likes Received: 27,077
  Trophy Points: 280
  wanajipenda mno.
  kila kitu kinapita.
   
 4. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uwii, wouldn't waste my breath if I were them. All their words are falling on deaf ears!
  Labda na wao wapunguze funding kwa serikali ndio watasikika
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana kabisa na wewe. Hawa nchi za wafadhili na mashirika yao (IMF na WB) mwaka jana walipiga sana kelele na kutishia kutotoa fungu lao katika bajeti ya Tanzania kutokana matumizi mabovu na wizi mkubwa unaofanywa wa pesa hizo toka nchi za Wafadhili.

  Imefika wakati sasa wa hawa kuacha kutoa vitisho vyao na kusimamisha kabisa kutoa pesa hizo mpaka watapoona Serikali inapambana na wahusika wote wa ufisadi na pia kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi makubwa ambayo hayaleti maendeleo yoyote kwa Watanzania.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Kuna kiongozi mmoja mzito wa serikali ya sasa aliwahi kuniambia "...kijana hizi safari safari ndio EPA yetu sisi tusio marafiki wa Rais....dawa ni kusafiri tu Rais anasafiri na sisi tunasafiri tu..tunakusanya marupupu" sasa naona hata wakubwa wa dunia wameshitukia, hapo wamegusa pabaya maana umaarufu wa uongozi wa kisiasa ulianza under Mkapa ndio kwa mara ya kwanza marupu rupu ya ajabu yalipoanza kwenye siasa, ninakumbuka under Mwinyi ilikuwa kichekesho sana mambo ya kugombea nafasi za siasa.

  - Wallahi hapo World Bank wamegusa pabaya sana, subiri uwasikie watakavyolia na maneno mengi ya ujanja ya kwamba Tanzania ni nchi huru haiwezi kuamuliwa mambo yake na Benki ya Marekani, watch! Walipouziana nyumba zetu za serikali walsiema wameambiwa na hiyo hiyo benki ya dunia sasa tizama watakavyobadilika hapa!

  - I do not care what hapo wamegusa pabaya sana, wewe subiri sasa hivi Membe atawaita mabalozi wa nje waache kuingilia mambo ya bongo, watch my words!

  Respect


  FMEs!
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,421
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  Asante babu ila kwa hawa jamaa zetu,......kazi ipo, hawawezi kusikiliza ukizingatia wameingia ili wavune!
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,052
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe unatarajia nini wakati mshahara wenyewe Serikalini ni mkia wa mbuzi? Haidhuru mshahara ungekuwa mdogo lakini social services zikawa nafuu, leo mambo yamekuwa tofauti kabisa. Kila kitu kulipia hospitali, elimu na kadhalika lakini hako kamshahara mhhhhhh!

  Sasa munatushauri vipi wajameni? Visafari ndio vinapunguza ile gap pale. Wangetulipa mishahara mikubwa kama ya hiyo Benki hapo tungeweza kuwasikia vyema kabisa.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Binti Mkongwe, ukiangalia majirani zetu kama Kenya, Uganda, Rwanda Viongozi wao na hata Mawaziri wao hawana safari nyingi za nje kama kwetu na sidhani mishahara ya viongozi wao wa juu wa Serikali ina tofauti kubwa sana na ya kwetu. Je, kulikoni hawa hawana safari nyingi na ilhali na wao wanalipia kila kitu!? au wao hawapendi pochi kama viongozi wa Tanzania?
   
 10. M

  Mundu JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ...viongozi wa Tanzania wanatudharau wananchi. Wanajua hatuwezi kufanya chochote. Wanavurunda, na wataendelea kuvurunda. Sisi kimya tu. Hadi jamaa wa world bank na imf watusemee. Shame on all of us!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...