Benki ya Dunia: Masharti ya Mkopo tuliotoa ni kutolewa elimu kwa wasichana wote; Sheria ya Takwimu iangaliwe upya...

Jiwe ni so ignorant and unsophisticated katika masuala na mahusiano ya kimataifa.
Ujima wake unaonekana pale anapoomba
1) S Africa imuombee mikopo ya kujenga reli
2)Kumuomba Mfalme wa Morocco atujeengee uwanja wa michezo
3)Kumuomba Kagame wataalamu wa IT
Kumuomba W/Mkuu wa Ethiopia utaalamu wa kuendesha ATCL
Kumuomba kisichojulikana muuaji wa Wapalestina aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Israel (nasikia Tiss wamepewa mbinu za kiyahudi kudhibiti wananchi)
Augustine Mahiga ni kilaza mwingine asiyeweza kumshauri ya maana( ndio maana alitimuliwa UN)
 
Msimamo wa WB hamna ubabaishaji-> Dr Ghanem emphasized yesterday that it would only
support the $300million education project, only if girls
—whether pregnant or not—are given a chance to go
to school.
“Girls’ education is central to development. We cannot
accept that girls be denied education. We are a
development institution,’’ Dr Ghanem told journalists
in Dar es Salaam.
 
Anajua hata walichoongea basi? Ngosha lugha haipandi mkiambiwa sikieni. Saivi wana Lumumba wanapandisha nyuzi za kumsifia jiwe kuwa anakuza kiswahili kwa vile hotuba zake zote hutumia kiswahili bila ya kujua kuwa jiwe kiswahili hajui wala kiingereza hajui

Wasitumie kichaka cha kiswahili kumficha huyo jamaa asiejua kiswahili wala kiingereza
Kwa hiyo mkopo mpaka wenyewe wajiridhishe kupitia wataalamu wao ndio watatoa na sheria ya takwimu lazima ifanyiwe marekebisho...

Sasa mbona Ngosha hakuongea hayo juzi.? Alificha akijua itakuwa siri.?
 
Wiki 2 zilizopita benk ya Dunia ilitangaza kupitia vyombo mbali mbali vya habari Duniani kua imefuta mkopo wa Dollar Million 300 kwa Tanzania baada ya sera ya kuwafukuza watoto wanaopata ujauzito shuleni kutokutolewa ufafanuzi wa kueleweka pamoja na sheria ya takwimu.

Baadae juzi benki ya Dunia ikaridhia kuidhinishwa kuachiwa kwa hizo hela.

Akiongea na BBC Focus on Africa, waziri Mahiga amesema benki hiyo ilikubali kuachia pesa hizo baada ya serikali kuihakikishia kua inabuni njia mbadala ya kuwapatia elimu wabinti watakaopata ujauzito shuleni.

=======

Baada ya kuzungumza na Serikali, makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Kanda ya Afrika, Dk Hafez Ghanem amesema kuna masharti wamekubaliana kabla Tanzania haijapewa mkopo wa Dola 300 milioni za Marekani (Sh680.5 bilioni) kwa ajili ya kuboresha elimu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk Ghanem alisema benki hiyo inatoa fedha kwa ajili ya wasichana wote bila kujali hali zao, hivyo kuwatenganisha kwa kigezo cha ujauzito au kingine chochote ni kwenda kinyume na mkakati wa elimu jumuishi.

“Wataalamu wetu watashirikiana na Serikali kuona ilivyojiandaa kutoa elimu kwa wasichana wote. Tutakapojiridhisha bodi ya wakurugenzi itaidhinisha mkopo husika. Kuchelewa kwake kutategemea lini Serikali itatekeleza masharti tuliyokubaliana,” alisema.

Mkopo huo ilikuwa ujadiliwe na kuidhinishwa Oktoba 30, lakini kutokana na msimamo wa Serikali kutotoa fursa ya kuendelea na masomo wasichana wanaopata mimba, bodi ya benki hiyo ilisitisha kuujadili. Kwa utaratibu wa benki hiyo, kabla mradi wowote haujaidhinishiwa fedha zinazohitajika, huujadili kwanza.

“Mradi wa Tanzania haujajadiliwa. Lakini kwa mazungumzo tuliyofanya, utajadiliwa Serikali itakapotimiza masharti tuliyokubaliana,” alisema Dk Ghanem.

Baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, Rais John Magufuli alisema benki imekubali kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara, nyumba za walimu na vifaa vya kufundishia.

“Kwa hiyo, (Dk Hafez) amekuja kututhibitishia kuwa Benki ya Dunia haitatuacha,” alisema Rais Magufuli.

Vilevile, Dk Ghanem alisema walizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Takwimu na wameishauri Serikali kuhakikisha wadau wake wanakuwa huru kukusanya na kutumia takwimu.

Alisema WB haiwezi kufanya kazi bila takwimu ambazo zitakusanywa kwa uhuru, lakini masharti yaliyomo kwenye muswada, huenda yakazorotesha ufanisi wake.

Mabadiliko ya Muswada wa Takwimu yaliyofanyika mwaka huu na kuridhiwa na Bunge, yanazuia mtu au taasisi yoyote kukusanya, kutafsiri au kutumia takwimu lazima zithibitishwe na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Mwananchi

Ni yule tu asieelewa WB hufanyaje kazi zake (na ameamua kutohusisha ubongo wake kuchanganua mambo independently) ndie aliemuamini jiwe kuhusu mkopo huo kutolewa siku chache tu baada ya taarifa rasmi za benki zenye mwelekeo kinyume.

Kwa kifupi ni kuwa HAKUNA senti tutakayopewa unless masharti yametimizwa. Na ndicho alichokisema Makamu wa Rais wa WB (" the bank is still open for discussion").
 
Taarifa ya Benki ya Dunia iko wazi sana.

wamekubali kutoa fedha hizi baada ya sisi kukubali masharti yao, ushabiki wa kutotumia busara tuuache kwani tunajiangamiza sisi wenyewe, haihitaji benki ya Dunia waje watetee watoto wetu walio katika hatari ya kukosa haki yao ya msingi ya Elimu eti tu kwa sababu wamepewa ujauzito. Wakati unazuia huyo binti, baba au kujana aliyempa ujauzito yeye anenda kuwapa ujauzito mabinti wengine.

kulikuwa na walakini kutoa msimamo wa kuwakataza watoto wajawazito wasiendelee na shule. TULIKOSEA NA TUMEJIFUNZA

KAMA ukiangalia vizuri tamko la World Bank, mabadiliko yaliyowekwa kwenye sheria ya takwimu nayo yaondolewe " wameishauri serikali kuhakikisha wadau wake " WANAKUWA HURU KUKUSANYA NA KUTUMIA TAKWIMU, ALISEMA WB HAIWEZI KUFANYA KAZI BILA TAKKWIMU AMBAZO ZITAKUSANYWA KWA UHURU,... "
 
Back
Top Bottom